Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hivi kwa hili linaloendelea sasa nchini kama waziri anaunda tume ya uchunguzi kupata ukweli kesho yake amesimamwishwa kazi. swali la kujiuliza je mawaziri waliobaki tutegemee kweli watafanya kazi kwa ufanisi na kusimamia ukweli na haki pale wananchi watakapo zulumiwa haki zao za msingi?
 
Mkuu hii Nchi haiongozwi na mawziri...

Kila kitu anasimamia Bashite na Mkulu
 
anakwenda mtajua akifika, si anakodakta wake? subirini vituo
 
Penzi la Jinsia Moja linazidi kuitesa Tanzania yetu.
 
Mh. Wewe mkuu saana.....
Siku zote umekua ukiapa na kutushawishi tuamini kuwa kila usemalo ni ukweli mtupu, na utasimamia ukweli bila kujali Elimu, ukabila, rangi, undugu wala cheo cha mtu, huku ukisisitiza maneno yako "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu"...
Sasa mkuu kwanini juzi umesikika ukisema... "Nikiamua niongee ukweli, wenye uchungu na nchi yao watatoa machozi"...kumbe umekua huongeagi ukweli?.. Kwanini usiongee ukweli, kwani wewe huna uzalendo na nchi yako.?.. Nawe kwanini usitoe machozi?
 
Alianza vizuri Na wengi tulimsifia ila anapo enda wengi hatupajui na huenda ikawa kilio nakusaga meno.
Ukimya wa viongoz wakuu wakitaifa unazua simanzi nzito kwa watanzania.
Madhara ya kauli zake imekuwa shubiri kwa watanzania. Askari barabarani wanawaumiza raia kwa tozo zisizo za msingi wala ukweli. Unyanyasaji wa jeshi la polisi umekuwa mkubwa kuanzia barabarani mpaka uraiani.
Kila mtu anasema hapa kazi while watanzania tunakamuliwa kwa speed ya kutisha.
Nadhani mkuu anafurahi kusomewa mapato yasio safi ya jeshi la polisi na kusahau jeshi hilo linatukamua sisi watanzania tena kwa makosa ya kubambikiwa ama kusingiziwa. Kiukweli hakuna mtanzania anaweza kumsifia kiongoz anawakandamiza watu wake huku akitumia vyombo vyake vya ulinzi.
Umesahau tulikupigia kura sasa unatutisha nakuwalinda majitu machache majinga kama bashite kwa Rasilimali zetu. Nani asiyejua kuwa vita ya madawa ni muendelezo wa kumlinda bashite.

Kiukweli umtoka kuwa kiongozi na sasa umekuwa simba mla watu. Hujali wala husikii ila Mungu atakujibu kwa wakayi as long as tulikuunga mkono na leo tumekuwa kitoweo chako mkuu.

Tumalize ila kumbuka malipo ni hapa hapa duniani. Kama tulivyo umia na kufedheheka kwa kauli zako zenye kujifanya una uchungu na taifa. Nawewe utafedheheshwa na kauli za wanachama na wazalendo ndani ya taifa hili. Imetosha
 
Hii nchi inatakiwa aibuke mtu Kama Donald Trump ambaye hana elements za siasa aongoze nchi Ndio itaenda
 
jamaa yeye hajali Kwa kuwa anabughia na kushindilia kwelikweli ugali wa bure magogon. Shibe ina dharau sana.
 
Hajawahi kuanza vizuri bali alikuwa mbovu toka mwanzoni.

Wachache walipogundua kuwa jamaa hana jipya na ni mbovu kuliko hata watangulizi wake na kuanza kueleza umma juu ya uelekeo wake mbovu, aliwaambia nyinyi wafuasi wake kuwa wanaompinga walikuwa wapiga dili.
Nyanyi mkaanza kuimba wapiga dili wanalalamika sababu wameshikwa pabaya na huu utawala.

Lakini kama ambavyo wasemavyo wengi wetu 'muda ni jibu zuri' na ukweli haufichiki na hata kama utafichika basi hautaharibika.

Sasa hivi ukweli unajifunua wenyewe, na watu wengi wa ndani na nje wanagundua kwa kasi kubwa kwamba hili dude ni bovu.

Aliyemwita tingatinga alimaanisha kuwa huyu mtu ana efficiency lakini kwa lenyewe haliwezi kufanya rational decisions hivyo hili tingatinga lilihitaji dereva makini. Kwa bahati mbaya tingatinga linajiongoza lenyewe na halihitaji kushauriwa na ndio maana tunaona jinsi linavyohama toka barabarani na kufanya uharibifu kwenye makazi ya watu.
 

Yaani nimeipenda hii. Kila mtu awe mbunifu na apambane na kuboresha maisha yake. Rais huyu anaturudisha kwenye njia sahihi kwani tulikuwa tumepotea. Tulilea ufisadi, tulilea uvivu, hatukujua kodi ni nini, tuliishi nje ya uwezo wetu na hatukujua kubana matumizi, tulizoea uchuuzi na viduka na vioski kila mahali na kupuuza uzalishaji. Sasa tukubali kuisoma namba na tusimlaumu Rais.
 


Tunaye mwanamme wa shoka "Magufuli," hatuhitaji mwingine zaidi yake.
 


NI
WATAMPIGIA KURA 2020
HAWAJAWAHI KUWA NA MAISHA BORA SO THEY HAVE NOTHING TO LOOSE
TA FANYA HIKI NA KILE
NIMEAMUA KUFANYA HIVI NA VILE
MIMI NIKIAMUA NIMEAMUA
NITAINYOSHA NCHI HII
NITAHAKIKISHA NATEKELEZA ILANI YANGU
NILIAMUA MWENYEWE KUCHUKUA FOMU
SIKUSHAURIWA NA MTU KUCHUKUA FOMU
MIMI NDO NILIZUNGUKA KUOMBA KURA NA SIO NYIE


TUTA vs NITA

SASA WEWE UNAYO YATAKA SI ANAYOYATAKA YEYE
WEWE UNAYO YATAKA HUTAYAPATA HADI AAMUE YEYE

NA HUNA CHA KUFANYA KWANI WATU WA VIJIJINI WANAKUELEWA SANA
KWAMBA MALALAMIKO YAKO NI UCHOCHEZI TU .WATU HAWA WANAMUELEWA SANA NA HAWANA
TIME NA MTANDAO YA KIJAMII NA HAWASOMI MAGAZETI,HAWATIZAMI TV,JAMII FORUM WALA
HAWANA WHATSAP
NA HAUKO HURU TO ZAT EXTENT KULALAMIKA
KAFANZE KAZI NA USITEGEME SERIKALI ITAKUSAIDI
SERIKALI HAINA MUDA WA KUSAIDIA WEWE KWANI INA MAMBO YA MUHIMU SANA YA KUFANYA
BE VERI KEAFU.
 
Pengine rais ana nia njema na Tanzania ila maamuzi yake ndiyo yenye utata
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…