Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....

HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!

Tatizo sio kuviandika kaka. Tatizo utekelezaji na upimaji wa utekelezaji kwa dhati. JK naye aliandika na semina elekezi alizifanya nyingi lakini unajua alikotuacha.
 
Fuatilia habari. Makamu wa Rais amesema kwa kipindi hiki wananyoosha nchi ilikwishapinda kwa hiyo watu watapata maumivu kidogo. Baada ya hapo tutakwenda vizuri. Sasa unaeuliza tunakopelekwa ni wapi jibu lako holo.
 
Mbowe na kina Lissu wameharibu sana watu humu, yaani hakuna watu walichoona ila ni wanafunzi 7000 na Sukari tu..hicho ndio kupimo cha Rais bora kweli, acheni kukatisha watu tamaa bhna. .kazi ya JPM ni ngumu sana kuliko watu wanavyodhani. .na wale wapinzani ni sehemu ya kazi yao makelele ili watt waendee choo.
Mzee JPM piga kazi utasikia kelele nyingi sana nyuma yako huyoooooo, huyooooo mchinje huyoooooo,
Sukariiiiii, wanafunziiiiiiiii 7000 hakuna kugeuka mpaka 2020 uchaguzi mwingine.

Unajua kuhesababu Kaka?


1. Wabunge kusimamishwa kazi za Bunge

2. Maamuzi ya Serikali kuhusu Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma

3. Hali ya Zanzibar

4. Mwelekeo wa Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Rais Magufuli

5. Tishio la Nchi kuelekea kwenye Utawala wa Imla wa MTU mmoja

Charles Elias Misungwi: Hotuba ya Zitto Kabwe katika uzinduzi wa “Operesheni Linda Demokrasia Nchini”.
 
Kazi tu; Fukuza, teua, vunja... Nchi haijengwi hivi brother

Rais wa awamu ya tano ana kila dalili za kufeli kama hatojirekebisha.
Dalili za awali.

1. Hamna hata waziri mmoja aliyeanza naye ambaye sasa wanaenda wote kwa ile kasi ya mwanzo. Maana yake wameshagundua kuwa gari imepotea dira na chombo ndio kinaenda mrama!

2. Maamuzi yote ya kukurupuka yameleta madhara zaidi kuliko faida kwa wananchi. Rejea Bomoabomoa ya mabondeni, sukari, ada elekezi na hili la vilaza!

3. Kukosa support toka chamani ni ishara tosha, serikali anazungumza kichina na chama kinazungumza "kidhungu" hapo lugha gongana kabisa!
Kwanini Magufuli atafeli na anaweza kuishia kutawala awamu 1.

1. Anachofanya rais kwa sasa ni kitu cha ajabu kabisa. Anaishi kama nchi haikuwahi kuwa na dira na wala chama chake hakikuwa na Sera na ilani za chaguzi zilizopita. Dr. Slaa alishayafanya haya ya kutumbua majipu lkn watu hawakumchagua kwa kuwa wao walitaka taasisi yenye dira kuliko mtu mwenye nguvu!

Magufuli anatawala kama rais wa upinzani, yet kwa karibu miaka 20 alikuwa anatuambia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm! Leo anashangaa na kufuta kila kitu!

2. Rais wa sasa amefuta na kudumaza taasisi zote imara zinazoisaidia serikali, na sasa yeye ndiye mwenye nguvu na mtendaji pekee! Huu ni utawala wa kifalme (Monarchy) ndio mfalme ana absolute power!

Mkuu unapunguza nguvu ya CAG leo unamnyima pesa CAG Ila unampa pesa Jaji Mkuu kwa mahakama ya majizi ambayo ina substitute mahakama nyingine nyingi, unahamisha pesa muhimu za kazi mbalimbali na kuzipeleka barabarani lkn unamnyima huyu msimamizi mkuu wa pesa za umma!

Serikali yako inalinyima bunge nguvu huku ukihubiri kusaka wezi na kusimamia haki! Hadi sasa kesi zilizogundulika na kuhukumiwa na bunge ni kubwa na nyingi kuliko zilizosimamiwa na mahakama zote toka Uhuru!

Kesi ya Richmond, EPA, Escrow, Lugumi zote ziliibuliwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa na wabunge wetu! Kesi zote hizo hamna hata moja iliyochunguzwa, kusimamiwa ama kuhukumiwa na chombo chochote cha serikali na hata kama vipo uchunguzi wake umeishia ktk makarabrasha!

Leo serikali kipenzi cha Mungu, nyinyi watenda haki mnapunguza nguvu za taasisi zinazosaidia na kusimamia haki zitendeke!

Rais na serikali yako, sisi tunataka matokeo mazuri tu, na ahadi zako ni njema kweli!

Shida kuu ya awamu hii, mnashindana na awamu iliyopita, hamtaki kufanya muendelezo hata wa Yale mema ya awamu zilizotangulia!

Mkumbuke Mwl alichosema "wao kuna mambo mazuri wamefanya na yapo ya kijinga, chukueni Yale mazuri na ya kijinga achaneni nayo", nyinyi mnaacha yote!

Failure is guaranteed;

Hadi mh. Umeanza kazi, hakuna taasisi aliyoijenga, kikwete pamoja na watu kumuona dhaifu lkn aliijenga ofisi ya CAG, alipanua demokrasia bungeni, alilijenga jeshi la polisi na jeshi la wananchi, alijenga barabara, alifufua elimu, alikuza mifuko ya hifadhi za jamii, shirika la nyumba, reli, kilimo (kilimo kwanza), nishati (umeme, gesi)!

Wewe miezi 6 sasa, ni kukamata, kufukuza, kufuta, kuteua, kugawa mali za watu etc!

Brother, every second counts, ni sasa or never!

Si chamanichamani wala serikalini ambapo tunaona legacy, hatuoni mfumo rasmi unaoutengeneza vinginevyo una create vacuum, siku ukiwa haupo ofisini kila kitu kitasimama au tutaanza upya!

Please mh. Raisi kaa chini, tengeneza task force ya watu watakaokushauri, tafuta strong person level ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Malecela, Warioba, Mwamnyange, Pinda, Sitta, Msuya, Pengo, Karume etc!

Tafuta watu ambao hawatakuogopa, watu waliojitosheleza kimadaraka, wenye upeo na uongozi wa muda mrefu ili wakushauri! Jifanyie semina elekezi kwanza, kisha unda team ya kudumu na jopo la wazee wa kuwa consult!

Una uwezo mkubwa, unadhamira ya dhati, lkn skills za uongozi na mbinu za kisiasa upo butu sana! Unahitaji kujifunza na kujifunza sio ujinga!

Ni wapumbavu tu ndio wataobeza au kucheka wazo hili, lkn kiukweli hata mwenyewe unajua ndani ya nafsi yako hukuwa president material, umeupata uraisi bila ya kujiandaa, unachojua tu ni kuwa unaweza! Ni kama dereva wa basi kapewa trekta!
 
Mlizoea kuiba , lazima kufukuzwa.
Kuna vijana wengi sana hawana kazi mitaani, lazima kitaeleweka tu.
 
Raisi wa awamu ya tano ana kila dalili za kufeli kama hatojirekebisha.
Dalili za awali.
1. Hamna hata waziri mmoja aliyeanza naye ambaye sasa wanaenda wote kwa ile kasi ya mwanzo. Maana yake wameshagundua kuwa gari imepotea dira na chombo ndio kinaenda mrama!
2. Maamuzi yote ya kukurupuka yameleta madhara zaidi kuliko faida kwa wananchi. Rejea Bomoabomoa ya mabondeni, sukari, ada elekezi na hili la vilaza!
3. Kukosa support toka chamani ni ishara tosha, serikali anazungumza kichina na chama kinazungumza "kidhungu" hapo lugha gongana kabisa!
Kwanini Magufuli atafeli na anaweza kuishia kutawala awamu 1.
1. Anachofanya raisi kwa sasa ni kitu cha ajabu kabisa. Anaishi kama nchi haikuwahi kuwa na dira na wala chama chake hakikuwa na Sera na ilani za chaguzi zilizopita. Dr. Slaa alishayafanya haya ya kutumbua majipu lkn watu hawakumchagua kwa kuwa wao walitaka taasisi yenye dira kuliko mtu mwenye nguvu!
Magufuli anatawala kama raisi wa upinzani, yet kwa karibu miaka 20 alikuwa anatuambia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm! Leo anashangaa na kufuta kila kitu!
2. Raisi wa sasa amefuta na kudumaza taasisi zote imara zinazoisaidia serikali, na sasa yeye ndiye mwenye nguvu na mtendaji pekee! Huu ni utawala wa kifalme (Monarchy) ndio mfalme ana absolute power!
Mkuu unapunguza nguvu ya CAG leo unamnyima pesa CAG Ila unampa pesa Jaji Mkuu kwa mahakama ya majizi ambayo ina substitute mahakama nyingine nyingi, unahamisha pesa muhimu za kazi mbalimbali na kuzipeleka barabarani lkn unamnyima huyu msimamizi mkuu wa pesa za umma!
Serikali yako inalinyima bunge nguvu huku ukihubiri kusaka wezi na kusimamia haki! Hadi sasa kesi zilizogundulika na kuhukumiwa na bunge ni kubwa na nyingi kuliko zilizosimamiwa na mahakama zote toka Uhuru! Kesi ya Richmond, EPA, Escrow, Lugumi zote ziliibuliwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa na wabunge wetu! Kesi zote hizo hamna hata moja iliyochunguzwa, kusimamiwa ama kuhukumiwa na chombo chochote cha serikali na hata kama vipo uchunguzi wake umeishia ktk makarabrasha!
Leo serikali kipenzi cha Mungu, nyinyi watenda haki mnapunguza nguvu za taasisi zinazosaidia na kusimamia haki zitendeke!
Raisi na serikali yako, sisi tunataka matokeo mazuri tu, na ahadi zako ni njema kweli!
Shida kuu ya awamu hii, mnashindana na awamu iliyopita, hamtaki kufanya muendelezo hata wa Yale mema ya awamu zilizotangulia! Mkumbuke Mwl alichosema "wao kuna mambo mazuri wamefanya na yapo ya kijinga, chukueni Yale mazuri na ya kijinga achaneni nayo", nyinyi mnaacha yote!
Failure is guaranteed;
Hadi mh. Umeanza kazi, hakuna taasisi aliyoijenga, kikwete pamoja na watu kumuona dhaifu lkn aliijenga ofisi ya CAG, alipanua demokrasia bungeni, alilijenga jeshi la polisi na jeshi la wananchi, alijenga barabara, alifufua elimu, alikuza mifuko ya hifadhi za jamii, shirika la nyumba, reli, kuliko (kilimo kwanza), nishati (umeme, gesi)!
Wewe miezi 6 sasa, ni kukamata, kutukuza, kufuta, kuteua, kugawa mali za watu etc!
Brother, every second counts, ni sasa or never!
Si chamanichamani wala serikalini ambapo tunaona legacy, hatuoni mfumo rasmi unaoutengeneza vinginevyo una create vacuum, siku ukiwa haupo ofisini kila kitu kitasimama au tutaanza upya!
Please mh. Raisi kaa chini, tengeneza task force ya watu watakaokushauri, tafuta strong person level ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Malecela, Warioba, Mwamnyange, Pinda, Sitta, Msuya, Pengo, Karume etc! Tafuta watu ambao hawatakuogopa, watu waliojitosheleza kimadaraka, wenye upeo na uongozi wa muda mrefu ili wakushauri! Jifanyie semina elekezi kwanza, kisha unda team ya kudumu na jopo la wazee wa kuwa consult!
Una uwezo mkubwa, unadhamira ya dhati, lkn skills za uongozi na mbinu za kisiasa upo butu sana! Unahitaji kujifunza na kujifunza sio ujinga! Ni wapumbavu tu ndio wataobeza au kucheka wazo hili, lkn kiukweli hata mwenyewe unajua ndani ya nafsi yako hukuwa president material, umeupata uraisi bila ya kujiandaa, unachojua tu ni kuwa unaweza! Ni kama dereva wa basi kapewa trekta!
Mpaka tubadilike n.a. kuheshimu utumishi wa umma. Tulijisahau sana
 
magufuliuraisumekushinda-jpg.354829
 
Watu mna guts mkiwa nyuma ya keyboards zenu!! Haya bana tumesoma japo hako sijui kapicha ama kavideo hakafunguki.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Asante sijui kama wengine wanaliona hili maana kale kawimbo mbele kwa mbele kana effect kubwa sana ukikapenda bila kutafakari zaidi
 
Mnaodai hamzungushi mikono tuambieni tunaelekea wapi kiuchumi? Binafsi najaribu kumsoma sielewi hata taifa la viwanda hakuna hatua zozote za tofauti za kumjulisha mtu kwamba tunaelekea kwenye viwanda,tupotupo tu
Kujua anatupeleka wapi soma ilani ya chama pia rejea hotuba zake.hivi sasa anrudisha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma pia kwa wanasiasa.unajua wabongo tulizoea mambo hovyohovyo kila mmoja analalama ndio maana baadhi ya watu hawamuelewi mqgu
 
Hatujui kwamba ataanza kuboresha kwanza umeme ndo afwate viwanda..

Au aanze viwanda kwanza ndo afwate umeme...
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] hii ndo Bongoland
Viwanda tgen umeme then tuboreshe veta tupate mafundi.......lol
 
Jamani mi niko serious, ninyi mnaleta siasa. Hii ni mada inayoweza kutusaidia na kumsaidia rais tukiondoa ushabiki
Ilani ya chama sio taifa .....lazima aseme anataka nn katika nchi ili watu wasiwe na tension.....maana wqnanchi wakiwa na tension they will never invest katika capacity yao ya kawaida
 
Nadhani tusubiri utekelezaji wa bajeti yake angalau kwa mwaka 1 ndipo tusema kufaulu au kufeli kwake.Kumhukumu kwa sasa ambapo anamalizia mngwe iliyoachwa na JK hatumtendei haki maana hatujui kwenye akaunti yetu kulikuwa na chochote au madeni tu!!!!!????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom