Hofu yangu juu ya yanayoendelea nchini
Ni dhahiri sasa bila kumung'unya maneno nchi hii inaelekea katika ombwe la Demokrasia.
(1) Tulianza kwa kuona nyumba za wananchi mabondeni zikibomolewa bila huruma, tushukuru mahakama ilipifa stop lile zoezi la sivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.
(2)Tumeona Bunge likiminywa, lisionekane Live
(3) Tumeona watu wakisimamishwa kazi hadharani kwenye majukwaa ya kisiasa
(4)Tumeona watoto UDOM, waliodahiliwa na serikali ileile ya CCM wakifukuzwa kwa notisi ya masaa machache tu
(5) Tumeona wafanyabiashara wakitaitiwa, wakipelekewa vyombo vya dola eti wameficha sukari.
(6)Sasa tunashuhudia Vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya siasa
HOFU YANGU.
(1) Mitandao ya Kijamii yenye Sauti kama JF kuanza kusumbuliwa
(2) Kubambikiana Kesi, ili kuwanyamazisha watu wenye kuukosoa utawala huu
(3) Kufukuza watu Kazi kisiasa, kuwapelekea wafanyabiashara bili za kodi kubwa
(4) Watu kupotezwa
TUNAFANYAJE?
(1) Tuwaunge mkono Wabunge wote wenye kuweka mbele maslahi ya Umma badala ya vyama vyao
(2) Ni lazima Vyombo vya habari viwe jasiri kuliita Sepetu, Sepetu
(3) Ni lazima tuendelee kuzungumza, kupiga kelele na kuusimamia ukweli
(4) Kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuwaelimisha wananchi madhara ya Ubanaji huu wa Demokrasia unaotamalaki kwa kasi nchini, vijiwe vya kahawa, vijiwe vya magazeti, kwenye magulio huko vijijini, misibani, kwenye vikao vya kifamilia, sherehe n.k
(5) Wasomi wetu, tunawahitaji kuliko wakati wowote ule tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni lazima wasimame bila woga
(6) Ni muhimu sana kuitumia mahakama kwa ajili ya kudai haki
Nchi hii tulipigania uhuru siyo kwa ajili ya barabara, maji na umeme peke yake, Tulitaka uhuru wa Kuendesha nchi yetu kidemokrasia, Tulitaka heshima ya kujitawala kwa maana uongozi unaoheshimu raia, unaolinda haki za binadamu, unaoheshimu uhuru wa watu wake, unaoheshimu utu na uongozi wa sheria.
Katika vitu ambavyo Watanzania hawatokubali na ninawatahadharisha viongozi wote wa leo na Kesho ni kwamba kwa mujibu wa misingi iliyowekwa na waasisi wanchi hii, Kamwe Watanzania hawatakubali Kuburuzwa Kiimla. ile hasira ya Umma waliyokutana nayo mwaka 2015, inaweza ikageuka mara kumi yake!, Ni hatari, naogopa sana! . Ni vizuri wakajifunza na kulijua hili.