Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Kingereza chake ni kipi
 
Kanisa katoliki, niko hapa na baba paroko na waumini wenzangu tunapiga safari lager bariiiidi na kutafakari masomo ya dominika ya leo
Mbuzi katoliki zipo ? Na zile mbuzi katoliki za mirinda nazo zipo ,da wakatoliki mnakula raha yaani maustazi wanasubiri mabikira 70 mbinguni ila nyinyi mmejitengenezea wenyewe mnawaita masister[emoji23]
 
Kipindi nipo advance kuna haya makanisa mawili niliyaelewa vyema (kwa upande wangu )maana waumini wake nilivyokuwa nawaona wapo vyema sana

1. Reformers SDA
2. Full gospelπŸ™‚
Uko sahihi,Sda kama wangekuwa wanaabudu jpili ninhesali huko,full gospel kakobe akifa patachimbika ila namkubali sana yule mtumishi,
 
Hii ndio shida yao KUBWA halafu wanajionaga wanajua sana bible kumbe magarasa tu
 
Uko sahihi,Sda kama wangekuwa wanaabudu jpili ninhesali huko,full gospel kakobe akifa patachimbika ila namkubali sana yule mtumishi,
Wasabato yaani SDA sio wakristo ndio hawaadhimishi kuzaliwa kwa Yesu wala kufufuka kwake
 
Subiri kidogo ntaanzisha Kanisa lenye sifa hizo, nakusanya mtaji kwanza.
 
Kama unajua kuwa pombe ni mzizi wa dhambi kwaninj ikuhadae?

Vitu vyote ni halali ila si vyote vifaavyo
Vitu vyote ni halala, kinachotakiwa ni KIASI
Hata upendo ni mzur ila uwe na kiasi, upole, ukarimu n.k
Ukizidisha utaonekana zombie usiye na akili ya ulinganifu wa mambo
 
Chagua hapa kanisa unalotaka

1: RC hawa Ni wazee wa uongozi. hawajali Mambo mengi sana wala kufuatiliana fuatiliana, unaweza kunywa na kulewa na father meza moja, kula kitimoto hata ndani ya kanisa. Huku kumejaa taaluma ya uongozi na kuongoza Dunia, hii ni taasisi endelevu kubwa na yenye mtandao mpana kote Duniani. Ukijiunga hapa tegemea kuishi maisha yako halisi kabisa, Kama pombe kunywa Ila usilewe, utapata connection kibao, elimu ya utawala na uongozi, Uhuru usio na mipaka, utakuwa na maadui wa dini pande zote nne, fanya upendalo ndani ya yesu ukiwa RC, japo unaambiwa utii bila shuruti.

2: KKKT, Wazee wa injiri, hapa utakutana na watu wwnye uwezo mzuri wa kuhubili injiri. Hii Ni sifa kuu ya kanisa hili Kama unataka kufahamu vyema injiri jiunge na wa KKKT. Ukijiunga hapa tegemea kuwa na uchumi bora, mwerevu na mtu usiyeyumbishwa kiimani, starehe nyingi muhimu utafanya bila hofu nyingi Kama wengine, hapa nu furaha tu muda wote.

3: SDA, unataka kuwa mwimbaji? Hapa patakuhusu, karama kubwa zaidi ya kanisa hili ni kwenye uimbaji, achana na sehemu zote hapa kuimba kumepewa nguvu zaidi na ndio alama kuu ya kanisa hili. Ukijiunga hapa tegemea kuachana na Mambo mengi muhimu katika maisha yako, siku za kazi zitapungua, mawigi hautavaa tena, pombe sahau, jumapili kwako ndio jumamosi, jiandae na maisha ya mbinguni hapa hapa duniani.

4: JW Mashaidi wa yehova, Kama unataka kuchambuliwa chambuliwa neno na biblia yote nje ndani jiunge nao, hawa karama yao kubwa Ni uchambuzi.. aiseeutachambuliwa kila kifungu kigumu cha biblia. Ukijiunga hapa tegemea mabadiliko makubwa sana ya life style yako kuanzia uvaaji, uongeaji, teknolojia ndugu zako wanaweza kukusahau maana hawa jamaa wapo serious sana na ushahidi juu ya Imani yao, unaweza kujitenga na jamii usipokuwa makini.

4:Anglican, Bendela inayokosa uelekeo mzuri. Ukiwaacha wa RC hawa jamaa walipaswa wafanane kwa ukaribu sana na kanisa hilo la kwanza kuanzishwa, shida yao kubwa ni kushindwa kuitumia vyema karama ya uongozi na mwishowe kubaki kuwa Kama Bendela, japo usiri Ni karama yao tukuka zaidi. Yaani fuata kilichokuleta. Ukijiunga hapa tegemea kuwa imara kimikakati na nguvu ya ushindani, uchumi imara na roho ngumu yakutokuyumbishwa yumbishwa na watu.

5: Wapentekoste wote ( TAG na ndugu zao wote) Ukiachana na uchonganishi chonganishi, hawa jamaa karama yao kubwa ni ku-boost boost kila jambo lililosahaulika ama kupuuziwa na makanisa mengine yote, yaani hawa kila siku wanaangalia wapige wapi? Ukijiunga nao hawa tegemea kufa masikini au kuishi maisha ya mateso bila kugusa starehe nyingi zilizopo hapa duniani kwa kigezo cha wokovu na kuokoka.

6: Mitume na manabii, Ukisikia wafanya biashara wakubwa wa kubwa au wajasiliamali wa dini, hapo umefika sehemu yake, hawa kalama yao kubwa zaidi ni biashara tu. Ukijiunga nao tegemea zaidi either uwe mwekezaji siku za usoni au ugeuzwe chanzo cha mapato ya ndugu nabii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…