Anayejua kuhusu kifo

Anayejua kuhusu kifo

kifo kina maelezo mengi. kwanza lazima tukubaliane kuwa death is the state and not the process, yaani kifo ni mwanzo tu wa kuendelea mbele na si mchakato. kifo ni hali ya mwili kutengana na conscious mind au ni kitendo cha mapigo ya moyo kuacha kufanya kazi kinachotokea ni kwamba roho zinabeba chuki, visasi na kinyongo na kama hujasamehe ile roho kwakuwa bado inaishi hubaki ikiwayawaya(wondering soul) ikitafuta kulipiza kisasi au kutimiza kile ilichokisema au kukinuiya huko nyuma
Mkuu, ebu fafanua hapo, unasema 'Death is the state, and not the process'.Kisha unasema,' yaani 'kifo ni mwanzo tu, wa kuendelea mbele, na si mchakato, kifo,ni hali ya mwili'
Hapo sipaelewi vizuri.
 
Kama Kuna MTU alikufa Kisha akafufuka,basi huyo ndo angetupa majibu ambayo yangekata kiu yetu.
 
Mkuu, ebu fafanua hapo, unasema 'Death is the state, and not the process'.Kisha unasema,' yaani 'kifo ni mwanzo tu, wa kuendelea mbele, na si mchakato, kifo,ni hali ya mwili'
Hapo sipaelewi vizuri.
Mchakato ni kitu chenye mwisho wakati kifo hakina mwisho
 
Kama miaka saba iliyopita mama mmoja jirani yetu wakati anafariki aliwambia ndugu hataki waombolezaji tuone maiti hivyo iliwekwa picha tu mpaka watu wakawa wanarudi mara mbilimbili kuangalia kama ni mwenyewe au ni picha...ila mama mwenyewe alikuwa ni mlozi na chanzo cha kifo chake kilikuwa yeye kumuua mkwewe yani mume wa mwanae hivyo upande wa pili wakafanya revenge mama wa watu alikuwa anapenda kulala na soksi basi siku hiyo kalala kuamka asubuhi kaungua kisigino ila soksi haijaungua hivyo kidonda kikawa kinakuwa taratibu...swali likabaki kwa sisi tuliohudhuria je mhusika kafa au laah na kwanini hatukuruhusiwa kumuaga kwa kuona mwili wake? Au kwenye jeneza hakuwepo mpaka wakaweka picha?
 
Well said Mkuu.Hawa wanao-comment wanaleta hadithi tu,Mimi siwaelewi na Nahitaji atakayetolea majibu basi awe alishawahi kufariki.
Kwa mawazo kama haya basi hata dawa za mgonjwa inabidi wagundue wagonjwa wenyewe na si na MTU ambaye hajawahi hata kuumwa ugojwa husika.
 
Mmh hebu nijibu haya tulinganishe na uhalisia
-kama kifo kingekuwa ni kurudi pale ulipotokea tungeweza kupata shuhuda nyingi tu....lakini fahamu kwamba anaye 'kufa' sio yule yeye aliyezaliwa
-ingekuwa kile tunachokula kinatokea pale pale kilipoingilia tena kikiwa kama kilivyo tungeweza kuwa na mjadala! Lakini bahati mbaya sana tunakula kingine kupitia mlango mwingine na kutoa kingine kupitia mlango mwingine ni vitu viwili tofauti vyenye asili moja
Dhana ya kifo iko hapo kama utakuwa umenielewa View attachment 384445
Mkuuuu ni Mimi macho yangu au Nina wenge la usingizi? Hiyo picha s dushelele?
 
Mmh hebu nijibu haya tulinganishe na uhalisia
-kama kifo kingekuwa ni kurudi pale ulipotokea tungeweza kupata shuhuda nyingi tu....lakini fahamu kwamba anaye 'kufa' sio yule yeye aliyezaliwa
-ingekuwa kile tunachokula kinatokea pale pale kilipoingilia tena kikiwa kama kilivyo tungeweza kuwa na mjadala! Lakini bahati mbaya sana tunakula kingine kupitia mlango mwingine na kutoa kingine kupitia mlango mwingine ni vitu viwili tofauti vyenye asili moja
Dhana ya kifo iko hapo kama utakuwa umenielewa View attachment 384445
Nakuelewa sana mkuu.
 
Moja ya sababu au uthibitisho wa uwezo/miujiza ya Mungu ni pamoja na kuwepo kwa kifo.

Kifo hakuna kiumbe anaeweza kukikwepa haijalishi anaishi vipi yaani awe anapata kila anaochohitaji katika uhai wake au awe fukara ni lazima afe tu.

Na hata wapinga Mungu wa humu wanadai kila kitu kina kinawezekana na kila kilichopo kina chanzo... lakini hadi leo hii hakuna maarifa yanayoweza kutumika kuongeza siku za kuishi kwa kiumbe yoyote yule.
 
Kama kifo ni kama umelala nafuta ile dhana kuwa aliekufa anasikia sema tu hawezi kusema
 
Kama miaka saba iliyopita mama mmoja jirani yetu wakati anafariki aliwambia ndugu hataki waombolezaji tuone maiti hivyo iliwekwa picha tu mpaka watu wakawa wanarudi mara mbilimbili kuangalia kama ni mwenyewe au ni picha...ila mama mwenyewe alikuwa ni mlozi na chanzo cha kifo chake kilikuwa yeye kumuua mkwewe yani mume wa mwanae hivyo upande wa pili wakafanya revenge mama wa watu alikuwa anapenda kulala na soksi basi siku hiyo kalala kuamka asubuhi kaungua kisigino ila soksi haijaungua hivyo kidonda kikawa kinakuwa taratibu...swali likabaki kwa sisi tuliohudhuria je mhusika kafa au laah na kwanini hatukuruhusiwa kumuaga kwa kuona mwili wake? Au kwenye jeneza hakuwepo mpaka wakaweka picha?

Labda mwili uliharibika vibaya
 
Kifo ni hali ya kawaida katika ulimwengu. Kila chenye mwanzo kina mwisho. Na mwisho wa kimoja ndio chanzo cha kingine. Kifo ni hali ambayo ina umuhimu sana. Kama kungekuwa hakuna kifo ulimwengu usingefika hapa tulipo na uhai usingekwepo.

Nyota zinazaliwa kupitia Star dust na zinakuwa jua. Jua kinazidi kukua kutokana na reaction ya hydrogen na kuwa Red Giant. Red giant zinakua na gas ya reaction inazidi kuisha na kupasuka na kuwa Nebula. Nyota hufa. Sayari nazo zinashikiliwa na nyota na kisha nyota ikipasuka inatengeneza black hole kuzichukua na sayari za karibu na kuzikusanya pamoja na inakuwa mwisho wao.

Volcano inatengeneza mwamba wa igneous, igneous rock inakuwa weathered na kufa na kuwa Sedimentary rock, sedimentary rock au igneous rock zinaweza kuwa forced na pressure na joto na kuwa metamorphic rocks.

Maji yanatoka katika hali ya maji, kuwa mvuke, kuwa mvua, kuganda na kathalika.

Kila kitu unachokiona ulimwenguni kinabadilika. Kila kitu kilochozaliwa/ chenye mwanzo kinazeeka na kufa/kupotea kabisa. Gari uliyonayo leo hii sio sawa sawa na ile uliyoinunua. Probably tairi hazipo sawa, mafuta na oil sio sawa na haiwezi kukaa zaidi ya miaka 200 itachakaa tu hata kama ukiwa hauiendeshi. Nyumba uliyonayo baada ya miaka 100 na zaidi itachakaa tu na kuwa gofu. Kila kitu kinachakaa (kinazeeka) na kutofaa kutumika (kufa).

Kila sekunde seli zetu zinabadilishwa na kuwekwa mpya. Sayansi inasema ndani ya miaka 2 kila seli ya mwili imebadilika.

Kifo ni hali ya kawaida. Ni hali isiyowakumba tu binadamu na viumbe bali ni sehemu ya hali ya ulimwengu. Faida yake kifo kinarudisha upya kitu kimoja kuwa kingine.

Ukifa mwili unakuwa mbolea na kila element uliyookusanya ulipokuwa unakula inarudi kuwa sehemu ya ardhi.

Pia kifo ni fundisho. Kuwa hakuna ambacho umekuja nacho na hakuna utakachoondoka nacho. Kila mali, mke/mme, pesa, tittle, kazi, raha, shida, na kila kitu unakiacha.

Hivyo kumbuka kutenda mema. Matokeo ya matendo yako (Karma) ndio mavuno ya pekee ambayo utaondoka nayo katika maisha baada ya kifo cha mwili huu wa sasa
 
Kifo kitabakia kuwa myth ijapokuwa kila mtu mmoja mmoja anasema kwa jinsi anavyofikiria na kuhisi ila bado maelezo yake hayajajenga mantiki ya kufikirika kwa wengine kama yupo sahihi!vitabu vya dini mungu aliandika kupitia mitume imeelezea kifo kama hakuna ajuae ajali hii itamfika lini?!kifo kama ilivyo roho haina elimu mujarabu.ila itabakia kuwa siri ambayo utaijua siku ukifa.quran tukufu ina sura inayoelezea vijana wa pangoni ambao walikimbia nchi yao na kwenda kujificha katika pango kumuhofia mfalme ambae katili.haijulikani idadi yao ila walikuwa na mbwa walipopotelea humo pangoni na kulala miaka 300 ukiongeza 60 yaani walilala wakijigeuza wakiota kwa miaka 360!walipoamka wakaulizana tumelala muda gani?!walijiridhisha kwa majibu kwamba wamelala siku moja au sehemu tu ya nusu siku!walihisi njaa hivyo wakamtuma mmoja wao akanunue chakula ila aende kwa uangalifu asije kuonekana atauawa!alipofika sokoni wakashangaa sarafu jamaa anatumia ya miaka 300 iliyopita kama wewe ukanunue dukani vitu na senti 20 yenye tobo katikati!kwahiyo kifo kilitafsiriwa hapo kwamba hata adamu aliekufa zamani akifufuka leo atasema amelala jana akaamka leo.
 
Kifo sio myth. Kifo hakipangiwi. Hakuna anayekufa bila sababu. Kila tokeo lina chanzo.
 
Back
Top Bottom