Madumbikaya
JF-Expert Member
- Jun 6, 2018
- 639
- 1,919
Ni kiwanja cha zamani sana hiyo mitaa ya uwanja wa mpira Nangwandayes bado ipo
Ndani palikuwa padogo sana ila nje aliweka vimitumbwi vya kukalia na bango kubwa juu lenye picha ya samaki limeandikwa shooters
Mtwara ilikufa rasmi mwaka 2013 mwishoni baada ya serikali kuondoa gas na processing zifanyike Dar lakini mpaka leo story za Gas kimya
Mji huo kama ungebaki bila serikali ya kikwete kubadili maamuzi ya Gas leo Dar ingeonekana ni kijiji cha wavuvi
Huo mji hapo mjini viwanja vilikuwa vinauzwa milion 900 miaka ya 2012 to 2013
Mtwara ilikuwa ni mji ambao matajiri toka mikoa mbalimbali wanagawana ardhi kama njugu
Bila Mambo ya Gesi kuzimwa na JK leo mtwara ingekuwa ni moja ya miji mizuri na mikubwa Tanzania na ya mfano
Mtwara pako vizuri sana na mji sio slum kama Dar,Mji wao ulipimwa
Wajanja walipiga pesa wakasepa lakini leo sijui hata milioni 10 kama vinauzika
Wanasiasa wote walinunua viwanja huko,Eneo lote la beach matajiri walilinunua kwa bei mbaya sana
Walijaa wazungu huko miaka ya 2012/2013 unaweza ukahisi ulaya imehamia mtwara
Kulikuwa na matumizi ya pesa ambayo sijapata kuyaona ,Maisha yalikuwa juu sana lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mkubwa sana
Taasisi zote za fedha unazozijua zilijaa mtwara,kulikuwa na utitiri wa mabenki huko lakini yote yameondoka wamebaki BOT na zile Giant Bank tu