Huu utaratibu na ustaarabu haukupaswa utumike hapa Tanzania kwasababu kila mtu ni mwizi,si abiria wala dereva wote ni majizi.Abiria sehemu ya umbali mrefu atataka akulipe kinyonyaji na dereva nae sehemu ya ruti fupi atahakikisha anafanya mafekeche akupige pesa ndefu,hii ndiyo Tanzania nchi iliyojaa wendawazimu isipokuwa mimi na ukoo wangu
Ustaarabu huu kwa wenzetu umewezekana kwasababu hakuna njaa na kila kitu kiko mahala pake,hakuna wizi wa kijinga jinga.
Unakuta Dereva kapewa gari na tajiri na kila siku anapaswa apeleke elfu 30 - 35,Bado hapo hajaweka wese,bado hapo hajapata posho yake ya siku nzima,bado hajasumbuliwa na wazee wa naya kung'arishia viatu,bado hajasumbuliwa na wazee wa parking,unadhani kwanini asifanye ulaghai kama huu ili asavaivu?
Mifumo na Ustaarabu huu kwa Tanzania bado sana na kinachosababisha watu kutokuwa waaminifu ni njaa na tamaa.
Mfano mdogo tu nenda katazame pale Mwendokasi,yaani zile mashine za kuskani kadi hazifanyi kazi na yote hii ukiuliza hutapewa jibu la kueleweka ila ukiwa mtu mwenye akili timamu utajua tu mambo ni mawili 1.WIZI 2.TAMAA
Afrika espeshali Tanzani huwa tunakurupikia mambo ambayo hatuna uwezo nayo,ndiyo maana kauli yangu ya siku zote ni ileile ya kwamba " AFRIKA NA WAAFRIKA WANA LAANA YA MILELE"
Sitokaa niibadirishe hii kauli hadi nakufa