Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hii ni sawa tu na watoto kumlalamikia baba au mama yao kuwa ni mnoko anawapa wakati mgumu. Sawa, kwa uelewa wao mdogo wanakuwa sahihi, lakini kwa aliyepevuka kiakili atagundua kuwa wakifanyacho wazazi kwa watoto ni sahihi. Mwisho wa siku hao hao watoto, wakishafikia umri wa utu uzima, watajirudi na kuanza kuwasifia wazazi wao kwa kuwapa malezi safi kabisa yaliyowajenga kimaadili.
Hakuna mzazi mwenye nia mbaya na makuzi ya mwanae. Vilevile mzazi akifuata maelekezo au malalamiko ya watoto kuhusu malezi kwa hakika ataharibu tu mfumo mzima wa malezi bora.
Nyie ndio mnazidi kumpoteza!
 
Nimesoma kanibania ajira, Nimekuwa machinga polisi wake wanavurumisha kama jambazi kila siku. Mtu anaekula kwa shida, atapata wapi pesa ya bundle. Anatumia www.freebasics.com Hakuna anayemsingizia, yeye ndie anaeua ndoto za vijana wa taifa hili.
- Usajili wa makampuni na trademarks gharama kubwa
- Machinga unapigwa na polisi
- Watumishi hawapati hata increment yeye watu wake wanalipana LAKI 4 per day
- Kakwamisha ajira, vyeo na nafasi mpaka jeshini

Hayo mazingira yako wapi wakati MALIPO ya PAYPAL yamewashinda
mijitu na PhD zao wakati Kenya ipo. In short anaua NDOTO za vijana wa Taifa hili kwa KASI Kubwa sana

Sema ameua ndoto za WAKORA kwa kasi kubwa, lakini ndoto za vijana wapenda kazi, wenye kujituma na kupenda taifa lao, ziko palepale
 
Sema ameua ndoto za WAKORA kwa kasi kubwa, lakini ndoto za vijana wapenda kazi, wenye kujituma na kupenda taifa lao, ziko palepale
Ni kweli ziko palepale kwenye KUBET, UMACHINGA, BODABODA, MANAMBA, JOBLESS
 
Sema ameua ndoto za WAKORA kwa kasi kubwa, lakini ndoto za vijana wapenda kazi, wenye kujituma na kupenda taifa lao, ziko palepale
Ni kweli ziko palepale kwenye KUBET, UMACHINGA, BODABODA, MANAMBA, JOBLESS, BAHATI NASIBU NK
 
Mkuu nimesema kulitia Taifa hasara kwa maamuz yake ya gafla unaweza uone ni kitu kidogo lakin kina athari kubwa sana kwenye uchumi wa nchi ni sawa na kuwa fisadi tu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Mkuu kama maamuzi gani ambayo hayana maslahi kwa taifa?Hebu tunaomba mfano.
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.
No free lunch
 
Kweli mwanzo niliona manyunyu ya udikteta sasa ni mvua ya udikteta kamili nchi hii
Nchi yetu ilikua ya mfano kidemokrasia leo hii imegeuka kama rwanda au zimbabwe
Wapinzani wamegeuka maadui nchi hii
Leo hii kumegeuka ubaguzi mkubwa kwa misingi ya uchama
Wengine wakifanya mikutano ni ruksa wengine ni haramu kufanya hivyo
Ila wajue kuwa mkuki ni kwa nguruwe tu ila kwa binadamu mchungu
Nchi imekua ya kidteta hii ******** na utawala wake wamegeuka watu wabaya na wanyanyasaji wa wananchi
Nchi imegeuka ya wachache tu ndo wanafaidi
Halafu anataka tumuombee who are u mpaka uombewe?
Leo hii kuvunja katiba kunaonekana wazi kabisa
Dalili zote za utawala wa mabavu nchi hii zimekwisha onekana
Ni kichaa pekee atakayejaribu kukanusha kuwa eti tanzania udikteta haujatamalaki ukweli ni kuwa udikteta upo na ndo tumeingia kwenye udikteta kamili
Natoa onyo tu kwa serikali ya ccm wasidhani watatawala milele wajue kuwa karibuni maji yatazidi unga
Hatuwezi kukubali nchi yetu iliyoongoza ukombozi africa nzima kugeuka kupokea miongozo kutoka rwanda ambayo ni nchi yenye ukabila na chuki tena na mizizi ya udikteta wa kagame
Lazima watanzania tuamke tusikubali kuona katiba na sheria zikivunja na tuamke kwa pamoja kuukemea na kuuondoa huu udikteta uchwara uloshika.mizizi hapa nchini
Walaaniwe madikteta wote na alaaniwe yule dikteta uchwara mvunja katiba
Mwisho wa unyama wa yote kila mtu ataonja mita 3 kaburini
Hatutakubali nchi kugeuzwa karata ya udikteta na ubaguzi wa kichama
 
Udikteta ni aina ya serikali ambayo nchi au kikundi cha nchi inatawaliwa na mtu mmoja (dictator) au kwa uhuru, na nguvu hutumiwa kwa njia mbalimbali ili kuhakikisha kwamba nguvu za taasisi zinabakia nguvu.

Udikteta ni aina ya uhuru, ambapo wanasiasa hutawala karibu kila nyanja ya tabia ya umma na binafsi ya raia. Udikteta na jamii za kikatili kwa ujumla hutumia propaganda za kisiasa ili kupunguza ushawishi wa wasaidizi wa mifumo ya udhibiti mbadala. Katika siku za nyuma, mbinu mbalimbali za kidini zilizotumiwa na waasi wa dikteta ili kudumisha utawala wao, kama vile mfumo wa monarchiki magharibi.

Katika karne ya 19 na 20, monarchies za jadi zilipungua na kupotea. Udikteta na demokrasia ya kikatiba iliibuka kama aina mbili za serikali kuu.
 
Kwa maana hiyo unataka watu wasifukuzwe kazi hata kama hawastahili kuwepo kazini? Ndicho hiki kutu mnacholilia?
Kumbe haukunielewa nimesema mfano aliotoa wa mzazi na mwana hauendani ,ujue mzazi ata akiwa na mtoto jambazi au mtukutu bado atampenda tu.
 
utawala wa awamu ya tano umevunja katiba kwa kiwango kikubwa sana. tungekuwa na bunge makini jpm alipaswa kuwajibishwa na bunge
 
Kweli mwanzo niliona manyunyu ya udikteta sasa ni mvua ya udikteta kamili nchi hii
Nchi yetu ilikua ya mfano kidemokrasia leo hii imegeuka kama rwanda au zimbabwe
Wapinzani wamegeuka maadui nchi hii
Leo hii kumegeuka ubaguzi mkubwa kwa misingi ya uchama
Wengine wakifanya mikutano ni ruksa wengine ni haramu kufanya hivyo
Ila wajue kuwa mkuki ni kwa nguruwe tu ila kwa binadamu mchungu
Nchi imekua ya kidteta hii ******** na utawala wake wamegeuka watu wabaya na wanyanyasaji wa wananchi
Nchi imegeuka ya wachache tu ndo wanafaidi
Halafu anataka tumuombee who are u mpaka uombewe?
Leo hii kuvunja katiba kunaonekana wazi kabisa
Dalili zote za utawala wa mabavu nchi hii zimekwisha onekana
Ni kichaa pekee atakayejaribu kukanusha kuwa eti tanzania udikteta haujatamalaki ukweli ni kuwa udikteta upo na ndo tumeingia kwenye udikteta kamili
Natoa onyo tu kwa serikali ya ccm wasidhani watatawala milele wajue kuwa karibuni maji yatazidi unga
Hatuwezi kukubali nchi yetu iliyoongoza ukombozi africa nzima kugeuka kupokea miongozo kutoka rwanda ambayo ni nchi yenye ukabila na chuki tena na mizizi ya udikteta wa kagame
Lazima watanzania tuamke tusikubali kuona katiba na sheria zikivunja na tuamke kwa pamoja kuukemea na kuuondoa huu udikteta uchwara uloshika.mizizi hapa nchini
Walaaniwe madikteta wote na alaaniwe yule dikteta uchwara mvunja katiba
Mwisho wa unyama wa yote kila mtu ataonja mita 3 kaburini
Hatutakubali nchi kugeuzwa karata ya udikteta na ubaguzi wa kichama
mwenziwe (JK) kamuasa kwa lugha ya kiuungwana kuwa kuna maisha baada ya urais. labda ana uhakika wa kuwa rais milele yote...
 
Sasa wewe JPM kakutesaje. Bundle lako la hapa badala ya kusave ufanye shughuli. Unamsingizia JPM.

Wengine wanahonga laki tatu kwa wiki. Ila Maendeleo tu akupe JPM. Wajibu wa Rais ni kusaidiana na System kuweka mazingira ya wewe kuishi kwa amani.

Kupata Muda kama huu wa kuropoka hapa kila siku bila tija wbila mtutu wa bunduki nk nk. Mengine ni yetu. Wewe
Hata nikikuuliza unachotetea moyoni kabisa unajua hukijui. Another hunchback at his own quality!
 
Sasa wewe JPM kakutesaje. Bundle lako la hapa badala ya kusave ufanye shughuli. Unamsingizia JPM.

Wengine wanahonga laki tatu kwa wiki. Ila Maendeleo tu akupe JPM. Wajibu wa Rais ni kusaidiana na System kuweka mazingira ya wewe kuishi kwa amani.

Kupata Muda kama huu wa kuropoka hapa kila siku bila tija bila mtutu wa bunduki nk nk. Mengine ni yetu. Wewe
Hali si hali you rug-headed piece of a person! Vumilia lugha hii! Hivi ukifanya mapenzi na moto huku haujanyoa nywele za "mapajani" unategemea zisiungue kwa mwendokasi!? Falsafa hii ukiielewa utakuwa umekua!
 
Mimi kipato changu kwa muda sasa ni Tsh 1.5m kwa mwezi. Unga niliokua nanunu kwa tsh. 11,000 sasahivi ni tsh. 8,000. Gas ya tsh. 52,000 sasa hivi ni 42,000. Toka tegeta hadi kivukoni ni tsh 600 badala ya 1400.

Nimmpeleka mgonjwa wangu muhimbili, tumepokelewa vizuri alilazwa kwa wiki moja na kufanyiwa operation ya jicho na tulichangia tsh. 120,000 tu, tena kwenye wodi safi na madaktari na manesi wanao nyenyekea wagonjwa. Binafsi naipongeza sana sana serikali ya JPM kwa sababu imenipunguzia makali ya maisha. Ila mimi ni mfanyakazi na nafanya kazi kwa bidii na kazi yangu ainaga magendo.
Acha umbea haikusaidii. Talk the talking itself!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom