Bhaaaassss...imekwisha!!Tajiri maisha ni machaguzi! Pia kupoteza hela ni suala binafsi na mtazamo binafsi.
Anaejenga nyumba yupo sahihi; anaepanga apartment na kulipa kwa $ yupo sahihi. Ni mtazamo, ni vile mtu anataka tumia pesa yake. 😊
Motivational Speakers haoHiyo jamii inayompongeza mtu aliepanga ni jamii gani..?
Maisha ni kuchagua; kujenga au kupanga.Fafanua
🤣Hiyo jamii inayompongeza mtu aliepanga ni jamii gani..?
Ngoja siku ukizeeka uje unyanyaswe kwenye nyumba za watuAnayelipa pango atakuwa anakula maisha. Kujenga ni umama na uoga wa maisha.
Hii ni mijadala ya club ya mafukara. Huwezi kukuta watu wenye fedha zao wanajadili haya. Kwa sisi mafukara, kila kitu ni maumivu.Huwa kuna mjadala mkali sana kwenye jamii wa kumsema na kumsimanga mtu anayejenga nyumba ya kuishi kuwa anazika pesa zake lakini hapohapo jamii inampongeza na kumuona mtu wa maana sana mtu anayejipositi kwenye apartment kali anayolipa kodi kwa dola.
Kiuhalisia mtu aliyepanga na kujisifu kukodi nyumba kwa gharama kubwa na mtu anayejenga nyumba yake mwenyewe ni watu wawili tofauti kabisa mbele ya safari, aliyejenga akiitaka hela yake atauza nyumba yake au atachukulia mkopo lakini aliyepanga hayo madola yake yameenda mazima hatayaona maisha yake yote.