Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Boss kwani hukumsikia yeye mwenyewe akikiri kuwa alikuwa anabip ikapokelewa!!!
 
Ivi mods wanatumia nn kufikili uzi independent kabisa mnaunganisha ns uzi mwingine
 
Huku vijana wanapoteza ajira
Huku Bodi inataka vijana wakatwe 15%/ya mishahara kulipa mikopo
Huku wananchi wanafunga biashara
Huku TRA wanataka kukusanya tr 2
Huku vijana hawana ajira
Huku serikali inawaita wadaiwa sugu

Uongozi huu wa awamu ya tano umetupa mwanga kuwa makini na watu wanao taka uongozi badala ya kuwa makini na vyama vya siasa.

huu ni mgogoro mkubwa

Kuna wazee walikua wanategemezwa na vijana wao, lakini baada ya vijana wao kupoteza ajira kuna hatari ya wazee hao kufa mapema.

Kuna wazee wameuza kila walicho nacho ili kuwasomesha vinana wao lakini Leo wanajuta maana vijana hawana ajira ya aina yoyote, banks hazikopeshi mitaji, ajira hakuna etc
 
Tanzania ni nchi iliyopoteza dira haielewi inataka nini hata viongozi waliopewa dhamana kichwani hamnazo, they don't care about its people even the future of the country. Na hivi tunaendekeza siasa za kipuuzi ndo hatufiki popote kwa kumuachia mtu mmoja ajiamulielie yeye atakavyo. As a country we have a long way to go
 
Kuisoma Pyscolog ya Kichwa chako ni Rahisi sana kutokana na Andiko lako.
Umeonekana kutaja neno ajira zaidi ya mara Tano ..Simply Umeonyesha ni mtu uliyedhani kwako Ajira ni kila Kitu baada ya Kumaliza Elimu yakonya Juu .

unapaswa kufahamu hitaji la Dunia ya Sasa .

ulimwengu ya Sasa inahitaji watu wenye Fikra Za Kuisaidia Dunia Kua sehemu pazuri.
Dunia Inahitaji BIG BRAINS.

Nenda tena kajifungie Chumbani kwako ,kabla hujaja na Kilio cha Ajira na Ujiulize haya Machache.

1. Ni zipi Jitihada zako za kutengeneza ajira. .?Ulishawahi jaribu hata kuuuza Mchicha. ?
2. Umefanya nn kuisaidia Serikali yako kujikwamua kiuchumi.? .
 
Kama Baba masikini asiyekuwa na akili nzuri atumikishavyo watoto kujipatia kipato, ndivyo pia serikali za nchi masikini hukamua wananchi wake.
 
Dah! ama kwr ile kauli yakwamba mtaisoma no naona tunaisoma no kwr kwr cjui n no gn hiyo tunayoixoma hatumalzi
 
Anatupeleka Canaan kwenye nchi ya maziwa na asali,easy money kwishney sasa ni HAPA KAZI TU
 
Kuna msemo usemao kuwa siasa siyo uadui, na hilo lina ukweli ndani yake lakini pia wakati mwingine siasa inaweza ikageuka kuwa mwiba!
Mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi kulikuwa kuna wimbo uliokuwa na kiitikio kwamba tumeipenda wenyewe ambao ulipambwa na maneno matamu matamu pamoja na kuwa na vionjo vya aina yake, kitu kilichowafanya wapenzi wa chama kilichokuwa kikisifiwa na huo wimbo kuserebuka sana..
Sasa baada ya uchaguzi mambo yamegeuka kwa upande wa wale waliokuwa wakiserebuka, na ni kwamba wapo walioachishwa kazi, waliokatiwa mishahahara, waliokuwa na vyeti feki ambao wengi wameamua kuacha kazi wenyewe na kukimbia, waliofilisika na kufunga biashara zao, waliokuwa wakitegemea ajira serikali hadi sasa hawajapata, waliokuwa wakitegemea serikali iwape watoto wao mikopo ya elimu ya juu lakini wakanyimwa, n.k!
Kiufupi ni mengi yametokea na kila mtu ni shahidi, sasa hawa waliokuwa wakiimba hicho kibwagizo wamekuwa wakiwaangukia na kuwaomba msaada wale waliokuwa upande wa pili kwa aibu ili kuokoa jahazi, japo hizi namba zinasomwa pande zote lakini wafuasi wa kijani waliokumbwa na hayo yote wanatia sana huruma, na ni wepesi sana wa kusahau!
Hivyo siyo chuki wala kinyongo lakini....
 
Wamepania kuutokomeza upinzani kwa nguvu zao zote.

Walianza na Billicanas ya Mbowe, jana wamemnyang'anya Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Sumaye shamba lake halali lenye hati la heka 35. Hatujui who is next. Lowassa? Kingunge? Yetu macho.

Watakapomaliza kutunyang'anya mali na kujikuta hatubadiliki na kukosa cha kutunyang'anya unafikiri kitakachofuata kunyang'anywa nini kama si roho zetu?

Ila wakumbuke what goes around comes around.
 
Nimelalamika kwa maneno ugumu wa maisha hadi nimeishiwa maneno,sasa natangaza kuunga mkono maandamano yoyoye Yale as long as theme itakuwa ugumu wa maisha,nimetengua kauri yangu ya zamani kuwa siwezi kushiriki maandamo,coz sioni mwisho ya kizisoma number,Mara ya mwisho n
Tulisoma number ngapi vile ( malizia basi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…