Tatizo na wewe hutaki kuona wala kuelewa. Kwani kushughulika na watumishi hewa ni nini? Ama kupunguza matumizi yasiyo na tija (mfano; safari, posho, matamasha, n.k..) wewe unaona ni kitu gani kwani?
Msilete hoja/mada za kishabiki humu halafu mkijibiwa kishabiki muone wanaowajibu kuwa ni punguani.
Maendeleo gani unayotaka kuyafikia bila kuchukua hatua za udhibiti, kurekebisha maadili na uwajibikaji?
Wewe mwenyewe ukiulizwa dira yako ni ipi, hata majibu huna halafu unataka serikali ije na dira?!!! Toa boriti jichoni mwako ndipo uone kibanzi kwa mwenzako.
Nakushauri ongeza juhudi kufanya kazi, lipa kodi shauri na familia yako yote ifanye hayo, jirani zako, ukoo wako nao pia kisha rudi hapa kuuliza tena hayo maswali yako.