Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
USIFIKIRI NITAKUKUBALI WATU WASIKIE HAPANA, ILA NATAMBUA UWEZO WAKO.

Kwamiaka mingi nimekuwa nikikosea serikali ya Tanzania toka nimepata kibali chakuitwa mpinzani, japo nikiri nilipata kibali na leseni hiyo bila ya semina na uzoefu kutoka kwa walionitangulia kupata kibali kujua maana ya UPINZANI na UTAIFA hilo nakiri.

Ila nimejitahidi kuwanapinga mambo yote yanayofanywa na serikali ili kudhihirisha mimi nimpinzani kweli.

Kipindi cha rais wa awamu tatu (3). Benjameni Mkapa nilipinga alipoamua kuhakikisha taifa linakuwa kiuchumi nilimuita majina yote mabaya unayoyajua wewe lakini yule Mh.aliweza kusimama imara nakukuza uchumi wa Tanzania na aliweza kufuta ile Kodi ambayo ilikuwa inaitwa kodi ya kichwa.

Kodi hii kama wewe nikijana wa sasa uwezi kuijua lakini mimi nakumbuka kuna siku baba alikimbia wakati tunakula kisa kodi sikumuona baba nyumbani kwa siku mbili masikini hata kufuta hili nilimpinga yule rais na kumuita Kapa.

Rais yule aliondoka lakini wakati anaondoka.

Akaja mwingine ambaye alifanyakazi kubwa sana ya kunipa uhuru huyu bwana alikuwa na huruma sana ilifika sehemu nilimpinga sana na kumtukana ananiita mahali anapoishi ambapo hata mimi natamani niishi kama yeye nakunywa nae chai pamoja na korosho juisi kahawa naondoka kwakweli pamoja na kudekezwa kote huku niliendelea kutukana na kumuita mjinga kwa upole wake, masikini kumbe nilishindwa tofautisha huruma na ujinga Mungu nisamehe kwa hilo, huyu bwana alijenga barabara za kutosha alijitahidi kuhakikisha kila mtanzania anapata maisha bora hapo kwangu ndio kukawa kosa kubwa hata pale alipoona nadaiwa sijalipa kodi alijaribu kunitetea japo nilimtukana sana na kuendelea kumuita dhaifu mpole lakini nilifika mbali nikasema nataka mtu ambaye anaelementi za Udikteta, Mtu anaweza kufanya maamuzi bila kuunda tume, sitasahau siku niliyomwambia aliyekuwa naibu waziri tamisemi wakati ule Mwangrii kuwa unanidanganya hapa kikaoni nenda halmashaurii uwone fedha zinaliwa kama mchwa, nikaenda mbali kuliko nikasema huyu mtu anasafiri sana kunanini anamaliza fedha.

Leo nimekupata wewe uliyekuwa kwenyendoto zangu hata kama sitasema hapa watu wasikie lakini kwa matamshi ya hapo nyuma waelewa wanajua nilikuwa na kutaja wewe.
Umekuja kufanyakazi na kweli Ukatwambia Hapa Kazi Tu, tuache majungu sasa nimeanza kukupinga tena kwanguvu mbele za watu kinachonishinda nikukosa hoja ya msingi kuwa napinga nini, nimeandaa vijana kwenye ofisi zangu katika njia za mitandao wapinge kila unalolifanya wamekuwa wanaandika mpaka wanakosea wanakosea mpaka yale ambayo hayafai kukosolewa nimebakia na aibu ila nashindwa kusema.

Wewe umeshikilia kodi mpaka baadhi ya ndugu zangu wanapata aibu nimejaribu kukutafuta sana ili nikwambie punguza makali simu unapokea ila unaniambia unataka mabadiliko ya kweli sio kama yale yangu ya kisanii.

Umeweza kushuhulikia nidhamu kazini, watumishi hewa waliyokuwa wanachota fedha bure, naona ndege tunazo pamoja na mambo mengine mengi ambayo sitaweza kuhataja hapa, nimebakia nasema kwaajinsi navyokwenda kuumbuka sasa natamani hata yule aliyokuwa ananipa kahawa pale kwako, nikifikiri miaka mitano itaisha bila kunywa kahawa yapale nachanganyikiwa kabisa.

Lakini naomba ufahamu nakukubali sana tena sana ila mbele zawatu sintasema hata siku moja ila moyoni nakukubali hata nikiwa na vijana wangu nawaambia wewe ni jembe nao wanakukubali kweli tu.

Huku kukupinga jua hii nikazi napokea mshahara mimi na jopo langu kwa kukupinga kwahiyo usitegemee nitakusifu hadharani.

Maana nitafukuzwa kazi mimi asante kwa kunielewa ni mimi mpinzani naepinga kili kitu.
 
Kama raise Mimi naona alishaishiwa hivi sasa anasubiri atachotamka Makonda hicho ndiyo dira ya taifa kwa wakati huo kwa hiyo tuendelee kuvumilia hadi Makonda naye atakapoishiwa matamko.
 
anatupeleka kwenye episode za mfalme J.uha, kila ratili moja iuzwe kwa pesa moja..
kila debe moja libadilishwe kwa ng'ombe watatu.
 
chadema imekua ajenda ya vikao vyote vya serikali. Kila kukicha wanahoma ya chadema.

Nakumbuka ukuta ilivyo wakimbiza hadi Jeshi letu kuingizwa kwenye mambo haramu yasiyo faa kwao.

Sasa chadema endelea kukaza hadi waombe poa hawa Lumumba.

Madawa ya kulevya mmefeli, na kwa taarifa police mnao watumia sio wajinga, sema tuu wanatii, ipo Siku watachoka.

Wananchi wanahitaji barabara, shule, mikopo ya elimu ya juu, walimu wazuri, madaktari etc, na siyo blabla kama hizi.

Ni lini mtaacha kuijadili chadema, mkatuliza akili na kujadili mambo ya msingi ya maendeleo?

Mnaweza wafunga wengi lakini fikra za ukombozi haziendi jela.

Jifunzeni, Ethiopia hadi Leo ina GDP ya dola 500 wakati Kenya sasa ivi inakimbiza 1,200 dola.

Uchumia wa kidictator hausaidii, wala hauhitajiki , tunahitahi viongozi wanao sikiliza , kukubali challenge etc.

Sasa hili la madawa ya kulevya sijui mtaligawa wapi maana nasikia mkibugi mnakimbilia kugawa kwa wengine matatizo yenu.

Peopleessssss, power.

FB_IMG_1485280281488.jpg
 
Siasa mbaya sana, hasa siasa za visasi,mbwa mdogo anabweka kumuita mbwa mkubwa, please wait......
 
Kama ni kukopa tu na kuanzisha miradi hata chama kichanga kama ACT-Wazalendo kisingeshindwa maana wataalamu wa ku-negotiate mikataba/mikopo wapo wengo tu ndani ya serikali na hata nje ya serikali.

Kama ni kununua ndege hata chama kama TLP kisingeshindwa kwani ni swala tu la kuamua kuagiza ndege bila kujali mambo mengine yatakuwaje.

Ukiacha mambo hayo,maswala mengine yote yamewashinda na sasa wamebaki kukimbizana na wapinzani na kuibua matukio kila kukicha.

Uchumi haueleweki(hata mh.Bashe ni shahidi) ,hifadhi ya Taifa ya chakula inazua maswali, mikopo ya wanafunzi shida(kuna baadhi ya vyuo wamezuia vyeti vya wahitimu wa mwaka jana kwasababu Bodi haijalipa ada za watu waliomaliza vyuo. Mfano St.Johns University).

Uhakiki wa watumishi umegeuka wimbo wa Taifa.Madai na malimbikizo ya watumishi hakuna anaejua watalipwa lini kila siku wanapigwa "sound"!

Hivi sasa wameahamia katika vita ya madawa ya kulevya lakini ulizeni kwenye bajeti ya maendeleo mwaka wa fedha 2016/2017 walitenga shilingi ngapi kwa ajili ya kupambana na madawa ya kulevya.

Jiulizeni miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani imetekelezwa kwa asilimia ngapi huku miezi 8 ikiwa inakatika.

Waulizeni mpaka sasa wamepeleka fedha kiasi gani(asilimia ngapi) kwa ajili matumizi ya kawada kwenye Idara, Wizara na Taasisi za serikali,n.k

Alafu ulizeni ni fedha kiasi gani zimetumika kuendesha kesi zinazohusu wapinzani ikiwa ni pamoja na gharama za kuwakamata na kuwasafirisha ili wakajibu mashitaka na muangalie aina ya hayo mashitaka.

Kuhusu Tanzania ya viwanda majibu unayo tumejenga viwanda vingapi mpaka sasa na vya size gani(binafsi sijaona).

Ukitafakari haya yote kwa makini ndio utajua ni kwanini hivi sasa wanaelekeza nguvu nyingi kwenye haya matukio huku watu wakihoji tu inakuwa ni kosa.

Something is better than nothing-Jk ulijitahidi.
 
Umeandika ukweli mtupu lakini ngoja waje wanaoamini kila raia ana chama na mpiga dili.
 
Active Mod 2 Mod 3 Mod 4 huu uzi kwanini mmeuunganisha?Wacheni watu tupaze sauti kupitia huu mtandao.

Hii hivi thread yenye page 156 ndio mmeamua kuitumia kuficha maoni ya watu?

Tabu sana hii!!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

kwa sababu wabongo hatujui tunapotaka kwenda so na yeye anatupeleka huko ambapo hatupajui coz ndio tunapataka
 
Tangu napata akili na kufaham siasa za hapa nchini sijaona viongoz wakiwa seriously na mambo muhimu, bali huwa bize na vitu visivyo na faida kwa taifa.
Na kama huongea vitu vya muhimu lakn huishia kuongea na si kutekeleza. Napata hofu sana kama tutakuja kuwa taifa lenye mabadiliko.

Et hii njia ya makonda ndio taifa liko seriously na madawa ya kulevya. Unawaita mnauza wanasema hatuuzi unawaambia haya asanten kwa ushirikiano wasalimie watoto. Maana huna ushahid. Hatuko seriously!!

Watumiaji unawapeleka mahakaman siku moja unawasomea tuhuma siku hiyo hiyo, hukumu siku hiyo hiyo kwa kuwafunga kifungo cha nje kisicho rasmi miaka mitatu. Harafu unasema uko seriously!!

Et hii serikali awam ya tano iko seriously na mafisadi huku wakikumbatia GSM, watu walioifilisi tz awamu iliyopita wamekuja na jina jipya wamekua wasafi!!
Awamu iliyopita walipitia kwa watoto wa viongoz awamu hii hupitia kwa huyu kondacta. Maana ndio husikilizwa na askofu mkuu[emoji779]️[emoji779]️ chochote akimwomba mkuu kukifanya huitikia ndio!! Hatuko seriously .

Et tunataka kuwa nchi ya viwanda kwa kuzindua mashine za kufyatua tofali nacho kiko miongon mwa ahad ya tanzania ya viwanda. Hatuko seriously!!

Et kuchagua ni kupanga, tunanua ndege kwa keshi huku tunaenda kuomba omba hela za kununulia dawa, za maji, za elimu . Hatuko seriously!!

Wananchi tumekubali kuingia kwenye mitego ya watawala pale wanapotutengenezea filam kututoa kwenye mambo muhim kwa taifa na kubaki kujadili filam zao kama hii aliyoanzisha makonda. Badala ya kujadili kushuka kwa elimu kulikopelekea watoto wetu kufeli kwa wingi tumesahau na kujadili wavuta unga na wauza madawa hewa! Tumeitupa huko njaa inayowakabili wananchi na kuanza kujadili hizi drama!! Inaniuma sana akili zetu tunavyozitumia chin ya 10%

Leo unga hapa Dar ni 1700 kwa kg . Sijawahi kuona tangu nizaliwe bei kuwah kutokea kama ya mwaka huu kwa unga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom