Biblia inasema sala inapaswa kwenda kwa Mungu kupitia Yesu Kristo tu( Yohana14:6) sasa kwanini mnamuhusisha Maria ni wapi Biblia inasema tusal kuptia Maria?
KWANINI WAKATOLIKI TUNAMHESHIMU BIKIRA MARIA?
•Maria ni Nani?
Maria ndiye mama mzazi wa Yesu Kristu (Luka 1:30-31,Mathayo 1:18-25)
Kwahiyo Yesu Kristu ni mtoto halisi wa Mariam.
•Kwanini Tunamhesimu?
Biblia inajibu kama ifuatavyo
(i)Tunaambiwa na Malaika kwamba amejaa Neema.
Luka 1:28,30
(ii)Alimzaa mtakatifu wa Mungu au kwa lugha nyingine mwana wa Mungu
Luka 1:31-33
(iii)Wakristo wa kwanza walimheshimu na walimshirikisha katika sala na mafungo yao.Kwanini na sisi tusimshirikishe na kumheshimu!
Matendo 1:14
(iv)Katika hali ya kumtukuza Mungu,alikiri kuwa 'Tangu sasa tutamwita Mwenye Heri'
Luka 1:48
(v)Elisabethi hali akijawa roho mtakatifu alimshuhudia na kumwita 'amebarikiwa kuliko wanawake wote'
Luka 1:41-45
(vi) Yesu mwenyewe mwana wa Mungu alitukabidhi kwetu kupitia kwa Yohane mwanafunzi aliyempenda
Yohane 19:25-27
Kwa uthibitisho huu wa kimaandiko sina shaka kuwa Maria ni Miongino mwa Watakatifu walioheshimina miongoni mwa Mitume tokea kanisa la kwanza.
Na ndivyo hivyo na sisi wakatoliki wa leo tunavyopaswa.
Ikumbukwe, wakatoliki hatufanyi IBADA KUMWABUDU BIKIRA MARIA,bali tunafanya ibada za maombezi kupitia kwa birika maria kwenda kwa Mwanae Yesu kristo kama wale wayahudi walivyofanya kule Kana ya Galilaya walipoishiwa divai katika harusi ile (Yohane 2:1-12).