PICHA HALISI YA TANZANIA
Imefika mahala nimeona niandike, amanitoe maoni yangu kuhusu hali ya kisiasa na maendeleo ya Tanzania kwa sasa. Kwa muda mrefu sasa mambo mengi yameendelea au yanaendelea kujadiliwa Tanzania taifa ambalo sasa lina miaka zaidi ya hamsini ya uhuru lakini robo tatu ya wananchi wake bado ni masikini sana.
WAPI TUMEKOSEA
Yafuatayo ni mambo makuu manne ambayo kwa mtazamo wangu tumeshayakosea toka nyuma na kwa ujumla wake yamepelekea sisi kuwa hapa tulipo;
· Mfumo wetu wa elimu tunao utumia mpaka sasa hauna matokeo mazuri katika kukuza uchumi na kutoa ajira kwa watazania. Ni mfumo unao funga ubunifu (creativity), unao mnyima kijana uwezo wa kujiamini (uthubutu), unao muandaa mtu kuajiliwa kwa asilimia 80 tena serikalini na sio kujiajili na kuajiliwa. Lakini ni mfumo usiowekeza katika tafiti za ndani hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia zinazo faa kutumika nchini, tafiti za kilimo na magonjwa
· Kutokuwa na viongozi wenye nia ya dhati ya uzalendo wa kweli, kujituma, wabunifu na wenye upeo wa kuongoza na si kutawala kwa mslahi ya taifa na sio chama wala kundi la watu wa aina Fulani.
· Kukosa katiba yenye kuendana na aina ya jamii tulionayo kwa sasa, yenye kuzalisha sheria na kanuni zenyekulifanya taifa kuwa na maadili ya kweli, uwajibikaji na uzalendo wa hali ya juu kwa kuzingatia utawala bora wa sheria na haki ya kweli
· Taifa kukosa mpango kazi wa taifa wa kudumu, wa muda mrefu wenye vipaombele vya kudumu na vifupi vinavoendana na sera za vyama vya kisiasa utakao tekelezwa na viongozi wanao chaguliwa kila baada ya miaka mitano.
KWANINI TUNAENDELEA KUWA HIVI TULIVYO NA TUTA KUWA HIVI TULIVYO
· Upeo mdogo; haina bishi kuwa upeo wa watanzania tuliowengi wa kupambanua na kung’amua mabo bado ni mdogo sana, hii imesababishwa na mfumo wa elimu tulionao na aina ya maisha tunayo ishi sisi kama taifa. Ndiomaana utashangaa tuliowengi hufuata upepo unapovuma badala ya kupima jambo na kuling’amua kwa makini kasha kutoa msimamo wenye hoja
· Mapungufu makubwa ya kikatiba; wengi wawatanzania kwanza hawaielewi katiba yao ilivyo na mapungufu yake. Hii ni faida kwa viongozi wetu wa sasa kwa kuitumia kuamaua na kupanga mambo mbalimbali kwa matakwa yao na si ya wanachi.
· Kukosa vipaombele vikuu vya kitaifa; taifa sasa limefika mahala halieleweki vipaombele vyake vikuu ni vipi. Tumefika mahala tunataka tutatue matatizo yote kwa pamoja bila kuchagua lipi likitatuliwa basi mengine yanajitatua yenyewe.
· Viongozi wenye tama; Tanzania ni nchi tajiri ya viongozi wenye tama, unafiki na binafsi wa hali ya juu. Ni nchi ambayo viongozi wetu hawana uzalendo wa kweli, bali ni wanyenyekevu kwa mtawala ilikupata wanacho waza kukipata
· Misingi mibovu ya kisiasa; siasa haikwepeki katika maisha ya kila siku ya jamii yoyote ile, siasa yetu kama nchi sasa imefika katika kiwango cha kutokujenga hoja za kukosoa kupata suluhisho la changamoto zinazotukabili na badalayake zimekua ni siasa za chuki, fitina, kuchafuana, ubinafsi, kukomona, visasi na tama.
MAFANIKIO NA MAPUNGUFU YA SASA
· Kama viongozi wetu wanania ya dhati kuipeleka Tanzania kwenye maisha wanayo ya hubiri ni vyema kurekebisha mapungufu tajwa hapo juu; leo nchi yetu bila kificho imefanikiwa katika yafuatayo;-
a) Ujenzi wa barabara za lami
b) Ujenzi wa njia za umeme mpaka vijijini
c) Ujenzi wa zahanati kwa kata
d) Ujenzi wa shule za msingi na sekondari
e) Ukusanywaji wa mapato (kodi)
f) Kutunza amani na utulivu
Ukiyatizama hayo sio mafanikio ya kubeza, ni ya kupongeza ingawa ni jukumu la serikali kuhakikisha uboreshaji ama upatikanaji wa huduma hizo. Lakini yote yaliyo tajwa hapo juu kwa miaka na miaka sasa yanamapungufu makubwa sana na hakuna jitihada za dhati za kweli na zinazo onekana katika kutatua changamoto hizo. Mapungufu hayo ni;-
a) Upungufu wa waalimu wa sayansi
b) Upungufu wa vifaa vya mabara
c) Upungufu wa wauguzi na madaktari
d) Upungufu wa vifaa na dawa za hospitalini
e) Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada
f) Upungufu wa nyumba za waalimu na wauguzi
g) Ukosekanaji wa huduma za maji safi na salama
h) Ukosekanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika
i) Ukosekanaji wa vyombo vya usafiri wa gharama na fuu
j) Maslahi duni yawa tumishi wauma
k) Ukosekanaji wa mifumo mizuri ya kukuza kilimo cha biashara
l) Ukosekanaji wa viwanda vidogo na vikubwa
m) Ukithiri mkubwa wa rushwa kubwa na ndogo
n) Ukosekanaji wa teknolojia kazi
o) Utumiwaji mbaya wa maliasili za kitaifa
p) Kukosekana kwa Uwajibikaji
q) Kukosekana kwa Uwazi
r) Utawala bora wa sheria
itaendelea....................................................