Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Yeye mwenyewe hajui anapotaka kutupeleka!
 
Mmmm ndio unaweza kuwa na dereva mzuri asiyejua mwelekeo.....Na hii ni hatari coz unaweza kujikuta unatumbukia mtoni....kama tulivotumbukia kwenye mtaro wa sukari najua hii imekua ni ajari ya ghafra ambayo JPM hakuitegemea....najua tutatoka ktk huu mtaro lkn sijui ni mpaka lini coz hii inatuasili sisi wachini sanaaa.
 
Magufuli sasa serikali yake imepoteza muelekeo kwani haina kipaumbele cha kuanza nacho, wanataka wafanye vitu vingi kwa mda mfupi matokeo yke hali ya kiuchumi kwa mwananchi wa kawaida imekuwa mbaya zaidi... Mtazamo wng tuendako ni kubaya zaidi huwez kusema uchumi wa taifa umekua huku wananchi wke wakiwa na hali mbaya....
 
Kanani, na tumeshafika kwa imani, mji mzuri uliyojaa maziwa na asali....amini usije baki jangwani...au ukauona mji lakini usiukajage...kuwa positive na amini mambo yote yatakuwa shwari......Mwenye Enzi Mungu ni mwaminifu sana katika kila jambo.... kipindi cha Mwl. JK Nyerere Tanzania nchi yetu tulitoa wanajeshi chungu mzima kwenda kutetea Waafrica wenzetu ili nao wawe huru kama sisi, ile damu ya Watanzania iliyomwagika ina thamani kubwa mno mbele ya Mwenye Enzi Mungu....Tumtumaini naye atatushindia..tuendelee kumwombea Mh Raisi wetu kwa baraka tele yeye na familia yake asipatwe na mabaya, na juu zaidi mama yetu Tanzania tumlinde na kila mtu awajibike katika sehemu yake....have a blessed day my friend
 
This is serious naomba niwajue watu wanao plan economic strategy za nchi
 
Masuala ya msingi kama haya aliyojaribu kuhoji mleta mada yanatakiwa yapatiwe mchango stahiki kama hoja yenyewe.

Tusifanye siasa kwa kila hoja. Hii nchi ni urithi wa vizazi vijavyo tusiiharibu jamani.
 
Masuala ya msingi kama haya aliyojaribu kuhoji mleta mada yanatakiwa yapatiwe mchango stahiki kama hoja yenyewe.

Tusifanye siasa kwa kila hoja. Hii nchi ni urithi wa vizazi vijavyo tusiiharibu jamani.
Hajaleta maswala yoyote hapa bali kutwambia kwamba ameduwaa hajui aendako; namshauri aumize kichwa, ayasome mazingira, atajua tunakoelekea; A fair, just and equitable society; serikali inayokusanya kodi, nchi ambayo kila mtu anakula mapato ya juhudi zake za kazi halali, na nchi isiyotukuza majizi, majangili na mafisadi ya mali ya umma, nchi ambayo mapato ya serikali yanatumika kuinua hali ya maisha ya wananchi wake wote bila ubaguzi au kuwanufaisha wachache walioko kwenye utumishi wa umma. Period
 
Tupe strategy tunafikaje huko siyo kupiga ramli
 
This is serious naomba niwajue watu wanao plan economic strategy za nchi
tatizo linaloweza kuwepo ni washauri kushindwa kumshauri mshauriwa ,...na hivyo wao washauri kugeuka washauriwa wa yule waliyepaswa kumshauri
 
Tatizo ni kufanya kila situ siasa. Kama serikali imechemsha katika suala la sukari, hakuna haja ya kuuma uma maneno. Lazima tuseme ukweli. Hakuna mwana CCM au Mwanachadema, kila mtu akienda dukani bei ya sukari ni kuanzia shs 3,000, na tena haipatikani. Serikali imeingia madarakani nchi ikiwa na sukari ya kumwaga, na bei haikuwa inazidi shs 2,000 kwa kilo. Nini wamefanya? (Wanajua wenyewe), lakini kile walichokifanya ni KIBAYA na HAKIKUBALIKI. Na sisi wabongo tujifunze kusema ukweli na kuwa wawazi. Kusifia na kushangilia tu kwa kila kitu hatutafika mbali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom