Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hilo pori utaliokota tu mkuu limezagaa hapo halina mwenyewe ?
Nikikuuliza maonesho ya kilimo ya nanenane kwenye kanda yako ulihudhuria? Au unataka fursa zikufuate?

Magufuli anataifisha mashamba kila uchwao wapewe walalahoi walime lakini nyinyi ndio vinara wa kumpinga katika jitihada zake za kuwakomboa walalahoi.
 
Tafuta pori ulime matikiti acha kulialia kama mtoto wa kike, ulishapeleka mazao sokoni yakakosa mnunuzi?

Endelea kupiga domo wenzako wanakuacha.

Mkuu kwani hayo mapori viongozi hawayaoni? Mbona wao wanang'ang'ania ofisini wakati wana mitaji? Kama mapori ni mali usingeona wakilazimisha watoto wao na ndugu zao kupatiwa kazi maofisini.
 
Naskia kikwete ana mpango wa kugombea 2025...kinyume cha katiba lakni...sjui watanzania mtamkubalia? Mana huko upinzani ndo giza kabisaaa

Kinyume cha katiba vipi? Kuna ibara inauokayokataza Rais mstaafu kutogombea?
 
Mkuu kwani hayo mapori viongozi hawayaoni? Mbona wao wanang'ang'ania ofisini wakati wana mitaji? Kama mapori ni mali usingeona wakilazimisha watoto wao na ndugu zao kupatiwa kazi maofisini.
Sasa na wewe pambana nao tuone nani anaumia,
Magufuli anawanyang'anya mashamba masikini au hao matajiri wanayoyakopea pesa bank?
 
Mimi niko Dar, haya sema hayo maonesho yamefanyikia wapi. Na useme ni wapi huko wanagawa mashamba ili hata sisi vijana wa GRADE A twende huko tukalime msimu ukifika
 
Mkuu kwani hayo mapori viongozi hawayaoni? Mbona wao wanang'ang'ania ofisini wakati wana mitaji? Kama mapori ni mali usingeona wakilazimisha watoto wao na ndugu zao kupatiwa kazi maofisini.
Halafu kuna watu wakiona pori wanafikiri halina mwenyewe wakati wenyewe ndio hawa kina SUMAYE na wengineyo tena unakuta washakula MKOPO wa MILIONI kwenye MABENKI
 
Mimi niko Dar, haya sema hayo maonesho yamefanyikia wapi. Na useme ni wapi huko wanagawa mashamba ili hata sisi vijana wa GRADE A twende huko tukalime msimu ukifika
Maonesho kanda hiyo yalifanyikia Morogoro nauli kwenda na kurudi time yoyote isingekugharimu zaidi ya elfu 10, nenda mkuranga mashamba mpaka elfu 20 unapata, vijana wengi wapo huko watapiga pesa kimya kimya mmebakia tu wa spoonfeeding mitandaoni.
 
Muhindi anaona fursa akiwa na pesa ya kutosha ama wenzake wenye uwezo wa kumnyanyua pale alipo. Watanzania wangapi wana uwezo ama spirit ya namna hio? Zaidi ya kuchekelea mtu anapofeli maisha au kurudishwa nyuma!?
 
Kikatiba Haiwezekani Hata akianzisha chama chake ama kujiunga upinzani Labada Tufuate Katiba ya Inchi ya Urusi
Hakuna kipengere kwenye katiba kinachomzuia Rais ambae alimaliza muda wake katika uongozi kupitia chama X ,then baadae akahama iko chama akaenda chama Y na kugombea urais katiba haizuii ilo nadhani,,,
 
Maonesho kanda hiyo yalifanyikia Morogoro nauli kwenda na kurudi time yoyote isingekugharimu zaidi ya elfu 10, nenda mkuranga mashamba mpaka elfu 20 unapata, vijana wengi wapo huko watapiga pesa kimya kimya mmebakia tu wa spoonfeeding mitandaoni.
Mkuranga nauli 10,000 lets assume usile, kukodi shamba 50,000 kulima 50,000, lets assume unapalilia mwenyewe. Mbegu 60,000, mpaka hapo tunaelekea LAKI 3

- Sasa chukua maelezo yako, yaweke kwa mtu ambaye ni FRESH FROM SCHOOL aliyesoma kwa kuunga unga na ambaye mpaka sasa CHUO KINAMDAI anaanzaje wakati hata kula kwake majanga.

- Hamjayajua maisha nyie ?
 
Muhindi anaona fursa akiwa na pesa ya kutosha ama wenzake wenye uwezo wa kumnyanyua pale alipo. Watanzania wangapi wana uwezo ama spirit ya namna hio? Zaidi ya kuchekelea mtu anapofeli maisha au kurudishwa nyuma!?
Hao wahindi kwa kuwatazama tu walikua ni walalahoi kama walalahoi wengine, mtu anayeiba maji kwa kujiunganishia kiuwizi huwezi kusema ana mtaji wa maana kwanza heka zenyewe ni tano tu.

Immigration wakiwatrace wanaweza kuwa ni wahamiaji haramu lakini somo ni kwamba wao wameiona fursa na wameichangamkia unaweza kukuta hilo shamba wamekodisha kwa wabongo wanaolalama maisha ni magumu lakini mgeni kawapita uwezo wa kufikiri.
 
Naskia kikwete ana mpango wa kugombea 2025...kinyume cha katiba lakni...sjui watanzania mtamkubalia? Mana huko upinzani ndo giza kabisaaa

kuliko kumpa lowasa bora 2025 awe kikwete na 2035 awe magufuli tena
 
Kuna vijana wameanza na utayari tu lakini saizi wapo mbali huko mkuranga, jifunzeni kwa hawa vijana Agribusiness (@jifunze_kilimo_na_ufugaji) • Instagram photos and videos

Elimu Biashara (@elimu_biashara) • Instagram photos and videos
 
Acha waendelee kulala chief...
 
Sasa na wewe pambana nao tuone nani anaumia,
Magufuli anawanyang'anya mashamba masikini au hao matajiri wanayoyakopea pesa bank?

Unampora shamba/pori mwenye uwezo wa kulilima kwa mashine unampa mtu anayekuja na jembe la mkono na panga, huo si wendawazimu. Nilitaraji akishapora apeleke dozzer kusafisha hayo mapori kisha agawe drip system na pembejeo nyingine kama mbolea na viuatilifu ili kufanyike kilimo chenye tija. Sasa unampora mtu pori kwa sababu ya tofauti za kiitikadi, wakati huohuo pembeni ya huyo uliyempora kuna pori tupu watu hawalitaki kama sio fikra duni ni nini?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…