Anayefahamu maudhui ya tamthilia ya saloon ya mama Kimbo kwa kizazi kijacho anijuze

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Leo jioni nikiwa kwenye kijiwe/kidukabia cha Manka hapa mtaani hasa mida kama hii nalazimika kuangalia kile wanachoangalia wateja wengine.

Basi bwana kikakuta tamthilia ya saluni ya mama Kimbo Ila kila nikiangalia sioni mafunzo chanya ya kizazi kijacho nikajiuliza hivi haka katoto kanachoigiza umbea na haya mashangingi mnauhakika baadae katabadilika?

Na huyu mwanamme m'mbeya anayeshinda na wanawake muda wote na anajisifua yeye umbea haachi, sio ndio atapelekwa mtaa wa 'Mpalange' hapo Buza?

kama kuna anayeelewa any +ve influence/teachings that will be built by this series anijuze.

Naona kama uovu unapigiwa chapuo sana humu.

Nawasilisha haya nikiwa na masikitiko sana.
 
Funzo usikae uswaz buza yatakukuta mambo ushangae, kaa huko ushuani masaki na obey uokoe kizazi chako
 
Mkuu sisi wazazi tunawaza kizazi kijacho aisee😡😡
 
Nadhani wazaramo watakua wanajua mafunzo yanayopatikana huko. Ukiona huoni mafunzo lakini wanaisifia basi ujue haikuhusu.
Mmmh so watoto huku Simiyu nao ni wazaramo?🤔🤔
 
Mkuu sisi wazazi tunawaza kizazi kijacho aisee[emoji35][emoji35]
Yeah.. tamthiliya ime portray uhuni kana kwamba ni kitu cha kujivunia,uswahili,wizi, umalaya NK

Pia buza Kama buza imepewa sofa mbaya,wasioijua buza wanaweza kudhani ni sehemu isiyofaa kuishi lkn Stori ni tofauti ukifika

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Asante mkuu kwa mawazo mujarabu, hii inapotosha sana hasa ukijua nguvu na utandawazi
 
Hichi kin'gamuzi ni udini sana .....kufundisha watoto kushika mapanga na mambo ya kishog@ sana.....angalia tamthilia zao nyingi haya mambo yamo......(ushoga,ugaidi na udini)
 
Hichi kin'gamuzi ni udini sana .....kufundisha watoto kushika mapanga na mambo ya kishog@ sana.....angalia tamthilia zao nyingi haya mambo yamo......(ushoga,ugaidi na udini)
Mkuu unahama mada, mimi nauliza mada ya Saluni ya Mama Kimbo, mambo mengine achana nayo, jikite kwenye mada
 
Mama kimbo kama upo humu ni pm, asiye mama kimbo asinitafute tafadhari,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…