Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Bado naona unachangamoto kiroho mkuu. Rudi kwenye imani ya wazazi wako kwanza maana point namba 8 sijui kama kuna kanisa la machizi tu duniani ila ukiwa kwenye jamii yoyote ile kanisani kuna watu wote wenye akili na wasio na akili, maskini na tajiri na wote tunamlilia Mungu.

Sasa mkuu anzisha kanisa lako nadhani litakuwa na misingi unayotaka. Ila makanisa ya CCT ni bora zaidi na yanalea na kukuza imani kwa usahihi maana ni makanisa yenye mifumo ya LITRUJIA yaani maandalizi ya ibada na maungamo.
 
😀😀 yaani katika kanisa ambalo sijalielewa ni hilo aise. Mh!😷
Waumini wa kanisa katoliki msingi wake ni familia. Kama unaota na unaamka nataka kanisa LA kujiunga uje katoliki hutalielewa kamwe.

Kabla ya kujiunga kuna mafundisho rasmi then ndio ubatizwe. Haujiungi tu kwasababu unajisikia but lazima uelewae Catholic maanake nini na ukiri imani.
 
Kama msingi wake ni family basi sabato ndo baba lao mkuu
 
Hayo ni juu yako mkuu. Njoo tunywe bia mkuu[emoji23][emoji91][emoji91][emoji91] sisi huwaga hatuna shida ndogo ndogo... we pambana na imani yako. Sisi tunaipenda wenyewe.. View attachment 1788897
Kanisa inatakiwa iwe sehemu ya mtu kulelewa na kukua kiroho.....sasa kanisa ambalo kila mtu anatenda vile apendavyo lengo lake ni nini? Siwezi kwenda kanisa kama hilo bora nilale home
 
Kanisa inatakiwa iwe sehemu ya mtu kulelewa na kukua kiroho.....sasa kanisa ambalo kila mtu anatenda vile apendavyo lengo lake ni nini? Siwezi kwenda kanisa kama hilo bora nilale home
Kwamba hatukui kiroho ama? Hatulelewi ama?
 
Nenda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri hutajuta.
 
Kwa sifa hizo nami niungane na wale waliokushauri kujiunga na kanisa la Waadventista wa Sabato linakidhi hizo sifa zote na nyinginezo ambazo hujaziorodhesha
 
Liwe linasaidia Waamini kwa hali na mali ikiwemo kifedha badala ya lenyewe kukamua fedha waamini mpaka kutoka ngozi.
 
Kanisa ambalo limedhamiria kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na Wanadamu badala ya kuvaa kama wanaenda night clubs na Mchungaji wala hakemei sababu ya kujali sadaka zaidi kuliko utaua na kuridhika [emoji108][emoji108][emoji108]
 


Mi nalijua lipo moja ingawa sio la kikristo pekee mtu yoyote mwenye yafuatayo

hana Self consciousness
mwenye self esteem
hard work personality
ethical
unselfish, decent and honest person
noble person
self discipline and principled person

ukiwa na hayo hapo juu mengine yanayofanana na hayo basi utaweza kuishi katika mfumo ulioutaja hapo juu , huitaji kutegemea kikundi cha watu...

sababu hautapata kanisa unalolitaka ulivyovilist ni mfumo wa maisha sio taratibu za taasisi, zinaweza zikawa kwenye makaratasi ila belive me utekelezaji hautafika hata 50%

unless mkutane wote wenye vitu nilivyovitaja hapo juu ndo utapata hivyo ulivyolist.

ila sasa kila tasisi inaongozwa na principles... na kanisa muongozo wake mkubwa ni maswala
ya Mungu. so swala la nyie waumini wote kuwa na mindset ulizozitaja halipo sababu sio criteria zinazohitajika kwa mtu kujiunga na kanisa..

Mwisho Biblia inasema kanisa Sio jengo au tasisi, haya ya hapa duniani tu. Kanisa liko ndani yako.. ukikutana na mwingine mwenye maudhui kama yako basi ushatanua wigo wa kanisa lenu
 
Kanisa ni moja, katoliki la mitume.
Hili ndilo lililiweka liturujia inayofuatwa na makanisa yote yanayojiita ya kiroho.
 
Tafuta Jumba la ufalme la mashahidi wa Yehova.

Utarudi kunishukuru
 
Liwe na gari ya kukutoa nyumban mpaka kanisani na kukurudisha tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…