Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kama hujui unakoelekea ni wewe sisi tunajua magufuri anatupeleka kwenye raha sasa wewe tunaomba ukae pemben usubiri 2020 uzungushe kiuno maana haitakuwa mikono tena.
Acha ujinga jibu hoja.
 
Kuna watu flani wenyewe wakiona
Rais hata nakosea kazi yao kubwa ni kupiga makofi tu wanaogopa kusema ukweli wanahisi watawastukia kwamba wametumwa na upinzani.
 
Alichokifanya mheshimiwa rais tangu aingie madarakani ni kugaragaza mafisadi, kuziba mianya ya rushwa na kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato. Hiyo ni hatua moja muhimu sana kwa taifa linalotaka kupiga hatua za maendeleo. Kutoa tathmini kwamba tunaelekea wapi kwa sasa ni mapema mno ingawa dalili njema zinaonekana. Ni muhimu kukumbuka kuwa bajeti yake mheshimiwa rais bado inajadiliwa bungeni, kwa hiyo tusubiri angalau mwaka mmoja hivi baada ya bajeti yandiyo tuseme kwamba tunaelekea wapi.
 
Kwa mzungusha mikono kama wewe huwezi jua muelekeo wa nchi...subiri 2020 uwazungushie tena mikono
Ifike mahali ushabiki wa vyama tueke pembeni....
"Sukari 3600"[emoji25] [emoji25] [emoji25]
 
Wandugu,
Kuna jamaa hapa kaanzisha thread ya kuuliza swali kuwa ni Nani anayejua Rais Magufuli anakowapeleka Watanzania, anafikiri Rais amepotea njia, na Mimi nikaona ni busara nimjibu tu hiviii "Wewe tembea tu umfuate Rais wakati mwingine sio busara kuuliza Safari inakoelekea wakati wewe mwenyewe huna mwelekeo. Waache wenye GPS watangulie wewe fuata nyuma yao, huenda na wewe ukawa kwenye vitabu vya history ya hii Safari Muhimu ya Rais wetu kuelekea nchi ya Ahadi. Kama una wasiwasi Mtumie text Nabii Musa umuulize wakati anaanza safari misri kuelekea Israel wakimkimbia farao Wayahudi wangapi walikuwa wanajua alikokuwa akielekea. Na kuna wengine wamlidhihaki wengine walimtukana na kuuliza maswali yasiyo na majibu. Lakini Leo hii zaidi ya miaka 2000 Wayahudi wanakula matunda ya safari ya Musa, maskini Musa mwenyewe hata safari hakumaliza.
Sasa wewe ndugu, tembea tu kama hutafika wajukuu zako watafika, na foot print ya Safari yako na Rais wetu itabaki kwenye historia ya Vitabu vyetu.
Nakutakia Safari njema.
 
Hivi huyu jingalao kumbe ni bwege zaidi ya ujinga. Mbona atadhaurika hata na nafsi yake. Yaani tukiwa na watanzania watano km jingalao Bora tuolewe na watulawit. Maana hakuna jinsi. Mimi natokeza Mara chache kupata ufahamu wa mambo humu, lkn jingalao km jina
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Wewe ndiye unayejua maana umeshasema tayari "tumepotea" sasa unataka wanachojua wengine sio!!
 
Nchi ya ahadi?? Acha kumfananisha nabii wa Mungu na Magufuli. Safari yenye walevi bungeni safari gani hiyo?? Safari ya kukurupuka bila kujiandaa safari gani hiyo.
 
Wewe ambaye huzungushi mikono na unayejua mwelekeo si utwambie tunaelekea wapi?
....unataka uambiwe nn wakati ume conclude tumepotea!!, unauliza ili ujisahihishe, ujikosoe, au ndo kuzungusha mikono siku ziende
 
Anatupeleka kwenye nchi iliyojaa maziwa na asili we shusha mikono chini acha kuizungusha hakika utaelewa tunaelekea wap
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Dr Makufuri na uendeshaji wake wa nchi kwa mihemko kama hatupeleki kuzimu basi anatupeleka jehanamu...kataa au kubali lakini huu ndio ukweli....na wote TUTAISOMA namba kwa pamoja...uwe mwanaLumumba au raia wa kawaida, kusoma namba kupo palepale. Iko siku tutapanga foleni kwenye maduka ya kaya (atakayoyaita MADUKA YA MAGUFURI) kununua nguo, kiberi, sabuni au mafuta ya kula.
 
Rais Magufuli amepewa urais na Mungu na maono ya Safari anataka kuwapeleka Watanzania anayo nyie ukawa mfateni tu mtafika. Katika safari ya mabasi ya mwendo kasi hata vitz vinajichomeka vinapigwa pasi vinakaa sawa
 
Treni inarudi kwenye njia yake...Kitu kizito kikipoteza uelekeo kurudi ktk njia yake ni kimbembe....Mbona kinarudi lazima kirudi.
 
Swali ni lamsingi kwelikweli mdau anataka kufahamu cha ajabu Sasa wachangiaji mnaleta ushabiki na kutupiana vijembe. Hakuna anayepinga kwamba raisi hana nia njema ishu ni kwamba strategies (mbinu) za kutimiza hizo nia njema

Mbinu (strategy) ya kwanza ni kupiga marufuku uingizaji wa sukari toka nje ili iadimike madukani na wachache waliyonayo waiuze kwa bei ya juu ili wame make profit kubwa!!
 
Nchi ya JPM inajengwa kwenye vyombo vya habari,serikali inahubiri mambo mazuri kupitia vyombo vya habari lakn kwenye uahalisia mambo hayaendi;mf ishu ya sukar bei elekezi ni ndoto,raia tunazid kuteseka,sukari bei juu,
Elimu bure ndio hovyo kabisa,mashuleni mambo hayaendi,wakurugenz na maafisa elimu wanashindwa kumweleza Mh. Magu ugum na changamoto kwa hofu ya kutumbuliwa jipu na kuonekana wanagomesha agizo,..
Mpaka sasa nchi haieleweki inaelekea wapi,sana sana ni shida tu znazid kuongezeka uraiani..
Ongezea apo...yan utendaji kazi wa watumishi binafsi na haswa wa umma umegubikwa na misingi ya woga uliopitiliza badala ya kusimamia kweli na haki!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anaye[/QUOTE

huwez jaza maji kwenye chombo kilicho toboka
so, nadhani anazba matundu kwanza ndo ajaze maji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom