Anayejua namna ya kutuma hela kwa usiri naomba anifahamishe

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
15,052
Reaction score
36,866
Kabla ya yote NRNE βœŒπŸ½πŸ‘ŠπŸ½

Kuna mtu kanipa raha sana leo nataka nimtunuku, naomba anayejua namna ya kutuma fedha iwe kwa simu au online bila jina kuonekana anijulishe.
  1. Mtumiwaji yupo Tanzania, so usisuggest cashapp au venmo.
  2. Naomba namna nyingine mbali na kutumia wakala ambayo ni lazima niende mwenyewe physically.
Ukiachana na sababu yangu binafsi:
  • Kuna kampeni za kisiasa, wengine wanatamani kuchangia ila wanaogopa kuwa traced na ikaathiri biashara au kazi zao.
  • Kuna watu humu huwa wanashare shida mbalimbali, sometimes tunaogopa kuwasaidia kuepuka kureveal identity zetu.
Anayejua namna au mwenye uzoefu tushirikishe tafadhali.

Natanguliza shukrani!



PS:
NRNE, nchi yetu wote, ukatili haukubaliki.
 
Fanya kati ya haya
1. Kama una Bank account namba yake kamuwekee bila kuandika depositor name
2. Nenda kwa wakala, mpe pesa na namba ya simu aweke kisha akuoneshe muamala kuwa umefanikiwa.

Hivyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…