Raisi wa awamu ya tano ana kila dalili za kufeli kama hatojirekebisha.
Dalili za awali.
1. Hamna hata waziri mmoja aliyeanza naye ambaye sasa wanaenda wote kwa ile kasi ya mwanzo. Maana yake wameshagundua kuwa gari imepotea dira na chombo ndio kinaenda mrama!
2. Maamuzi yote ya kukurupuka yameleta madhara zaidi kuliko faida kwa wananchi. Rejea Bomoabomoa ya mabondeni, sukari, ada elekezi na hili la vilaza!
3. Kukosa support toka chamani ni ishara tosha, serikali anazungumza kichina na chama kinazungumza "kidhungu" hapo lugha gongana kabisa!
Kwanini Magufuli atafeli na anaweza kuishia kutawala awamu 1.
1. Anachofanya raisi kwa sasa ni kitu cha ajabu kabisa. Anaishi kama nchi haikuwahi kuwa na dira na wala chama chake hakikuwa na Sera na ilani za chaguzi zilizopita. Dr. Slaa alishayafanya haya ya kutumbua majipu lkn watu hawakumchagua kwa kuwa wao walitaka taasisi yenye dira kuliko mtu mwenye nguvu!
Magufuli anatawala kama raisi wa upinzani, yet kwa karibu miaka 20 alikuwa anatuambia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm! Leo anashangaa na kufuta kila kitu!
2. Raisi wa sasa amefuta na kudumaza taasisi zote imara zinazoisaidia serikali, na sasa yeye ndiye mwenye nguvu na mtendaji pekee! Huu ni utawala wa kifalme (Monarchy) ndio mfalme ana absolute power!
Mkuu unapunguza nguvu ya CAG leo unamnyima pesa CAG Ila unampa pesa Jaji Mkuu kwa mahakama ya majizi ambayo ina substitute mahakama nyingine nyingi, unahamisha pesa muhimu za kazi mbalimbali na kuzipeleka barabarani lkn unamnyima huyu msimamizi mkuu wa pesa za umma!
Serikali yako inalinyima bunge nguvu huku ukihubiri kusaka wezi na kusimamia haki! Hadi sasa kesi zilizogundulika na kuhukumiwa na bunge ni kubwa na nyingi kuliko zilizosimamiwa na mahakama zote toka Uhuru! Kesi ya Richmond, EPA, Escrow, Lugumi zote ziliibuliwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa na wabunge wetu! Kesi zote hizo hamna hata moja iliyochunguzwa, kusimamiwa ama kuhukumiwa na chombo chochote cha serikali na hata kama vipo uchunguzi wake umeishia ktk makarabrasha!
Leo serikali kipenzi cha Mungu, nyinyi watenda haki mnapunguza nguvu za taasisi zinazosaidia na kusimamia haki zitendeke!
Raisi na serikali yako, sisi tunataka matokeo mazuri tu, na ahadi zako ni njema kweli!
Shida kuu ya awamu hii, mnashindana na awamu iliyopita, hamtaki kufanya muendelezo hata wa Yale mema ya awamu zilizotangulia! Mkumbuke Mwl alichosema "wao kuna mambo mazuri wamefanya na yapo ya kijinga, chukueni Yale mazuri na ya kijinga achaneni nayo", nyinyi mnaacha yote!
Failure is guaranteed;
Hadi mh. Umeanza kazi, hakuna taasisi aliyoijenga, kikwete pamoja na watu kumuona dhaifu lkn aliijenga ofisi ya CAG, alipanua demokrasia bungeni, alilijenga jeshi la polisi na jeshi la wananchi, alijenga barabara, alifufua elimu, alikuza mifuko ya hifadhi za jamii, shirika la nyumba, reli, kuliko (kilimo kwanza), nishati (umeme, gesi)!
Wewe miezi 6 sasa, ni kukamata, kutukuza, kufuta, kuteua, kugawa mali za watu etc!
Brother, every second counts, ni sasa or never!
Si chamanichamani wala serikalini ambapo tunaona legacy, hatuoni mfumo rasmi unaoutengeneza vinginevyo una create vacuum, siku ukiwa haupo ofisini kila kitu kitasimama au tutaanza upya!
Please mh. Raisi kaa chini, tengeneza task force ya watu watakaokushauri, tafuta strong person level ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Malecela, Warioba, Mwamnyange, Pinda, Sitta, Msuya, Pengo, Karume etc! Tafuta watu ambao hawatakuogopa, watu waliojitosheleza kimadaraka, wenye upeo na uongozi wa muda mrefu ili wakushauri! Jifanyie semina elekezi kwanza, kisha unda team ya kudumu na jopo la wazee wa kuwa consult!
Una uwezo mkubwa, unadhamira ya dhati, lkn skills za uongozi na mbinu za kisiasa upo butu sana! Unahitaji kujifunza na kujifunza sio ujinga! Ni wapumbavu tu ndio wataobeza au kucheka wazo hili, lkn kiukweli hata mwenyewe unajua ndani ya nafsi yako hukuwa president material, umeupata uraisi bila ya kujiandaa, unachojua tu ni kuwa unaweza! Ni kama dereva wa basi kapewa trekta!