Anayejua michezo ya Bolt kuongeza bei aniambie

Anayejua michezo ya Bolt kuongeza bei aniambie

Wakati na request bolt bei ilokuja ni 15, 000 tunafika destination risiti inasoma 21,000 tumebishana sana ila kwakuwa nilikuwa na mgojwa wa nikaitoa hiyo hela, haijawahi kutokea hii mara zote nilizorequest bolt,

Je kuna vijana wanafanya uhuni? Naomba shule katika hili
Kamchezo ka ku-cancel route ovyo huwa Kuna adhabu. Uneza kuta unapandishiwa bei balaa.
 
Baadhi ya bolt drivers ni wahuni sana.
Niliwahi kukodi gari toka Mliman City kuja home maeneo ya Bahari beach, nauli ilionesha ni 14000.
Nafika home bill inakuja 22,000.
I was so confused, nikamlipa dereva akasepa.
Kuja kuangalia email inaonesha nimetoka Airport, tukapitia Darajani kigamboni Ndio tukaja home.
Nilipeleka malalamiko bolt jamaa akafungiwa leseni.
 
Huu utaratibu na ustaarabu haukupaswa utumike hapa Tanzania kwasababu kila mtu ni mwizi,si abiria wala dereva wote ni majizi.Abiria sehemu ya umbali mrefu atataka akulipe kinyonyaji na dereva nae sehemu ya ruti fupi atahakikisha anafanya mafekeche akupige pesa ndefu,hii ndiyo Tanzania nchi iliyojaa wendawazimu isipokuwa mimi na ukoo wangu

Ustaarabu huu kwa wenzetu umewezekana kwasababu hakuna njaa na kila kitu kiko mahala pake,hakuna wizi wa kijinga jinga.

Unakuta Dereva kapewa gari na tajiri na kila siku anapaswa apeleke elfu 30 - 35,Bado hapo hajaweka wese,bado hapo hajapata posho yake ya siku nzima,bado hajasumbuliwa na wazee wa naya kung'arishia viatu,bado hajasumbuliwa na wazee wa parking,unadhani kwanini asifanye ulaghai kama huu ili asavaivu?

Mifumo na Ustaarabu huu kwa Tanzania bado sana na kinachosababisha watu kutokuwa waaminifu ni njaa na tamaa.

Mfano mdogo tu nenda katazame pale Mwendokasi,yaani zile mashine za kuskani kadi hazifanyi kazi na yote hii ukiuliza hutapewa jibu la kueleweka ila ukiwa mtu mwenye akili timamu utajua tu mambo ni mawili 1.WIZI 2.TAMAA


Afrika espeshali Tanzani huwa tunakurupikia mambo ambayo hatuna uwezo nayo,ndiyo maana kauli yangu ya siku zote ni ileile ya kwamba " AFRIKA NA WAAFRIKA WANA LAANA YA MILELE"

Sitokaa niibadirishe hii kauli hadi nakufa
Upewe maua yako mkuu 👏🏾
 
Back
Top Bottom