Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

Na haya yote yanasababishwa na chama Cha mazezeta Tanzania CCM
 
Endelea kusema kweli mkuu tena kila mahali hasa ukiwa na mkeo utapata majibu. Kuna siku utajua kwanini Ibrahim alimwambia mkewe adanganye kuwa yeye ni dada yake kule kwa mfalme wa Canaan.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 

Sasa mtoto KAZALIWA katika ardhi ya Kenya, nimeweka msisitizo kwenye neno kuzaliwa, halafu unataka awe na cheti cha kuzaliwa cha Tanzania...hadi hapo huoni tu kasoro?

Mtu anapewa cheti cha kuzaliwa kwenye nchi ambayo wakati wa kuzaliwa alizaliwa akiwa katika mipaka ya hiyo nchi...

Hivyo mwanao anatakiwa awe na cheti cha kuzaliwa cha nchi ya Kenya, isipokuwa uraia wake utakuwa Mtanzania kukufuata wewe (sina uhakika kwa sheria za uraia za Kenya zipoje juu ya mtoto anayezaliwa kwenye ardhi yao)...
 
Sheria za nchi yeyote duniani hutambua mtoto nchi anayozaliwa huwa raia wa hiyo nchi hadi afikie miaka 18 aamue mwenyewe anataka kuwa raia wa nchi gani

Hivyo hadi miaka 18 ataendelea kutambuliwa kama raia wa Kenya
 

Akiwa na cheti cha kuzaliwa cha nchi yeyote, ataandikishwa na kusoma vizuri tu...
 
Nchi zote hutambua haki za mtoto hata uende Marekani au ulaya

Mtoto nchi anayozaliwa anakuwa raia wa hiyo nchi automatically hata kama wazazi wake wote wawili watanzania

Ila hupewa nafasi atabaki kuwa raia wa nchi husika hadi afikishe miaka 18 achague uraia

Akikaa kimya ataendelea kutambuliwa kama raia wa nchi alizaliwa

Mtoto hawezi zaliwa Kenya
cheti cha kuzaliwa ukataka upate Tanzania

Cheti.cha kuzaliwa mtu hupewa nchi alikozaliwa sio nchi ambayo hakuzaliwa
 
Atakuwa kalewa huyo mtoto.azaliwe Kenya halafu cheti cha kuzaliwa utafute Tanzania

Maajabu ya dunia
 
S
Usemayo ni sawa kabisa, nafahamu sana hilo, kuliko unavyofikiria.

Wenye watoto na wajukuu waliozaliwa nje ya Tanzania ndiyo tunaielewa adha ya ujinga wa Watanzania.
 
Mtoto nchi anayozaliwa anakuwa raia wa hiyo nchi automatically

Sio nchi zote zenye huu utaratibu including Tanzania...

Mtoto atakuwa na haki ya kupata cheti cha kuzaliwa cha nchi aliyozaliwa lakini sio uraia...

Kwa Tanzania ni hadi mzazi mmoja awe Mtanzania...

"Uraia wa Tanzania kwa Kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Na. 6 ya Mwaka 1995, mtu yeyote anayefuzu kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ni yule aliyezaliwa nchini Tanzania na ambaye wakati wa kuzaliwa kwake mmoja wa mzazi wake alikuwa raia wa Tanzania."
 
Je akifika 18 years atapewa?
 
Atatengeneza vipi cheti cha kuzaliwa bila vielelezo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…