Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Ukikaa. Kisiasa na kibishani. Huto jua na wala hauto kaa ujue rais anatutoa wapi na anatupeleka. Wapi kwa sababu upo kisiasa zaid
 
Vipaumbele hatuna. Bunge limenyofolewa meno. Maamuzi yote yanatoka kwa Mkuu wa nchi. Bajeti anapanga yeye, anaidhinisha fedha kwenda kufanya analotaka yeye. Vyama vingi marufuku nchini. Hakuna fedha kuidhinishwa kwa kazi yoyote badala yake inatakiwa ikusanywe hadi iadimike kabisa ila watu wafanye kazi. Afu lazima nchi irudi kwenye Ujamaa na Kujitegemea. Hakuna safari za kwenda nje ya nchi kuombaomba ni fedheha kwa taifa, badala yake tunawaalika wageni afu wakifika wanaombwa hapahapa. Kutembeza bakuli ni aibu wasijeliona watu. Ni mabadiliko ya staili."If you don't know where you are going any road can take you there". Ndio
 
Ukikaa. Kisiasa na kibishani. Huto jua na wala hauto kaa ujue rais anatutoa wapi na anatupeleka. Wapi kwa sababu upo kisiasa zaid
Huwezi kuhoji sababu eti na wewe unawaza kuwa utakuja kuteuliwa sasa km bando unapewa bule na posho buku7 unawaza nini?
 
Mzazi hujua mahitaji ya msingi ya watoto wake kuliko hata watoto wenyewe. Hivyo, kama familia ilipanga kununua gari lakini mzazi akaona kwa wakati ule kinachohitajika zaidi ni chakula na akanunua hicho chakula kwa manufaa ya familia mimi naona hakuna tatizo hata kidogo. Tatizo lingekuwepo kama angekuwa anachukua hizo fedha na kuzitumia kwa manufaa yake.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Dodoma
 
alichofanikiwa hadi sasa ni kujaribu kupunguza kasi ya mtandao wa wachagga kujinufaisha kwa njia ya kujuana na kupiga madili, mengine sijui.
 
Tulikuwa na mpole, tupo hapa tulipo
Tumepata mkali, tuone atatupeleka wapi
Baada ya hapo tutajua kama taifa
Tunahitaji mpole au mkali
 
Sitaki kuanza na salamu maana niko vibaya kiakili leo maana kila kona imekuwa madawa madawa tu mara huyu mara yule mara huku mara kule mara huyu kakamatwa mara huyu kaachiwa... mara huyu kamtukana huyu na huyu katukanwa hivi na huyu kajibu hivi ikawa hivi na inaenda kuwa hivi ila haitakuwa hivyo..........Sasa hii nchi inaenda wapi?? maana kila mtu kashakuwa Mtu kwenye nchi hii maana sasa naona matabaka kila kona kuanzia juu hadi mlangoni kwangu (angalia na kwako wewe unaesoma) isijekuwa kila mtu anahusika na hii kitu maana kwa namna inavyopelekwa kila mtu naona anakwenda jera sasa.......naona kama maigizo muda mwingine mfano UTUMBUAJI umekuwa ukeketaji sasa maana unabagua jinsia za wengine (tafakali hapo nyuma usimaanishe Ukeketaji kwa namna unavojua wewe) sasa kila kukicha ni KIKI tu huyu huku huyu kule sasa nani ni nani?? na kwa nani? maana sijajua tunaenda wapi.......Hivi mmesahau kuwa tunahitaji viwanda? meli hapa kanda ya ziwa Flyover je miundominu..........ila yote yamesahaulika yanayoonwa ni unga tu jamani na faru john na mama yake maana hata hiyo nayo ilikuwa kiki tu ya kuogopesha watu tujue wanafanya kazi................NADHANI NIMEPATA JIBU KUWA TANZANIA INAENDA KUWA KOLONI TENA LA NDUGU TRUMP SOON AS POSSIBLE..........
 
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..

Badilisha jina to ''elevulao''
 
Sitaki kuanza na salamu maana niko vibaya kiakili leo maana kila kona imekuwa madawa madawa tu mara huyu mara yule mara huku mara kule mara huyu kakamatwa mara huyu kaachiwa... mara huyu kamtukana huyu na huyu katukanwa hivi na huyu kajibu hivi ikawa hivi na inaenda kuwa hivi ila haitakuwa hivyo..........Sasa hii nchi inaenda wapi?? maana kila mtu kashakuwa Mtu kwenye nchi hii maana sasa naona matabaka kila kona kuanzia juu hadi mlangoni kwangu (angalia na kwako wewe unaesoma) isijekuwa kila mtu anahusika na hii kitu maana kwa namna inavyopelekwa kila mtu naona anakwenda jera sasa.......naona kama maigizo muda mwingine mfano UTUMBUAJI umekuwa ukeketaji sasa maana unabagua jinsia za wengine (tafakali hapo nyuma usimaanishe Ukeketaji kwa namna unavojua wewe) sasa kila kukicha ni KIKI tu huyu huku huyu kule sasa nani ni nani?? na kwa nani? maana sijajua tunaenda wapi.......Hivi mmesahau kuwa tunahitaji viwanda? meli hapa kanda ya ziwa Flyover je miundominu..........ila yote yamesahaulika yanayoonwa ni unga tu jamani na faru john na mama yake maana hata hiyo nayo ilikuwa kiki tu ya kuogopesha watu tujue wanafanya kazi................NADHANI NIMEPATA JIBU KUWA TANZANIA INAENDA KUWA KOLONI TENA LA NDUGU TRUMP SOON AS POSSIBLE..........
 
Kuanzia nilipoibua mjadala wa Uhalali wa Phd ya Mhe.Magufuli niliacha rasmi kumu-address kama Dr.Magufuli na kutumia Ndugu au Mheshimiwa tu hadi itakapothibitika ni Halali.
Nimesoma Hoja ya Prof.Kitila kuhusu PhD ya Magufuli.
Prof.Kitila ni Rafiki yangu sana.Yeye ni kaka yangu na ananichukulia kama mdogo wake.
Katika Kuchangia Mjadala wa PhD ameandika "UDSM hakuna namna mtu kupata Cheti Fake na huwa hatuangalii sura ya Mtu...". Kwa hiyo. .. "PhD ya Magufuli haina kasoro"...
Vilevile kuna watu Mwanzo walisema masuala ya Machapisho hayana maana lakini cha ajabu wameweka waliyoita Machapisho ya Magufuli na pia kuweka Picha akiwa amevaa mavazi ya Graduation kama vile ndio Authentification ya PhD ya Magufuli.
Wengine wakaanza kusema Rombo ina matatizo hivyo niachane na PhD ya Magufuli.Utadhani kuhoji uhalali wa PhD ya Magufuli ndio kumeleta madhara Rombo.Wasomi wetu wengine wakoje?
Nataka kugusia hoja ya Prof.Kitila kuhusu kuwa hakuna namna ya kufanya Udanganyifu UDSM .
1-Prof.Kitila anaweza kuwa Mwaadilifu sana katika kusimamia taaluma na kazi yake kama Mhadhiri Chuoni.
Lakini ni kosa kubwa ku-assume kila mtu ni mwadilifu.
Tukienda hivyo tutaua nchi na ndio maana wengine tunasizitiza sana Kuimarisha Taasisi zetu na mifumo.
Hapo ni kama vile ku-assume kuwa kila mtu ni mpigaji.Hivyo tunasizitiza haja ya kuimarisha taasisi na mifumo ambayo itadhibiti mafisadi na watu wasio waadilifu baadala ya ku-assume kila mtu ni mtakatifu .
Kama watu waliweza ku-forge documents Serikalini na Kuchota Fedha Za EPA au ESCROW ni mechanism gani itakayozuia PhD za Mbeleko vyuoni kwetu hasa zinazohusu wanasiasa?
Tena katika mazingira yanayoashiria mbeleko kwa Mbebaji kumshusha aliyembeba nae akambeba kwa kumteua kushika ujumbe wa Bodi?
2-Kama Seif-Al Islam Mtoto wa Ghaddafi alikuja kuibuliwa kwa kashfa ya kuhonga na kupata PhD ya mbeleko Kule London School of Economics(LSE) sass UDSM ina mfumo gani thabiti wa kuepuka fraud kuliko LSE?
Kwa Mujibu wa Academic Perfomance Center chuo kikuu cha London School of Economics kilishika nafasi ya pili kwa miaka kadhaa mfululizo kwa ubora duniani wakati UDSM ikishika nafasi ya 1618 kati ya Vyuo 2,000.
LSE iko vizuri kiteknolojia na kitaaluma katika kuzuia academic Misconduct kuliko UDSM lakini bado Seif Al-Islam alifanya.
3-UDSM imewahi kukumbwa na staff waliofanya Udanganyifu kwenye taaluma na Prof.Maboko aliwahi kuutangazia Umma.
UDSM hii hii imeshawahi kutoa wanafunzi waliofanya udanganyifu na baadhi yao kuvuliwa Degree zao
Charles I . Ng'imba aliwahi kuvuliwa Digrii yake aliyoipata kwenye Graduation ya Tarehe 29 August ,1987.
Unasema haiwezekani?
4-Kuna hao walioleta machapisho waliodai ni Ya Magufuli na kudai kuwa alistahili PhD kwa sababu alishaandika tangu 2003.
Tena nimeona ameshirikiana baadhi na huyo Supervisor wake.
Sasa watuambie alifanya PhD by Publication?
Sweden ,Australia na hata Uholanzi(Najua Unafahamu) inaruhusiwa PhD by Publication.
Kwa faida ya mjadala tu: Ni kuwa PhD by Publication zinakusanywa paper zote na kuziandikia Covering Essay na jumla na paper iwe na maneno si chini ya 20,000 ikiwa condition na masharti mengine ya submission yapo constant.
Pia inazingatiwa ni paper ngapi umeandika mwenyewe na ni ngapi umeshirikiana(Co-Author).
Na katika kushirikiana ni ipi jina lako limekua la kwanza maana inabeba uzito wa synopsis.
Sasa Katika hizo Paper alizoweka the so called (Dr.!?) Chahali ni Tatu tu anazooneshwa kaandika yeye na zipo kwenye vijarida vya uchochoroni tu sio kwenye respectable Journals huko.
So swali la PhD Candidate huyu kuipata PhD kwa miaka 3 akiwa Part time Candidate kinyume na Prospectus halijajibiwa.
Ingawa Prof.Kitila umetoa maoni yako tu kama mchangiaji na Sio Authority ya UDSM au Supervisor wake(Ofcourse hawezi kujitokeza tena maana ni mteule wa Bodi) lakini naheshimu maoni yako uliyotoa kistaarabu bila matusi kama hao waliomtetea kwa vitisho na matusi kwa hoja zao za kula nae Canteen au kumuona amevaa vazi la graduation.
UDSM kama vilivyo vyuo vingine au taasisi nyingine nchini haina kinga thabiti dhidi ya Academic Fraud hasa zinazohusisha wanasiasa na vigogo serikalini.Hiyo hoja haijaleta uzito wa kutosha katika authentification ya PhD ya Mkuu wetu.
Tena nilicheka sana nilivyo-imagine jinsi kazi ya Literature Review ya Mkuu wetu ingefanana. With knowledge that Examiners may tolerate grammer idiosyncratic than any other mess.Sijui Lugha na VIVA ilikuaje. Don't joke! Ile lugha yake ile ...! Haya!
Hoja ya Prof.Buchweshwaija kuwa co-author kwenye paper yake kisha kuja kuwa Supervisor wake na kisha kuja kuwa mteuliwa wa Waziri aliyeteuliwa na yeye mwanafunzi wake tunaweza kuli-debate left-right-center hasa tunapoangalia mfumo wetu wa elimu na uadilifu.
Ofcourse nakiri kuwa wakati wa kuanza PhD yangu niliwahi kukuambia nilipata headache sana kuhakikisha kuwa napata Supervisor maahiri ndani yawanakamati.Maana uliwahi kufanya mchakato wa kujiunga na chuo hicho kabla hujajiunga Southampton University kwa PhD yako.
I knew as PhD candidate,Institution'll gain through my presence by gaining credibility,profile and funding. Why should I allow them to treat me as an inconvinient ,Incompetent fool? Si lazima nami niwe smart kujilinda?
So kwa Case ya Magufuli na SUP wake twaweza kui-debate kweli kuanzia co-authorship.
Sijui independence ya Mwanafunzi huyo ilikuaje hata kama ilikua ni Ph.D by Publication.
Ni vyema tu akajitokeza kutoa ufafanuzi au Chuo .Mbona lile la silaha alipohakiki hadi watu wengine walikua proud kuiweka picha yake na bastola kama Profile ya groups za Watsap?
Asante kwa kukoleza mjadala.Good day Prof.Baadae tena Kaka. ...
# MagufuliHakikiPhDyako
# MagufuliVerifyYourPhD
# MagufulideclareyourPaytubes
A Luta Continua,Victory Ascerta.....
Ben Saanane.
 
Watanzania tuna akili fupi sana ndo maana hatusonge mbele kama taifa na mtu mmoja mmoja, maada ni nzuri inawweza kutusaidia kuibua njia mpya za kumsaidia rais kama ushauri, mtoa mada hana nia mbaya na rais bali anajaribu kutushirikisha tuangalie mwelekeo wa sisi kama taifa, kwa hiyo tuache kumkebehi tuchangie mada kwa mtazamo chanya kwa kutoa michango na ushauri wa kujenga taifa.
Kaka wachangiaji wengine humu wanatuma maoni wakiwa Milembe mental Hospital ndiyo maana maoni yao utaona kabisa ni upupu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom