Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Maudhui yake ni ujingaujinga.Hawana uwezo wa kupangilia visa endelevu.Kwa nini?Huwa napenda wanachokiangalia watoto wangu kukifuatilia.Niliangalia nikagundua ni mipumbafu fulani ambayo haiongei kwa utuo na inapiga mikelele kwa kuvaa hovyohovyo.Wabadilishe muongozaji.Kuna wakati nikiwa kwenye kijiwe/kidukabia cha Manka hapa mtaani hasa mida kama hii nalazimika kuangalia kile wanachoangalia wateja wengine.
Ila kila nikiangalia sioni mafunzo +ve ya kizazi kijacho, hivi haka katoto kanachoigiza umbea na mashangingi mnauhakika baadae katabadilika?
Na huyu mwanamme m'mbeya anayeshinda na wanawake muda wote sio ndio atapelekwa mtaa wa 'Mpalange'?
kama kuna anayeelewa any +ve influence that will be built by this series anijuze.
Naona kama UOVU UNAPIGIWA CHAPUO SANA HUMU.
Nawasilisha nikiwa na masikitiko sana