Anayejua kupika chipsi vuruga anielekeze

Anayejua kupika chipsi vuruga anielekeze

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mko poa familia,

Jamani nina hamu na chipsi vuruga leo hatari, ila sijui kuziandaa. Sitaki kwenda kununua naombeni kuelekezwa ili niandae mwenyewe.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.

maxresdefault.jpg

Picha kutoka maktaba
 
Unakaanga chips

Mahitaji: Nyanya, kitunguu swaumu, tomato paste, mafuta ya kupikia, Chumvi,

Unakaanga kitunguu maji kwenye mafuta, swaumu, (karoti, hoho au pilipili manga ni optional).

Unaweka nyanya mbili hivi. Ikichemka unaweka nyanya ya pakti hii hufanya iwe sticky, inachemka ikiwa nzito imeiva

Chumvi muhimu ukumbuke kuweka

Unachukua chips ulizozikaanga unachanganya kwenye mchanganyiko wake. Hakikisha chombo kinatosha kuchanganya yani kiwe kikubwa

Unaweza kuweka ketchup kwa ajili ya kuongeza ladha iwe nzuri. .

Kwa hisani ya mke wa Gily
 
Asante Mkuu, umetisha sana nakaanga sasa hivi
 
Ujuzi umeupataje mkuu na kula hujawahi
Nilivyosoma huu uzi nilikuwa na wife nikamulixa anajua kupika hii kitu akansema ndio

Sasa akawa ananiambia jinsi ya kupika na mie nikatype jamaa apate msaada wa kupika. Huku watu hawajishughulishi na uzi za msingi wanachelew kujibu. Au wengi wako kwenye nyuzi za KATAA NDOA 😁

Nimemsaidia njia kwa maelekezo ya wore tu ila hata mimi sijawahi kula kweli.
 
Kuna aina nyingi za chips aisee nj tembea uone,kuna waengine wanaweka mchicha,wengine kabichi,wengi spinach na kabichi,wengine kitunguu,hoho,karoti aah kumbe nipo nje ya mada.

Mapishi mema mkuu
 
Ukichanganya na nyama halafu vimchuzi kwa mbali vi-absorb kwenye chips na viungo huwa ni Tamu sana.
 
Back
Top Bottom