Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
We mbona hujadili mwelekeo wa chadema? Mna Sera ipi kwa sasa, je ya sukari, au kupambana na ufisadi au ipi hasa??
Kinachozungum,ziwa hapa ni mwelekeo wa taifa sio vyama soma tena kwa umakuni utamwelewa mtoa mada ana manisha nini
 
kikwete aliwahi kuulizwa hivi.....''unataka wananchi wakukumbuke kwa lipi katika utawalawako huu wa miaka 10??''...akajibu..''nataka wanikumbuke kuwa niliwatoa hapa na kuwapeleka pale''...kwa huyu wa sasa anatupeleka hapa....sio pale..
Kwa hiyo alituacha pale?
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Very poor comment,duuuhhh
 
Vumilia uko safarini unaweza kuona kibao cha ulipofika kama ww ni mgen
 
Wadau,

Binafsi hali ninayoiona inaendelea nchini ni kama kuna deadlock , tumekwama kwa kweli. Najaribu kujiuliza ni sahihi kuzidharau kura Milioni sita (6,000,000) kama si chochote si lolote? Hapana! hivi ni kweli wale wafuasi wa Lowasa ndani ya bunge na CCM na jamii wameyeyuka? mbona hawajawahi kumkana?.

Kwa maoni yangu ni kuwa, maono ya mitazamo ya Lowasa yangali hai ndani ya vifua vya wafuasi wake ndani ya serikali, kwenye chama na kwa jamii yote, hawa watu kwa namna moja au nyengine wanakwamisha utendani na mipango ya hii serikali ya hapa kazi tu.

Ushahidi wa haya ni kuona kwamba hadi sasa miezi 7 tokea Magufuli aapishwe, bado kila akifanya ziara sehemu yoyote anakumbana na madudu utafikiri hakuna uongozi katika sehemu husika, hii ni ishara ya wazi kuwa, watendaji anaowaamini wamemsusia mzigo aubebe mwenyewe, hakuna team work wala hakuna mipango ya pamoja.

Ndani ya siku chache zijazo, tutashuhudia upinzani wa wazi wazi ndani ya chama na serikali kama ambavyo tumeanza kushuhudia.

Ushauri wangu: Magufuli amshirikishe Lowasa ili mambo yaende, sisemi apewe nafasi la hasha! ila afanyie kazi baadhi ya mawazo chanya.

Ni hayo tu

Tume ya katiba

Mcheza Pool Table.
 
Kwani lowasa ni kijana ambaye hajala hela chafu, sasa hivi Magufuli anataka kuanza na Damu safi, ambayo haijakula Nyama ya Mtu!!
 
Hivi mkuu makusanyo ya mwezi April yalikuwa trilioni ngapi? Na za mwezi May je?

Zamani tulikuwa tunatangaziwa mapato na matumizi ya serikali lakini kwa sasa ni kimya kabisa. Pia ukiongea na watumishi serikalini watakwambia hakuna hela ya DEVELOPMENT imetumwa mwezi wa nne na wa tano, pia hata hela ya kuendesha ofisi maarufu kama OC haijatumwa kwa miezi miwili. Hii ni dalili kuwa nchi haina muelekeo mzuri kiuchumi ingawa sisi wengine tunampa muda huyu nahodha wetu hadi atakapoanza kutekeleza bajeti yake mwezi July
 
Hahahahahaaaaaa! Fisadi ajumuishwe kwenye serikali ya Magufuli? Hiyo si sawa na shetani kumshirikisha kwenye mamlaka ya Malaika? Au ni sawa na fisi kumshirikisha kazi ya ulinzi ya zizi la Mbuzi? Hahahahahaaaaa. Magufuli si dhaifu kiasi hicho. Hawezi kufanya makosa kama hayo
 
Kwani lowasa ni kijana ambaye hajala hela chafu, sasa hivi Magufuli anataka kuanza na Damu safi, ambayo haijakula Nyama ya Mtu!!

Mkuu Magufuli anasema Vijana sio wapiga deal....sijui kaufanyia wapi utafiti huu.
 
Hahahahahaaaaaa! Fisadi ajumuishwe kwenye serikali ya Magufuli? Hiyo si sawa na shetani kumshirikisha kwenye mamlaka ya Malaika? Au ni sawa na fisi kumshirikisha kazi ya ulinzi ya zizi la Mbuzi? Hahahahahaaaaa. Magufuli si dhaifu kiasi hicho. Hawezi kufanya makosa kama hayo

Mkuu huyu "Fisadi" aliaminiwa na watu milioni 6, inawezekana kuchukua ushauri wa shetani kama ushauri huo una kweli ndani yake.
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!

Acha kutoa povu kijana, buku 7 utakula siku ngapi?
Hapa tunajadili mustakabali wa Taifa na huu ni ukweli kwamba bado Taifa letu halina Dira, Mwanga,Muelekeo,Malengo,Namna ya Utatuzi n.k. wa Umasikini,Maradhi,Ujinga,Ufisadi, n.k.nk.

Kwa mfano leo Taifa letu liko mkiani nafasi ya NNE katika nchi ya tunaoishi Chini ya Mstari wa Umasikini ( Under Poverty Line).
Hebu acheni kufikiri kwa kutumia MATUMBO, maana sasa hii ni laana huenda toka kwa Mungu.
 
Hama nchi au ukishindwa saga chupa unywe!
 
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifa
Kwa hiyo wewe umeona miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali hakuna sio...?????
Kama umeshindwa kuangalia kusoma na kutathmini, usiseme hujui tuendako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom