Tangu tupate Uhuru nchi hii ndio Mara ya pili kuwa na Rais bora ukiacha Jk Nyerere.
Hoja zake nzuri, ana msimamo, hapendi watu wavunje amani ya nchi. Anateua makada wa chama chetu kile kuwa Ma DC,RCS, DEDS,RAS,DAS,N.k
Pia ni msomi kuliko wote toka Uhuru, ana PhD ya kusomea!!!
TATIZO
Mimi na ka elimu kangu ka ngumbalu, kana kitu sijakielewa kidogo, hii ni kutokana na Elimu kiduchu niliyo nayo, pia ni ya hapa na pale.
1. Rais alisema "Wilaya yoyote itakayokumbwa na njaa, mkuu wa wilaya hana kazi". Sasa Musoma,Bunda,Serengeti, Magu zimetangaza njaa je mbona Rais yuko Kimya?Mbona Anna Kilango alifyekwa fasta?
2.Rais alisema akiwa Bukoba kuwa waathirika wa tetemeko hawata jengewa nyumba na serikali, kwani tetemeko halikuletwa na serikali!!!
KWA HIYO NJAA IMELETWA NA WAKUU WA WILAYA? MAANA ALISEMA NJAA IKITOKEA ANAWATIMUA KAZI!!!
Ninge omba mwenye elimu ya PhD au hata darasa la nane anifafanulie, sikuambulia kitu hapo. Mimi uelewa wangu mdogo, tuvunuliane tu jamani, nipewe majawabu.