Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Miaka kumi! Hivi kumbe mmeisha badilisha katiba?
Najua umenielewa,basi tu.Mkuu kwani Katiba haimruhusu kama akichaguliwa kuendelea na miaka mwingine mitano baada ya kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano kwisha?Au ni ubishi ule ule wa akina Halima na Lissu.
 
"Ukiwa Raisi unatakiwa ujue hali za wananchi wako na kuzifanya ziwe bora",,raisi anapigania matatizo ya jumla kama elimu,dawa,barabara,maji,umeme na miundo mbinu kwa ujumla,tatizo nyie mnaongelea matatizo binafsi ndo maana nilikupa mifano fulani.Ok.. mfano mwingine USA tunaiita LAND OF OPPORTUNITY,ila marekani hiyo hiyo kuna wabongo kibao wanalalamika mambo magumu na kulalamikia system,tofauti kule unakufa kivyako tu,hakuna wakukusikiliza,maana yangu ni kuwa mtu mweusi ameumbwa mlalamishi sana.Tangu serikali ya Nyerere mpaka hii awamu ya tano hakuna siku watu hawajalalamikia serikali hata ingefanya nini.Pambaneni na hali zenu.
Kupambana kwetu inategemea na Sera bora za serkali kuhusu uchumi wa nchi yetu

Naamin ninaposema Sera bora unaelewa haiiishi kupeleka dawa hospitalin tu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Maisha hayajirudii Mara mbili tunahitaji kupiga hatua, tunataka maamuzi yenye tija kwa nchi sio maamuzi yenye hasara kila kukicha.

Magufuli wewe ni mkuu wa nchi, tumekupa kila kitu ili uwe dereva wa nchi yetu.

Sasa kwanini unakosea kila maamuzi unayofanya? Ni kweli watanzania tulikosea kukuchagua?

Magufuli kuwa fisadi sio kuiba Mali ya umma tu hata kulitia Taifa hasara kutokana na maamuzi ya hasira na yasiyofuata sheria ni ufisadi.


Tulikuamini, tukasema Tanzania imepata Nyerere mpya lakini imekuwa tofauti.

Tupo njia panda mkuu Magu hatujui jahazi laenda kus au kas.

Tuliza kichwa Fanya maamuzi sahihi usituharibie nchi.

We live once, miaka mitano au kumi inatosha kabisa kuharibu maisha ya watu kutokana na Sera zako.

This is a wake up call

02 : 35
Sep.05.2017

Usiku mwema

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Any decision you make in life you are responsible for it

2368d7083a3d9c4565b0dcefd5381979.jpg


 
Nchi iko sawa tu..Kwa mfano ukiwa nje ya nchi,ukapitia Jamii Forums kwa wiki 3 au 4 mfululizo,unaweza ukafikiria Tanzania inaungua moto,labda watu hawali hata mchana kwa malalamiko ya humu,ila ukifika bongo ni picha tofauti kabisa,maisha yanaendelea kama kawaida.Kuna mtu alianzisha uzi hapa september mwaka jana akidai hali ya uchumi ni mbaya sana hata wiki tatu hazitaisha yaweza tokea hatari yoyote uchumi usipobadilika,baadae nikagundua yawezekana ilikuwa deadline yake ya kulipa kodi asitolewe vitu nje au kitu kama hicho.Wengi wakizidiwa madeni wanakimbilia JF kulalamika.
Mkuu unaweza kuwa na mawazo sahihi katika ego moja but ukaacha kundi kubwa la watu

Mh maguful bado anakosea mambo mengi na asipobadilika uchumi utayumba

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Tena ule mchele wa tsh.2000 sasa ni 1500. Kitoweo toka tsh7000 hadi 5000. Maji nilikua nalipa tsh 80,000/ kwa mwezi sasa nalipa tsh. 30,000/tena maji safi na ya kutosha. Hapo awali maji yalikua na matope/mchanga. Ujambazi katika eneo letu sasa umepotea. Kwangu maisha yamekua bora zaidi kuliko wakati ule. Sasa hivi nimeanza kununua matofali 300 kwa mwezi na nina matumaini baada ya miezi 10 nitaanza kujenga. Namshukuru sana JPM.
Wasikukatishe tamaa hao mkuu,ni wale Mwalimu Nyerere aliosema watazomea kila jambo jema kiongozi analolofanya kwa niaba ya mapebari.Hao ni makuadi wa mabepari achana nao.Mimi nawaita "huyoo huyoo" maneno ambayo Mwalimu alitumia.
 
.
Mkuu, tafadhali ainisha hapa hayo maisha mabaya wanayoishi watu. Pia tuwekee hapa ni kwa namna gani kiongozi anawatesa watu.

Pia kumbuka hakuna mtu aliyekatazwa kuwa tajiri. Ufukara wa watu ni kutokana na lifestyle yao mkuu, hakuna kiongozi atakuja awe anagawa pesa kwa watu ili kuwakwamua kiuchumi. Kama mnategemea hicho sahauni, hata mitume wakishuka hawataweza kuwaridhisha.

Mara nyingine watu kama nyie ndio mnapalilia umaskini hapa nchini kwa kuamini na kuhubiri kuwa umaskini unasababishwa na serikali. Tumieni raslimali na nguvu zenu kujikwamua, msingoje serikali iwawekee mabomba ya maziwa na asali.


Mkuu, nadhani kuna kitu unakikosa. Jukumu KUU la serikali yeyote ni kuweka Mazingira sahihi kwa watu wake wawe na maisha bora. Mazingira bora ya elimu, afya, KILIMO, biashara, MIFUGO n.k.

Sikiliza ninasema Mazingira bora maana yake nini. Rais hakutakiwa kununua bombardier leo. Alitakiwa awaangalie jeshi kubwa la vijana wanaotoka mashuleni kuingia soko la ajira (ambalo halipo) Mfano; pesa ile angejenga mifumo ya umwagiliaji.

Angalia pesa ya bombardier zote hizo zingejenga mtandao wa umwagiliaji ekari ngapi ? Kwa miaka mitano mtandao huo wa umwagiliaji ungeajili watu wangapi? Nchi ingekusanya kodi kiasi gani. Tungepunguza vibaka wangapi ? Hilo ndilo jukumu la serikali. Ni ujinga kuamini mhitimu atarudi kijijini kushika jembe LA mkono.

Wenzetu Singapore, Malaysia. Korea Kusini, serikali waliweka Mazingira mazuri ya fursa, waliwawezesha wananchi. Isitoshe watu wawe huru katika nchi yao, pasiwe na udikteta, mtu mmoja asiwe ndiyo sheria. Samahani nikutoe kidogo.

Uliona kilichotokea Tanga siku za nyuma kidogo. Mama aliyeingia na bango akitaka Rais amwone ili kudai mirathi yake. Siku ya sheria nadhani. Rais alitoa agizo kwa Jaji Kiongozi hadharani, eti Jaji chukua simu ya mama huyo shughulikia shida yake. Ooh my God. Rais anamwamulisha Jaji Kiongozi !!!!? Rais anaingilia Mahakama !!

Acha ile mpya ya awali; Mahakama wamalize kesi haraka na kuwafunga mafisadi ili awape pesa wanayodai !!!? OK katika hali kama hii, Kiongozi Dragoon utapata nchi na wananchi wenye maisha bora. Kwa kusema hayo siwatetei wala rushwa, wakwepa kodi, wala wapiga dili maofisini.

Hao wapo na wataendelea kuwepo maana hata Marekani, Japan bado wapo. Tujitajidi walau tuwe kama Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.
Ufukara au umaskini uletwa na Tawala mbovu ktk Nchi Husika ....
Pili umesema hakuna Rais /serikali inayo gawa pesa kwa Raia zake sio kweli zipo NCHI DUNIAN hugawa pesa kwa Raia zake tena pesa nyingi tu kwa watu wake wote wasio kuwa na kazi ..



Zimwi likujualo......
 
tatizo lenu meweka high expectations,

na yeye ni binadamu,

mie naamini kwenye mgawanyo wa madaraka,

Nchi igawanywe katika zones,

east wawe na kiongozi wao,

west zone,wawe na wa kwao,

north and south wawe na viongozi wao,

Rais awe mtendaji mkuu wa zones zote,hii itampunguzia mzigo,sio leo makanikia kule,leo sijui vichwa vya treni,for one person its a lot take on,




Huu ni ushauri mzuri kabisa

Bila hata nchi kugawanywa kwenye zone kwa wakati huu angeweza kutumia hata wati wanaomzunguka ana washauri,mawaziri, makam rais, majasusi ya kiuchumi nk

Nchi ingeweza kuwa stable tu kuliko saiv tunapiga maktaim

Mh asiamin katika kile kilichopo kichwani mwake tu kuna watu very intelgence and patriotic awatumie

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Kwa maana hiyo unataka watu wasifukuzwe kazi hata kama hawastahili kuwepo kazini? Ndicho hiki kutu mnacholilia?
Kufukuzwa kazi ni makosa ya mtu bnafis haiusiani na uchumi wa nchi kuporomoka au kuganda

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Hii ni sawa tu na watoto kumlalamikia baba au mama yao kuwa ni mnoko anawapa wakati mgumu. Sawa, kwa uelewa wao mdogo wanakuwa sahihi, lakini kwa aliyepevuka kiakili atagundua kuwa wakifanyacho wazazi kwa watoto ni sahihi. Mwisho wa siku hao hao watoto, wakishafikia umri wa utu uzima, watajirudi na kuanza kuwasifia wazazi wao kwa kuwapa malezi safi kabisa yaliyowajenga kimaadili.
Hakuna mzazi mwenye nia mbaya na makuzi ya mwanae. Vilevile mzazi akifuata maelekezo au malalamiko ya watoto kuhusu malezi kwa hakika ataharibu tu mfumo mzima wa malezi bora.
Unataka kusema wananchi wote tunaufahamu wa kitoto isipokuwa kiongozi wetu mkuu?, nauliza hivyo kwa kuzingatia mfano uliotoa wa mzazi na watoto. kwa kuwa watoto wanakuwa bado hawajapevuka kiakili lakini kwa hili la raisi na wananchi wenzake ni mwafaka kwa mfano wako?.
 
Nilitegemea kuona sehem alipokosea sana hadi ukaamua kuandika uzi huu... Usiwe kama asilimia kubwa ya waandishi wa tanzania kuchukua habari kwenye mitandao na kuandika bila uchunguzi wa kina. Toa ufafanuzi wapi amekosea sana ili ajue ajirekebishe wapi mana kila mtu hukosea...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna mambo mengi hayapo sawa
Mfn mdogo
Watumishi wa umma ambao huwa wanapata annual increment kila mwaka toka aingie madarakan hakuongezea unafikiri wamedhulumiwa kias gani mpaka sasa

Na wasipoongezewa kwa 5 or ten years watadhulumiwa shilling ngap

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Ufukara hauletwi na Raisi wa nchi yoyote,wala hakuna Raisi anayegawa pesa,tafuta alternative pale ulipo kwa namna yako,swala la kulalamikia serikali lipo miaka yote na nchi nyingi za Africa,hatupendi kufanya kazi,tunataka shortcut,tunaishi nje ya uwezo wetu,tunapenda kubahatisha,huna uwezo wa kuweka mafuta kwenye gari unanunua gari la CC 2500 au 3000,umetoka chuo juzi juzi unatangaza ndoa fasta na budget mil 25,mshahara laki 8 unamlipia mtoto milioni 2 kwa mwaka school bus laki na 60 kwa mwezi tena nursery.Kumbe ni michongo ya ofisini,uongozi ukibadilika akaingia mwingine mambo yakabadilika unalalamikia serikali,ikusaidieje?,.,.Kwa waliozoea kula kwa jasho na kuishi ndani ya uwezo tunaona ni poa tu.Kila mtu apambane na hali yake hakuna namna.

Mkuu, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya utawala bora Vs Maendeleo ya nchi. Unajaribu kuonyesha kana kwamba serikali au viongozi wa umma hawana nchango wowote katika maendeleo ya watu. Eti kwamba kila mtu apigane tu kivyake. Huo ni ujinga wako wa mwaka 1947! Kuna uhusiano mkubwa sana, na tena wa moja kwa moja kati ya hivyo vitu viwili.
 
hivi nyie mnaosema vijana wanashinda vijiweni chakula ni serikali inawapa au huwa wanakuja makwenu kuwaomba chakula? niondolee upuuzi hapa
Kuna watu hawajui jinsi watu wanavyopigana mtaan kupata mkate wa siku

Labda hawa wapo ofisi znazozolipa vizur sana

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Hayati Nelson Mandela, aliwaambia wananchi wake kuwa, hawatapata kile wanachokitaka bali watafuata maelekezo yake, na nchi ikasimama kweli. Hii ni baada ya uhuru wananchi wake walitaka vita kuwaondoa wazungu. Haya maneno ya wananchi wa Tz ni sawa na elimu za fursa za ujasiriamali na jinsi zinavyowachanganya wahitimu na wasomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom