Anayehitaji msaada wa mambo ya kodi

Anayehitaji msaada wa mambo ya kodi

MALYENGE! MUNGU akubaliki sana japo kwenye saccos umeweka kona nyingi ila umepambanua vizuri sana kwenye AMCOS.Kuwa na usiku mwema.
 
Nilisema hivi"

Mkuu hiyo kodi ya kamisheni anayelipa ni kampuni inayotoa huduma ya simu yaani vodacom, Airtel, Tigo nk. Kwa hiyo wakala anapolipwa pesa yake anakuwa amepata kipato kipya yaani anaangukia kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya kodi ya mapato kinachosema mtu atalipa kodi ikiwa anakipato.......
Kwa hiyo huyu wakala akishapokea pesa zake anakuwa amepata kipato sasa. kabla ya hapo pesa hiyo ilikuwa bado mikononi mwa kampuni ya simu.
Kama hujanielewa niulize tena.

Wapi panakuumiza kichwa?

Siku zote nilikuwa najua ile kamisheni ikishatolewa kwa wakala inakuwa kodi ishakatwa so wewe kama wakala unaendelea na biashara tu bila kuhangaika na TRA.
Nashkuru kwa darasa mkuu.
Umenifumbua macho, ntawajulisha na wengine.
 
Siku zote nilikuwa najua ile kamisheni ikishatolewa kwa wakala inakuwa kodi ishakatwa so wewe kama wakala unaendelea na biashara tu bila kuhangaika na TRA.
Nashkuru kwa darasa mkuu.
Umenifumbua macho, ntawajulisha na wengine.

Nashukuru mkuu. Mkuu unajua nchi hii wataalam wa kodi ni wachache sana! Wanasoma kodi kama somo na si kama kozi. Na hata wale wanaosoma kodi hawaisomi kama ni taaluma ya sheria. Wanaisoma kama maelezo tu na si tafsiri ya kisheria wakiamini kodi si sheria. They are wrong! Kwa kuwa umeelewa nashukuru. Tuendelee kuelimishana in future.
 
Asante sana. Nimekupa like hapo. Kazi nzuri sana.
Hii ndo inamaanisha great thinkers kinaga ubaga.

Endelea kuwaelimisha wengi wengi zaidi ili wafaham zaidi
 
Kuna kitu kinaitwa "presumptive taxation". Hii ni aina ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wenye mauzo yasiyozidi milioni 20 na pia hawana uwezo wa kutengeneza mahesabu (kuajiri certifified public accountant kutengeneza mahesabu). Hawa wanalipa kodi kwa kukadiriwa. Makadirio hayo yanafanyika mara unapoanza biashara unatakiwa kwenda TRA kuomba kukadiriwa. Sheria ya kodi ya mapato kifungu cha 133 kinasema ukishaanza biashara ndani ya wiki mbili unatakiwa kwenda TRA kupata kitambulisho ya mlipa kdodi yaani TIN. Sasa wakati wa kupewa TIN ndipo unakadiriwa. makadirio si kwa mtaji ulio nao bali kwa mategemeo utauza shilingi ngapi kwa mwaka.
Kwa hiyo baada ya kujua utauza sh ngapi kwa mwaka kodi ndipo inakadiriwa kutozwa. Kuna viwango vimewekwa.

Mfano


[TABLE="width: 491"]
[TR]
[TD]MAUZO KWA MWAKA[/TD]
[TD]KIWANGO CHA KODI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 4 lakini hayazidi Milion 7.5[/TD]
[TD]Sh 200,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 7.5 lakini hayazidi Milion 11.5[/TD]
[TD]sh 424,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 11.5 lakini hayazidi Milion 16[/TD]
[TD]sh 728,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 16 lakini hayazidi Milion 20[/TD]
[TD]sh 1,150,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Zaidi ya Milioni 20 unapaswa utengeneze mahesabu[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Umenisaidia sana mkuu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kuna mtaalamu mmoja wa Kodi alisema "Tax is not always proportionate rather is progressive" Naomba ufafanuzi mtaalamu huyo alikuwa ana maanisha nini?
 
Kuna mtaalamu mmoja wa Kodi alisema "Tax is not always proportionate rather is progressive" Naomba ufafanuzi mtaalamu huyo alikuwa ana maanisha nini?
Mkuu nyelesa umeona kichwa cha mada hapo juu? Tunajadili sheria za kodi na si principles za kodi. Maana principles za kodi si sheria. Stick to the topic please!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Malyenge naomba kuuliza swali la awali kabisa,Kwanza kuna aina ngapi za kodi zinazopaswa mwananchi kulipa Tanzania? Nnavyojua kuna VAT,PAYE na zipi?

Naomba mchanganuo tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Malyenge naomba kuuliza swali la awali kabisa,Kwanza kuna aina ngapi za kodi zinazopaswa mwananchi kulipa Tanzania? Nnavyojua kuna VAT,PAYE na zipi?

Naomba mchanganuo tafadhali.

Mkuu nemulo hebu liweke vizuri swali lako. Huyo mwananchi uliyemkusudia ni yupi? Maana kwa ninavyojua ukisema "mwananchi" ulikusudia mtu ama kampuni raia wa Tanzania. Kitu ambacho kwa sheria za kodi sivyo......Kila mtu anapaswa kulipa kodi bila kujali ni Mwananchi wa tanzania ama la.
Pia swali lako lina ambiguity kwa maana hujafafanua huyo "mwananchi" anashughuli gani mpaka apate kulipa hiyo kodi. Huwezi kusema mwananchi aliyeajiriwa alipe kodi ya corporate tax wakati hana kampuni. Hebu liweke vizuri swali.
Kwa kukusaidia kuna vyanzo vitatu vya kutoza kodi navyo ni pato litokanalo na ajira, pato litokanalo na biashara na pato litokanalo na uwekezaji. Ukichagua aina ya pato hapo ninaweza kukutajia idadi ya kodi inayopaswa kulipwa kutokana na aina ya chanzo.
 
[TABLE="class: cms_table, align: left"]
[TR]
[TD]Mkuu sirdelta nilishaweka formula huko nyuma. Tazama #3 huko juu kisha pachika mshahara wako na utapata jibu.
Niliweka formula hii (si ya kutunga bali iko kwenye jedwali la kwanza la sheria ya kodi ya mapato 2004)


SHAHARA KWA MWEZI[/TD]
[TD]



KIWANGO CHA KODI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 0 –Mpaka shilingi 170,000[/TD]
[TD]HAKUNA yaani mshahara huo umesamehewa kodi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 170,000 –Mpaka shilingi 360,000[/TD]
[TD]Kodi ni 12% ya ziada ya shs 170,0000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 360,000 –Mpaka shilingi 540,000[/TD]
[TD]Kodi ni sh 22,800 kujumlisha 20% ya ziada ya 360,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 540,000 –Mpaka shilingi 720,000[/TD]
[TD]Kodi ni sh 58,800 kujumlisha25% ya ziada ya 540,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 720,000 –Na zaidi[/TD]
[TD]Kodi ni sh 103,800 kujumlisha 30% ya ziada ya 720,000

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Last edited by a moderator:
habari
vp kwa mtu anaeanza biashara,anahitajika afanye biashara kwa muda kdg (miezi 6)ndio aanze kulipa mapato au ni lazima akadiriwe kodi kwanza ndio aanze biashara,na je anakadiriwa nn wakati hajaifanya hy biashara? sheria ya kodi ikoje
 
Back
Top Bottom