Anayehitaji msaada wa mambo ya kodi

Anayehitaji msaada wa mambo ya kodi

Ili kuwa vizuri katika masuala ya sheria inakupasa uijue sheria yenyewe inasemaje. Umeniuliza TRA wana deal nayo vipi suala la Deferred taxation ni vizuri nikujibu kwa mujibu wa sheria inavyosema na si TRA wana deal nayo vip maana wanaweza kuwa wanakosea. Subiri nitakujibu muda si mrefu sheria yasema nini kuhusu deferred tax.

I remain kiongozi,
 
Je,mfanyakazi wa serikali anayekatwa paye(kodi) kupitia mshahara wake ana haki ya kutowalipa TRA kama anabiashara yeyote ile?
 
[TABLE="class: cms_table, align: left"]
[TR]
[TD]Gratuity ya Shilingi 2.5 milioni inaangukia katika wigo wa kodi wa kati ya shilingi 720,000 –Na zaidi ambao kodi ni sh 103,800 jumliosha 30% ya ziada ya sh 720,000
Kwa hiyo ukikokotoa kwa kutumia kanuni hapo juu utapata jumla ya kodi. Suala la kodi kuwa kubwa kwenye kipato kikubwa ni suala la kisera. Uzuri muundo wa serikali ya Tanzania ni mzuri kuanzia ngazi ya chini kabisa. Muone diwani wako aliwasilishe ngazi ya wilaya mpaka ngazi ya taifa litafika. Inawezekana kabisa kwa kulizungumzia ngazi husika sera inaweza kubadilishwa na kodi ikawa nafuu kwa wanaopokea mishahara na marupurupu.[/TD]
[TD]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

mkuu nakushukuru sana kwa majibu yako mazuri ila ninachokiona hapa ni kuwa huu mfumo wetu wa kodi sio rafiki kabisa wa sisi watu wa kipato cha chini,kingine mkuu inakuaje kwa mtu anayepokea kiinua mgongo chake baada ya kutumikia wadhifa Fulani kwa miaka 30 mpk 35 yule naye akipokea pesa yake inakatwa kodi?
 
Kiinua mgongo kinatozwa kodi mkuu (kwa mujibu wa kifungu cha 7(2)(d) cha sheria ya kodi ya mapato).
Wahasibu na Tax consultants wanashindwa kutofautisha retirement contributions na retirement payments. Ni vitu viwili tofauti! Retirement contribution ni hela anayoipeleka mwajiri kwenye mifuko ya jamii (ambayo hela hiyo haikatwi kodi kwa mujibu wa kifungu cha 61 cha sheria ya kodi ya mapato). Wakati retirement payments ni pesa unayolipwa na mfuko kama kiinua mgongo (na si mchango ulioupeleka wewe 10% kujumlisha na 10% aliyopeleka mwajiri) Kiinua mgongo kinatozwa kodi chini ya kifungu cha 7(2)(d) cha sheria hiyo kama nilivyosema hapo juu.
Ingawa retirement contributions nazo zitatozwa kodi ikiwa pesa hiyo imezaa riba (interest). Ni interest iliyozaliwa ndiyo itakayotozwa kodi na si ile hela (principal amount). Na hii tunaona katika kifungu cha 63 cha sheria ya kodi ya mapato.
Umenipata hapo mkuu?
 
Je,mfanyakazi wa serikali anayekatwa paye(kodi) kupitia mshahara wake ana haki ya kutowalipa TRA kama anabiashara yeyote ile?

Hapaswi kukataa.
Kuna aina tatu za kipato zinazotozwa kodi
1. Kipato kutokana na ajira (Income from Emplaoyment chini ya kifungu cha 7 cha sheria ya kodi ya mapato 2004)
2. Kipato kutokana na biashara (Income from Busines chini ya kifungu cha 8 cha sheria ya kodi ya mapato 2004)
3. Kipato kutokana na uwekezaji ((Income from Investment chini ya kifungu cha 9 cha sheria ya kodi ya mapato 2004)

Kwa hiyo kama umelipa PAYE kimsingi unakuwa umelipia chanzo kimoja tu cha kipato kama una biashara nyingine. Hiyo biashara nyingine itatozwa kodi kwa kifungu cha 8 ama cha 9 kutegemeana ni biashara ya kuuza ama ni uwekezaji.
Kifungu cha 5(2) cha sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 kinataka kila chanzo cha kipato kitozwe kodi bila kuchanganya na chanzo kingine.
 
hivi AMCOS hutakiwa kulipa kodi kikifikisha ushuru unaotokana na mazao unaofikia shilingi ngapi?
 
Kiinua mgongo kinatozwa kodi mkuu (kwa mujibu wa kifungu cha 7(2)(d) cha sheria ya kodi ya mapato).
Wahasibu na Tax consultants wanashindwa kutofautisha retirement contributions na retirement payments. Ni vitu viwili tofauti! Retirement contribution ni hela anayoipeleka mwajiri kwenye mifuko ya jamii (ambayo hela hiyo haikatwi kodi kwa mujibu wa kifungu cha 61 cha sheria ya kodi ya mapato). Wakati retirement payments ni pesa unayolipwa na mfuko kama kiinua mgongo (na si mchango ulioupeleka wewe 10% kujumlisha na 10% aliyopeleka mwajiri) Kiinua mgongo kinatozwa kodi chini ya kifungu cha 7(2)(d) cha sheria hiyo kama nilivyosema hapo juu.
Ingawa retirement contributions nazo zitatozwa kodi ikiwa pesa hiyo imezaa riba (interest). Ni interest iliyozaliwa ndiyo itakayotozwa kodi na si ile hela (principal amount). Na hii tunaona katika kifungu cha 63 cha sheria ya kodi ya mapato.
Umenipata hapo mkuu?

mkuu nimekupata,kumbe ile principle haitozwi kodi bali interest ndio inakatwa kodi,thanks a lot mkuu nimekusoma.
 
Nisaidie kama nataka kufungua duka la mtaj wa laki saba nalipa kodi bei gani? Hapo umesema mtaji haukatwi kodi wakat mi nlivyofungua duka majiran wananiambia bila kulipa kodi tra watakuja kufunga? Hembu nisaidie kabla ya kufungua duka hujaanza kuuza kuna haja ya kwenda tra?
 
Kuna kitu kinaitwa "presumptive taxation". Hii ni aina ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wenye mauzo yasiyozidi milioni 20 na pia hawana uwezo wa kutengeneza mahesabu (kuajiri certifified public accountant kutengeneza mahesabu). Hawa wanalipa kodi kwa kukadiriwa. Makadirio hayo yanafanyika mara unapoanza biashara unatakiwa kwenda TRA kuomba kukadiriwa. Sheria ya kodi ya mapato kifungu cha 133 kinasema ukishaanza biashara ndani ya wiki mbili unatakiwa kwenda TRA kupata kitambulisho ya mlipa kdodi yaani TIN. Sasa wakati wa kupewa TIN ndipo unakadiriwa. makadirio si kwa mtaji ulio nao bali kwa mategemeo utauza shilingi ngapi kwa mwaka.
Kwa hiyo baada ya kujua utauza sh ngapi kwa mwaka kodi ndipo inakadiriwa kutozwa. Kuna viwango vimewekwa.

Mfano

[TABLE="width: 491"]
[TR]
[TD]MAUZO KWA MWAKA[/TD]
[TD]KIWANGO CHA KODI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 4 lakini hayazidi Milion 7.5[/TD]
[TD]Sh 200,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 7.5 lakini hayazidi Milion 11.5[/TD]
[TD]sh 424,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 11.5 lakini hayazidi Milion 16[/TD]
[TD]sh 728,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 16 lakini hayazidi Milion 20[/TD]
[TD]sh 1,150,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Zaidi ya Milioni 20 unapaswa utengeneze mahesabu[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mkuu hiyo kodi ya kamisheni anayelipa ni kampuni inayotoa huduma ya simu yaani vodacom, Airtel, Tigo nk. Kwa hiyo wakala anapolipwa pesa yake anakuwa amepata kipato kipya yaani anaangukia kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya kodi ya mapato kinachosema mtu atalipa kodi ikiwa anakipato.......
Kwa hiyo huyu wakala akishapokea pesa zake anakuwa amepata kipato sasa. kabla ya hapo pesa hiyo ilikuwa bado mikononi mwa kampuni ya simu.
Kama hujanielewa niulize tena.

Lakini mkuu pamoja na hayo wakala wakati anatumiwa/anapopokea kamisheni inaonyesha kuwa pesa hiyo tayari imeshakatwa kodi. Kwanini bado analazimika kulipa kodi? Mfano, ukinunua vocha ya kukwangua duka la reja reja kuna haja ya kwenda TRA kulipia tena kodi ya vocha uliyonunua?
 
vyama vya ushirika vya msingi( agricultural marketing cooperative societies)

Very good! Sasa nimekuelewa.
Vyama vya ushirika vya msingi vimesamehewa kodi ikiwa mauzo yake hayajazidi Tshs 50,000,000 (milioni hamsini) kwa mwaka. Hii inapatikana kwenye jedwali la pili (second schedule to the Income Tax act, 2004) aya ya (g). Maana yake yakizidi kiasi hicho chama cha ushirika kitalipa kodi. Ama kwa lugha nyingine shilingi milioni 50 zimesamehewa na kiasi kinachozidi kinatozwa yaani threshhold ili uitoze kodi chama cha ushirika ni hicho cha sh milion 50.
Nimekujibu mkuu.
 
Lakini mkuu pamoja na hayo wakala wakati anatumiwa/anapopokea kamisheni inaonyesha kuwa pesa hiyo tayari imeshakatwa kodi. Kwanini bado analazimika kulipa kodi? Mfano, ukinunua vocha ya kukwangua duka la reja reja kuna haja ya kwenda TRA kulipia tena kodi ya vocha uliyonunua?

Uliuliza kipato cha watu wanaofanya biashara ya tigo pes, M-pesa nk. Nikakujibu kwamba hiyo ni pesa imekatwa mikononi mwa kampuni ya simu. Leo umeliuliza vizuri swali lako nimekuelwa tofauti na mara ya kwanza kwamba wakala anapopokea pesa inakuwa imekatwa kamisheni. Usahihi ni kwamba hiyo kamisheni inakuwa ni tax deducted at source ama kwa uzuri nikufahamishe kodi hii itatolewa kwenye faida yako wakati wa kutengeneza hesabu. Kwa hiyo kiasi kitakachobaki ndipo unatakiwa kulipa kodi na si faida yote uilipie kodi wakati tayari umeshalipa kiasi fulani. Inapaswa ukitoe ili ubaki na kiasi ambacho kinakuwa bado hakijatozwa.
Ukinunua vocha ukaikwangua huwezi kwenda TRA kulipa kodi maana tayari unakuwa umeshalipa kodi. Ile bei ya vocha na kodi imo. Vocha ama chakula ama nguo ama viatu ukinunua tayari kodi inakuwamo. Vitu hivi nilivyovitaja vimo katika orodha ya vitu kodi yake unailipa ukinunua yaani consumption tax ambayo kimsingi ni indirect tax. All indirect taxes are consumption taxes.
 
saccos zinatakiwe zilipe kodi zikiwa na mapato kuanzia kiasi gani?

SACCOS zimo kwenye orodha ya kampuni zinazofanya biashara kwa hiyo kutozwa kodi chini ya kifungu cha 8 cha sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004. Kama SACCOS hiyo ipo kwa madhumuni ya kuondoa umaskini basi itatozwa kodi chini ya kifungu cha 64 cha sheria hiyo. Kabla ya kufanya hivyo SACCOS inatakiwa kuomba kwa maandishi kwamba madhumuni yake ni kuondoa umaskini miongoni mwa jamii kama kifungu cha 64 kinavyosema. maombi hayo yafanyike kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Kanuni za shria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004.
Hata hivyo SACCOS nyingi zimesajiliwa chini ya sheria ya makampuni y amwaka 2002 sura ya 212 hivyo kutafsirika kuwa ni kampuni kama kampuni zingine. Kutafsrika kama Charitable organization inakuwa ngumu kidogo.
NB usijali spelling maana nina presha najibu watu wengi sana hivyo nakosa muda wa kusahihisha makosa ya spelling.
 
Uliuliza kipato cha watu wanaofanya biashara ya tigo pes, M-pesa nk. Nikakujibu kwamba hiyo ni pesa imekatwa mikononi mwa kampuni ya simu. Leo umeliuliza vizuri swali lako nimekuelwa tofauti na mara ya kwanza kwamba wakala anapopokea pesa inakuwa imekatwa kamisheni. Usahihi ni kwamba hiyo kamisheni inakuwa ni tax deducted at source ama kwa uzuri nikufahamishe kodi hii itatolewa kwenye faida yako wakati wa kutengeneza hesabu. Kwa hiyo kiasi kitakachobaki ndipo unatakiwa kulipa kodi na si faida yote uilipie kodi wakati tayari umeshalipa kiasi fulani. Inapaswa ukitoe ili ubaki na kiasi ambacho kinakuwa bado hakijatozwa.
Ukinunua vocha ukaikwangua huwezi kwenda TRA kulipa kodi maana tayari unakuwa umeshalipa kodi. Ile bei ya vocha na kodi imo. Vocha ama chakula ama nguo ama viatu ukinunua tayari kodi inakuwamo. Vitu hivi nilivyovitaja vimo katika orodha ya vitu kodi yake unailipa ukinunua yaani consumption tax ambayo kimsingi ni indirect tax. All indirect taxes are consumption taxes.

Maelezo yako ni mazuri lkn nilikuquote kwenye point uliyosema kwamba iyo kamisheni anayopata wakala mwisho wa mwezi inakuwa ishakatwa kodi kupitia mtandao wa simu. So hayo maelezo uliyonipa sasa ndo napata nayo shida kuona TRA bado inahitaji kushikana shati na wakala kuchukua iko kidogo alichopata. Inaumiza kichwa asee
 
Nilisema hivi"

Mkuu hiyo kodi ya kamisheni anayelipa ni kampuni inayotoa huduma ya simu yaani vodacom, Airtel, Tigo nk. Kwa hiyo wakala anapolipwa pesa yake anakuwa amepata kipato kipya yaani anaangukia kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya kodi ya mapato kinachosema mtu atalipa kodi ikiwa anakipato.......
Kwa hiyo huyu wakala akishapokea pesa zake anakuwa amepata kipato sasa. kabla ya hapo pesa hiyo ilikuwa bado mikononi mwa kampuni ya simu.
Kama hujanielewa niulize tena.

Wapi panakuumiza kichwa?
 
Back
Top Bottom