Nilisema hivi"
Mkuu hiyo kodi ya kamisheni anayelipa ni kampuni inayotoa huduma ya simu yaani vodacom, Airtel, Tigo nk. Kwa hiyo wakala anapolipwa pesa yake anakuwa amepata kipato kipya yaani anaangukia kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya kodi ya mapato kinachosema mtu atalipa kodi ikiwa anakipato.......
Kwa hiyo huyu wakala akishapokea pesa zake anakuwa amepata kipato sasa. kabla ya hapo pesa hiyo ilikuwa bado mikononi mwa kampuni ya simu.
Kama hujanielewa niulize tena.
Wapi panakuumiza kichwa?
Siku zote nilikuwa najua ile kamisheni ikishatolewa kwa wakala inakuwa kodi ishakatwa so wewe kama wakala unaendelea na biashara tu bila kuhangaika na TRA.
Nashkuru kwa darasa mkuu.
Umenifumbua macho, ntawajulisha na wengine.
Kuna kitu kinaitwa "presumptive taxation". Hii ni aina ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wenye mauzo yasiyozidi milioni 20 na pia hawana uwezo wa kutengeneza mahesabu (kuajiri certifified public accountant kutengeneza mahesabu). Hawa wanalipa kodi kwa kukadiriwa. Makadirio hayo yanafanyika mara unapoanza biashara unatakiwa kwenda TRA kuomba kukadiriwa. Sheria ya kodi ya mapato kifungu cha 133 kinasema ukishaanza biashara ndani ya wiki mbili unatakiwa kwenda TRA kupata kitambulisho ya mlipa kdodi yaani TIN. Sasa wakati wa kupewa TIN ndipo unakadiriwa. makadirio si kwa mtaji ulio nao bali kwa mategemeo utauza shilingi ngapi kwa mwaka.
Kwa hiyo baada ya kujua utauza sh ngapi kwa mwaka kodi ndipo inakadiriwa kutozwa. Kuna viwango vimewekwa.
Mfano
[TABLE="width: 491"]
[TR]
[TD]MAUZO KWA MWAKA[/TD]
[TD]KIWANGO CHA KODI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 4 lakini hayazidi Milion 7.5[/TD]
[TD]Sh 200,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 7.5 lakini hayazidi Milion 11.5[/TD]
[TD]sh 424,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 11.5 lakini hayazidi Milion 16[/TD]
[TD]sh 728,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yanazidi Milion 16 lakini hayazidi Milion 20[/TD]
[TD]sh 1,150,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Zaidi ya Milioni 20 unapaswa utengeneze mahesabu[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mkuu nyelesa umeona kichwa cha mada hapo juu? Tunajadili sheria za kodi na si principles za kodi. Maana principles za kodi si sheria. Stick to the topic please!Kuna mtaalamu mmoja wa Kodi alisema "Tax is not always proportionate rather is progressive" Naomba ufafanuzi mtaalamu huyo alikuwa ana maanisha nini?
Mkuu Malyenge naomba kuuliza swali la awali kabisa,Kwanza kuna aina ngapi za kodi zinazopaswa mwananchi kulipa Tanzania? Nnavyojua kuna VAT,PAYE na zipi?
Naomba mchanganuo tafadhali.
Je unatatizo la kodi. Lete suala lako hapa na utasaidiwa.