Anayedaiwa kutengeneza radi auawa na wananchi

Anayedaiwa kutengeneza radi auawa na wananchi

Huyo angekuwa mjanja angekuja dar , Radi moja angeuza laki moja
Ma ex wangetupiana sana radi
 
What a shame!Hili ndiyo Taifa ambalo limejengwa kwa miaka 60 ya uhuru ambapo watu wake bado wanaamini kuwa radi hutengenezwa na binadamu🚶🚶🚶
Angalau basi miaka 60 itupe uzalendo wa kuwaenzi wanasayansi wetu wa jadi. Ukatili haulipi
 
Katavi. Baraka Said (30) mkazi wa kijiji cha Mtisi halmashauri ya Nsimbo ameuawa na wananchi baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na kupigwa na kitu kizito kisogoni akituhumiwa kujihusisha na ushirikina wa kutengeneza radi.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 29, 2022 kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahimu amesema tukio hilo limetokea Januari 24, 2022 saa 12 jioni kijijini hapo.

Amesema wananchi hao walimtuhumu marehemu kutengeneza radi iliyompiga Anjelina Revocatus (16) mkazi wa kijiji hicho na kusababisha kifo chake wakati anatibiwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Katavi.

"Watuhumiwa nane wamekamatwa,John Mayonjuwa, Mashaka Mathias, Sele Richard, Revocatus Reymond, Julias Dalali, Hawa Rashid, Agnes Rashid na Tausi Abdu. Upelekezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Ibrahimu.

Katika tukio jingine Ibrahimu amesema nyumba 10 zilizojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kijiji cha Igongwe zimechomwa moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani.

Amesema tukio hilo limefanywa na baadhi ya wananchi wa Stalike waliojichukulia sheria mkononi wakigombania mashamba kati yao na kijiji cha Igongwe lililopelekea kifo cha Klisent Mwananjela (40) mkazi wa kijiji cha Stalike.


Wametupotezea mtaalam mvumbuzi kama Tesla.
Inabidi serikali ifikirie kuwaajirí watu hawa wawe wanatengeneza silaha ambazo tutazitumua kujilinda. Tunatuma radi moja inaenda kupiga fleet za ndege za F15 zilizopaki zikijiandaa kutushambulia 🤣🤣
 
Baraka Kabisu, mkazi wa Halmshauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi, ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni mchawi anayetengeneza radi, ambayo ilikwenda kumpiga Anjelina Revocatus na kufariki dunia. RPC Katavi amesema tukio hilo limetokea Januari 24, 2022
IMG_20220131_183936.jpg
 
Haya mambo hayana ushahidi ila yapo katika ulimwengu wa roho. Mpaka ukimwi unatengenezwa.
 
Back
Top Bottom