Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kama rais angekuwa anabase na kimoja na kukimaliza then kingine tungekuwa mbali

Kiukweli nchi ili itajirike ni lazima izalishe je sisi tunazalisha?
Bado tupo butu
Vingi vimefanyika nusu nusu
 


Usiwe na akili finyu wewe....mbona nchi inakwenda kuzuri tu shinda tawala zote zilizopita? Ulitaka nchi iendelee kutawaliwa na wauza unga na watu wa misheni taun au?
 
Ni kweli umepotea wewe mpiga dili hujui unakokwenda kupiga dili hakuna kupiga dili bro fanya kazi.hapa kazi tu
 
Tuna Mfalme ambaye ni mjuaji( much know kwa lugha nyingine).Kila kitu anajua yeye,na anataka kiende kwa jinsi anavyojua yeye.Mbaya zaidi,aliowateua (Mawaziri,Ma Rc,Ma Dc) ili walinde ugali wao wanaenda sambamba na mawazo ya mfalme huyu ambaye ameshaonyesha dalili zote za nchi kumshinda.
Serikali hii imeona kupunguza matumizi ndio njia pekee ya kuendesha serikali na kuongeza kodi katika bidhaa.Kuna msemo unaosema "Asiepoteza,Haokoti".Tuna Mfalme ambaye anapingana na huu msemo uliopo hata kwenye bibilia.Serikali inayobana matumizi kamwe haiwezi kupanua Fursa za uchumi..Na swala la Ajira kwa vijana halipo. kwa kifupi,ni serikali ya ovyo sana haijawai kutokea.
Elements za serikali ya awamu hii
*Uongozi wa matamko
*Uongozi wa kulipizana visasi
*Uongozi wa kulalamika lalamika ovyo badala ya kuonyesha matendo.
Baba Mungu mwenyezi tunakuomba utuongoze tupo Gizani.Amen
 
We unapoona inaelekea ujue ni huko huko. We ulitaka iende wapi? Maana nchi iko vile vile sema watu ndo wanabadilishana
 
Tupo gizani ndugu yangu tumepotea kwa ubishi wetu, kila siku movie mpya na watoto wadogo wanaanza kusumbua watu wazima wenye akili nyingi. Pumbavu kabisa katika vyama vibovu duniani ccm imeoza
 
Punguza kulalamika utajua tunaelekea wapi.
Kila speech anayotoa Mtukufu wetu lazima utaona analalamika mambo ya nyuma tu.Unaona imekaa sawa? Hivi wewe kama ni Baba wa familia kila siku watoto wako wanakuona unalamika kuhusu Maisha ya Baba yako kwamba yalikua ya anasa,amechezea hela hadi akashindwa kuacha uridhi unaoeleweka.ndo maana leo hii wewe ni masikini..Unadhani watakuelewa kila siku.kurudia rudia story hyo tu kila siku.
 
Hawataelewa. Mtukufu hajui la kufanya na ubabe umeanza kugonga mwamba. Itambidi sasa aanze kusikiliza ushauri.
 
Speech yake ya kwanza naya mwisho kuiangalia niya ufunguzi wa bunge,baada ya hapo sijawahi kujisumbua kabisa kumwangalia tena

Wazee wetu wako kimya kabisa wanaona kila kitu kinavyozidi kuvurugwa lakini wapo kimya
Warioba
Butiku
Bomani
Mkapa
Na wengineo
 
Sisi watumishi wa tz,tunajua fika kuwa asilimia kubwa hatukukupigia kura ya kukufanya rais,hali ambayo imekufanya utuadhibu vibaya mno,tumeishi kama mashetani,inatosha uwiiii twafaaa
 
Mkuu ana chuki na watumishi sana, anatamani awafukuze wote au hata kuwapunguza. Sijui walichomfanya, uhamisho kikatili, kazi hakuna motisha, mishahara midogo watu wamesusa ule moyo wa kujitolea kwa dhati umepungua. Watumishi wengi wanaamini jamaa anawabagua, anajali wanajeshi na polisi hata promotion zipo jeshini tu huku kwa walimu na wengine hakuna. Kipindi cha kampeni aliongea kwa unyenyekevu sana ila sasa kawageuka.
 
Tatizo mlizoea kukaa ofcn bila kazi na kusubiria mwisho wa mwezi. Huduma zikawa duni sana.

Mtu anafika kwenye ofisi ya serikali kuhitaji huduma anaangaliwa kama nyanya chungu. Huduma hovyo alimradi tu liende. Kisa mwisho wa mwizo si nitapokea tu hata nisipokuhudumia,, kwa ni vip sipungukiwi chochote. After all kuna semina nategemea kwenda kesho kutwa na marupurupu kibao.

Acha tu heshima kwenye maofisi ya serikali irudi.

Tunachomwomba tu awaangalie vijana waliomaliza vyuo wawezeshwe kwa ajira wasijae ana mtaani, itakuwa tatizo kwa future ya Taifa hili.
 
Mm nashauri akaze hvyo hvyo ikiwezekana apunguze mishahara kabisa ili wapate akili.
 
Wakati wa kampeni tuliwasihi sana, mimi binafsi nilitafuta kila namna ya kuwashauri watumishi wa umma muachane na mkoloni mweusi hamkutaka. Wacha muisome labda akili itawaingia. Mie nshazoea kuuza genge langu najua walalahoi wawashindwi kununua mchicha ntauza tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…