Anayejua kwanini Polisi jijini Mbeya jana Jumamosi 04/11 waliandamana atujuze

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Jana Jumamosi 04/11 wakati ninaangalia taarifa ya habari usiku, niliona picha ikionesha kikosi cha jeshi la polisi jijini Mbeya kikiwa kimebeba silaha nzito wakiandamana.

Jambo lililonivutia ni mama mmoja namkadiria umri wa miaka 80 na zaidi alipowauliza waandamanaji kunani? Mbona mtaani kwetu kuna amani nyie mmebeba silaha nzito!

Walimjibu hakuna tatizo kuna amani tu, naye akaitikia japo kwa mashaka.

Anayejua huko Mbeya kunanini mpaka polisi waandamane huku wakibeba makombora, atujuze.
 
Usikute ni mkwara kama ule wa wanajeshi siku ya maandamano wao wakatangaza watakuwa mtaani wanafanya usafi. 😂

Nchii hii polisi na ndugu zao wanatumika vibaya sana, mishahara yao yenyewe sasa ni ya kimbwiga kwelk, ila wameshupaza vichwa wanapata visenti vya rushwa kwa kubambikia watu kesi ama kudhulumu haki ya mtu.
 
Kilichojitokeza jana huko Mbeya si kitendo sahihi kwa nchi iliyoingia mfumo wa vyama vingi, japo kuna kila dalili CCM inatumia jeshi la polisi ili wananchi waoune mfumo huo ni hatari kwa amani yao. Wanaotaka kufanya maandamano wametumia taratibu elekezi kwenye katiba inayowataka watoe taarifa ili wapate ulinzi. Mkuu wa mkoa anasema watu hao wanataka kuvuruga amani ya nchi! Hapa wakulaumiwa ni aliyeruhusu nchi iwe na katiba badala ya kuendeshwa kwa utashi wa watawala wenyenchi yao wasiokuwa na simile. Yule mama aliogopa sana kwani kikosi kilisimama karibu na nyumba yake huku magari ya deraya yakifunga barabara! Ni wazi alitegemea mapambano nyumbani pake, jeshi la polisi lifanye kazi bila kututisha wananchi.
 
Jana Jumamosi 04/11 wakati ninaangalia taarifa ya habari usiku, niliona picha ikionesha kikosi cha jeshi la polisi jijini Mbeya kikiwa kimebeba silaha nzito wakiandamana. Jambo lililonivutia ni mama mmoja namkadiria umri wa miaka 80 na zaidi alipowauliza waandamanaji kunani? Mbona mtaani kwetu kuna amani nyie mmebeba silaha nzito! Walimjibu hakuna tatizo kuna amani tu, naye akaitikia japo kwa mashaka.
Anayejua huko Mbeya kunanini mpaka polisi waandamane huku wakibeba makombora, atujuze.
Wapigie simu.
 
**** Amani tele tu hakuna shida.
 
Anapigwa mkwala Mwabukusi na Mdude . Aibu sana kwa jeshi la polisi.
 
Jana Jumamosi 04/11 wakati ninaangalia taarifa ya habari usiku, niliona picha ikionesha kikosi cha jeshi la polisi jijini Mbeya kikiwa kimebeba silaha nzito wakiandamana. Jambo lililonivutia ni mama mmoja namkadiria umri wa miaka 80 na zaidi alipowauliza waandamanaji kunani? Mbona mtaani kwetu kuna amani nyie mmebeba silaha nzito! Walimjibu hakuna tatizo kuna amani tu, naye akaitikia japo kwa mashaka.
Anayejua huko Mbeya kunanini mpaka polisi waandamane huku wakibeba makombora, atujuze.
Unachanganya maandamano na mazoezi ya kijeshi kwa kutokujuwa Kiswahili au kwa makusudi kabisa?

Wewe ni Mtwnzania au mlowezi?maana tunafahamu Mbeya kuna walowezi wengi.
 
Mazoezi ya kijeshi unafanyia kwenye mitaa ya Uhindini, Mabatini, Nzovwe na Mbalizi! Wangekwenda Kawetere wakafyatua makombora ningeelewa, lakini hawa walikuwa wanatembea na wengine kwenye magari.
 
Back
Top Bottom