Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
hahahaha....mpaka tutaomba PO hii miaka mitano! Pombe si mtu wa kisport sport aisee!
 
Mabeyo ni full Gen...rekebisha!!
 
Hahaha unajua hata wanao mtetea wanafanya Ivo ILA moyoni wanajua kabisa tushaliwa vichwaaa uyu jamaaa kweli akina lisu waliona kuleeeeeeeeeeeeeeeee !!! Deni la taifa na skia limefika trilioni 48 (sinauhakika) najamaa kasema anaendelea kukopa
 
Jamaa anazidi kutupoteza na jamaa wamekaa kimya tu
 
Mtabiri mmoja aliwahi kusema CCM itakufa pale itakapojaribu kujigeuza tena kuwa chama bora, halali na chenye ushawishi kwa umma. Pale chama kitakapojaribu kuskani mfumo wake na kuondokana na maovu yake hapo ndipo mwisho wake utakapofika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba maovu ndio mfumo uliohalalishwa na kujijenga kwa miongo kadha wa kadha.
 
Leo ni majuto wakati muda ulotumika wakati wa kampeni kuwadhihaki na kuwadhalililsha wagombea ungetumika kuwachunguza kufikiria na hasa busara na hekima kutumika hakika now ushenzi huu usingekuepo kamwee viongozi tuliowachagua hatuwaelewi kamwe na bado ana miaka 4 mbele na tukicheza 2020 atatubuluza tena[emoji37] [emoji37] [emoji37]
 
Go! Go! Go! Magufuri atakayegeuka mfanye kuwa teja. NAPE tayari hii vita iko na maadui wengi.
 
Maneno yake mwenyewe yanatimia 'hakujiandaa" alichukua form tu ila hakujiandaa.
 
Mimi binafsi sina imani naye tena. Kama kuna wanao muamini shauri yao. Hta aende bandarini akamate makontena 2000 sitamuamini. Maana tumeshajua michezo yake.

Hata clauds wamesema hwataki mazoea ya kupangiwa kusoma habari zake.
 
Picha:Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar

SWAHILI TIMES / Swahili Times / 1 hour ago

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.

Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.

Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.

“Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusu makontena 20 yenye mchanga wa madini uliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.



Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari pamoja na vitu vilivyochakaa March 23,2017





Moja ya kontena likiwa lina magari matatu ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake wanakuwa wameficha magari ya kifahari.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

23 Machi, 2017
 
Am be
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo tu.

Am beginning to question even this. Yoh can not defend a fraud to this extent. Hata hiyo nia nzuri si ajabu yakikuwa maigizo.

Huyu alikuwa mnyenyekevu kila akiongea anakunja mikono. Kumbe alikuwa chui ndani ya ngozi ya kondoo.

This is MADNESS!
 
PICHA HALISI YA TANZANIA

Imefika mahala nimeona niandike, amanitoe maoni yangu kuhusu hali ya kisiasa na maendeleo ya Tanzania kwa sasa. Kwa muda mrefu sasa mambo mengi yameendelea au yanaendelea kujadiliwa Tanzania taifa ambalo sasa lina miaka zaidi ya hamsini ya uhuru lakini robo tatu ya wananchi wake bado ni masikini sana.

WAPI TUMEKOSEA​

Yafuatayo ni mambo makuu manne ambayo kwa mtazamo wangu tumeshayakosea toka nyuma na kwa ujumla wake yamepelekea sisi kuwa hapa tulipo;

· Mfumo wetu wa elimu tunao utumia mpaka sasa hauna matokeo mazuri katika kukuza uchumi na kutoa ajira kwa watazania. Ni mfumo unao funga ubunifu (creativity), unao mnyima kijana uwezo wa kujiamini (uthubutu), unao muandaa mtu kuajiliwa kwa asilimia 80 tena serikalini na sio kujiajili na kuajiliwa. Lakini ni mfumo usiowekeza katika tafiti za ndani hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia zinazo faa kutumika nchini, tafiti za kilimo na magonjwa

· Kutokuwa na viongozi wenye nia ya dhati ya uzalendo wa kweli, kujituma, wabunifu na wenye upeo wa kuongoza na si kutawala kwa mslahi ya taifa na sio chama wala kundi la watu wa aina Fulani.

· Kukosa katiba yenye kuendana na aina ya jamii tulionayo kwa sasa, yenye kuzalisha sheria na kanuni zenyekulifanya taifa kuwa na maadili ya kweli, uwajibikaji na uzalendo wa hali ya juu kwa kuzingatia utawala bora wa sheria na haki ya kweli

· Taifa kukosa mpango kazi wa taifa wa kudumu, wa muda mrefu wenye vipaombele vya kudumu na vifupi vinavoendana na sera za vyama vya kisiasa utakao tekelezwa na viongozi wanao chaguliwa kila baada ya miaka mitano.

KWANINI TUNAENDELEA KUWA HIVI TULIVYO NA TUTA KUWA HIVI TULIVYO​

· Upeo mdogo; haina bishi kuwa upeo wa watanzania tuliowengi wa kupambanua na kung’amua mabo bado ni mdogo sana, hii imesababishwa na mfumo wa elimu tulionao na aina ya maisha tunayo ishi sisi kama taifa. Ndiomaana utashangaa tuliowengi hufuata upepo unapovuma badala ya kupima jambo na kuling’amua kwa makini kasha kutoa msimamo wenye hoja

· Mapungufu makubwa ya kikatiba; wengi wawatanzania kwanza hawaielewi katiba yao ilivyo na mapungufu yake. Hii ni faida kwa viongozi wetu wa sasa kwa kuitumia kuamaua na kupanga mambo mbalimbali kwa matakwa yao na si ya wanachi.

· Kukosa vipaombele vikuu vya kitaifa; taifa sasa limefika mahala halieleweki vipaombele vyake vikuu ni vipi. Tumefika mahala tunataka tutatue matatizo yote kwa pamoja bila kuchagua lipi likitatuliwa basi mengine yanajitatua yenyewe.

· Viongozi wenye tama; Tanzania ni nchi tajiri ya viongozi wenye tama, unafiki na binafsi wa hali ya juu. Ni nchi ambayo viongozi wetu hawana uzalendo wa kweli, bali ni wanyenyekevu kwa mtawala ilikupata wanacho waza kukipata

· Misingi mibovu ya kisiasa; siasa haikwepeki katika maisha ya kila siku ya jamii yoyote ile, siasa yetu kama nchi sasa imefika katika kiwango cha kutokujenga hoja za kukosoa kupata suluhisho la changamoto zinazotukabili na badalayake zimekua ni siasa za chuki, fitina, kuchafuana, ubinafsi, kukomona, visasi na tama.

MAFANIKIO NA MAPUNGUFU YA SASA

· Kama viongozi wetu wanania ya dhati kuipeleka Tanzania kwenye maisha wanayo ya hubiri ni vyema kurekebisha mapungufu tajwa hapo juu; leo nchi yetu bila kificho imefanikiwa katika yafuatayo;-

a) Ujenzi wa barabara za lami

b) Ujenzi wa njia za umeme mpaka vijijini

c) Ujenzi wa zahanati kwa kata

d) Ujenzi wa shule za msingi na sekondari

e) Ukusanywaji wa mapato (kodi)

f) Kutunza amani na utulivu

Ukiyatizama hayo sio mafanikio ya kubeza, ni ya kupongeza ingawa ni jukumu la serikali kuhakikisha uboreshaji ama upatikanaji wa huduma hizo. Lakini yote yaliyo tajwa hapo juu kwa miaka na miaka sasa yanamapungufu makubwa sana na hakuna jitihada za dhati za kweli na zinazo onekana katika kutatua changamoto hizo. Mapungufu hayo ni;-

a) Upungufu wa waalimu wa sayansi

b) Upungufu wa vifaa vya mabara

c) Upungufu wa wauguzi na madaktari

d) Upungufu wa vifaa na dawa za hospitalini

e) Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada

f) Upungufu wa nyumba za waalimu na wauguzi

g) Ukosekanaji wa huduma za maji safi na salama

h) Ukosekanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika

i) Ukosekanaji wa vyombo vya usafiri wa gharama na fuu

j) Maslahi duni yawa tumishi wauma

k) Ukosekanaji wa mifumo mizuri ya kukuza kilimo cha biashara

l) Ukosekanaji wa viwanda vidogo na vikubwa

m) Ukithiri mkubwa wa rushwa kubwa na ndogo

n) Ukosekanaji wa teknolojia kazi

o) Utumiwaji mbaya wa maliasili za kitaifa

p) Kukosekana kwa Uwajibikaji

q) Kukosekana kwa Uwazi

r) Utawala bora wa sheria

itaendelea....................................................
 
Kwa magu alishatupoteza kitambo sana sema wengi mlikuwa hamjakubali na bado mpaka tukiona atujui tutarudi vipi tulipotoka ndiyo tutachukua hatua kama wananchi nasio hizi hadithi tunazo simuliana humu n sehemu nyingine
 
Hakuna salamu nauchunguu
Kiufupi mimi ngependa hii hali iendelee ivi ivi na iongezeke zaidi ili Tuisome namba vizuri mpk 2020 tutakuwa tumepata akili na tutafanya maamuzi sahihi
 
Du! Naona tulipofika huku siko kabisa
Mpaka Nape kushikiwa bastora hii balaa sasa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…