kuku wa kienyeji
JF-Expert Member
- Apr 9, 2012
- 494
- 151
Ili kuwa vizuri katika masuala ya sheria inakupasa uijue sheria yenyewe inasemaje. Umeniuliza TRA wana deal nayo vipi suala la Deferred taxation ni vizuri nikujibu kwa mujibu wa sheria inavyosema na si TRA wana deal nayo vip maana wanaweza kuwa wanakosea. Subiri nitakujibu muda si mrefu sheria yasema nini kuhusu deferred tax.
[TABLE="class: cms_table, align: left"]
[TR]
[TD]Gratuity ya Shilingi 2.5 milioni inaangukia katika wigo wa kodi wa kati ya shilingi 720,000 Na zaidi ambao kodi ni sh 103,800 jumliosha 30% ya ziada ya sh 720,000
Kwa hiyo ukikokotoa kwa kutumia kanuni hapo juu utapata jumla ya kodi. Suala la kodi kuwa kubwa kwenye kipato kikubwa ni suala la kisera. Uzuri muundo wa serikali ya Tanzania ni mzuri kuanzia ngazi ya chini kabisa. Muone diwani wako aliwasilishe ngazi ya wilaya mpaka ngazi ya taifa litafika. Inawezekana kabisa kwa kulizungumzia ngazi husika sera inaweza kubadilishwa na kodi ikawa nafuu kwa wanaopokea mishahara na marupurupu.[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
mkuu nakushukuru sana kwa majibu yako mazuri ila ninachokiona hapa ni kuwa huu mfumo wetu wa kodi sio rafiki kabisa wa sisi watu wa kipato cha chini,kingine mkuu inakuaje kwa mtu anayepokea kiinua mgongo chake baada ya kutumikia wadhifa Fulani kwa miaka 30 mpk 35 yule naye akipokea pesa yake inakatwa kodi?
Je,mfanyakazi wa serikali anayekatwa paye(kodi) kupitia mshahara wake ana haki ya kutowalipa TRA kama anabiashara yeyote ile?
Kiinua mgongo kinatozwa kodi mkuu (kwa mujibu wa kifungu cha 7(2)(d) cha sheria ya kodi ya mapato).
Wahasibu na Tax consultants wanashindwa kutofautisha retirement contributions na retirement payments. Ni vitu viwili tofauti! Retirement contribution ni hela anayoipeleka mwajiri kwenye mifuko ya jamii (ambayo hela hiyo haikatwi kodi kwa mujibu wa kifungu cha 61 cha sheria ya kodi ya mapato). Wakati retirement payments ni pesa unayolipwa na mfuko kama kiinua mgongo (na si mchango ulioupeleka wewe 10% kujumlisha na 10% aliyopeleka mwajiri) Kiinua mgongo kinatozwa kodi chini ya kifungu cha 7(2)(d) cha sheria hiyo kama nilivyosema hapo juu.
Ingawa retirement contributions nazo zitatozwa kodi ikiwa pesa hiyo imezaa riba (interest). Ni interest iliyozaliwa ndiyo itakayotozwa kodi na si ile hela (principal amount). Na hii tunaona katika kifungu cha 63 cha sheria ya kodi ya mapato.
Umenipata hapo mkuu?
Nisaidie kama nataka kufungua duka la mtaj wa laki saba nalipa kodi bei gani? Hapo umesema mtaji haukatwi kodi wakat mi nlivyofungua duka majiran wananiambia bila kulipa kodi tra watakuja kufunga? Hembu nisaidie kabla ya kufungua duka hujaanza kuuza kuna haja ya kwenda tra?
Mkuu nifafanulie hiyo AMCOS nini kisha nitakufahamisha.
Uliza swali vizuri mkuu nikuelewe......
Mkuu hiyo kodi ya kamisheni anayelipa ni kampuni inayotoa huduma ya simu yaani vodacom, Airtel, Tigo nk. Kwa hiyo wakala anapolipwa pesa yake anakuwa amepata kipato kipya yaani anaangukia kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya kodi ya mapato kinachosema mtu atalipa kodi ikiwa anakipato.......
Kwa hiyo huyu wakala akishapokea pesa zake anakuwa amepata kipato sasa. kabla ya hapo pesa hiyo ilikuwa bado mikononi mwa kampuni ya simu.
Kama hujanielewa niulize tena.
vyama vya ushirika vya msingi( agricultural marketing cooperative societies)
Lakini mkuu pamoja na hayo wakala wakati anatumiwa/anapopokea kamisheni inaonyesha kuwa pesa hiyo tayari imeshakatwa kodi. Kwanini bado analazimika kulipa kodi? Mfano, ukinunua vocha ya kukwangua duka la reja reja kuna haja ya kwenda TRA kulipia tena kodi ya vocha uliyonunua?
saccos zinatakiwe zilipe kodi zikiwa na mapato kuanzia kiasi gani?
Uliuliza kipato cha watu wanaofanya biashara ya tigo pes, M-pesa nk. Nikakujibu kwamba hiyo ni pesa imekatwa mikononi mwa kampuni ya simu. Leo umeliuliza vizuri swali lako nimekuelwa tofauti na mara ya kwanza kwamba wakala anapopokea pesa inakuwa imekatwa kamisheni. Usahihi ni kwamba hiyo kamisheni inakuwa ni tax deducted at source ama kwa uzuri nikufahamishe kodi hii itatolewa kwenye faida yako wakati wa kutengeneza hesabu. Kwa hiyo kiasi kitakachobaki ndipo unatakiwa kulipa kodi na si faida yote uilipie kodi wakati tayari umeshalipa kiasi fulani. Inapaswa ukitoe ili ubaki na kiasi ambacho kinakuwa bado hakijatozwa.
Ukinunua vocha ukaikwangua huwezi kwenda TRA kulipa kodi maana tayari unakuwa umeshalipa kodi. Ile bei ya vocha na kodi imo. Vocha ama chakula ama nguo ama viatu ukinunua tayari kodi inakuwamo. Vitu hivi nilivyovitaja vimo katika orodha ya vitu kodi yake unailipa ukinunua yaani consumption tax ambayo kimsingi ni indirect tax. All indirect taxes are consumption taxes.
Maelezo yako ni mazuri lkn nilikuquote kwenye point uliyosema kwamba iyo kamisheni anayopata wakala mwisho wa mwezi inakuwa ishakatwa kodi kupitia mtandao wa simu. So hayo maelezo uliyonipa sasa ndo napata nayo shida kuona TRA bado inahitaji kushikana shati na wakala kuchukua iko kidogo alichopata. Inaumiza kichwa asee