.
Mkuu, tafadhali ainisha hapa hayo maisha mabaya wanayoishi watu. Pia tuwekee hapa ni kwa namna gani kiongozi anawatesa watu.
Pia kumbuka hakuna mtu aliyekatazwa kuwa tajiri. Ufukara wa watu ni kutokana na lifestyle yao mkuu, hakuna kiongozi atakuja awe anagawa pesa kwa watu ili kuwakwamua kiuchumi. Kama mnategemea hicho sahauni, hata mitume wakishuka hawataweza kuwaridhisha.
Mara nyingine watu kama nyie ndio mnapalilia umaskini hapa nchini kwa kuamini na kuhubiri kuwa umaskini unasababishwa na serikali. Tumieni raslimali na nguvu zenu kujikwamua, msingoje serikali iwawekee mabomba ya maziwa na asali.
Mkuu, nadhani kuna kitu unakikosa. Jukumu KUU la serikali yeyote ni kuweka Mazingira sahihi kwa watu wake wawe na maisha bora. Mazingira bora ya elimu, afya, KILIMO, biashara, MIFUGO n.k.
Sikiliza ninasema Mazingira bora maana yake nini. Rais hakutakiwa kununua bombardier leo. Alitakiwa awaangalie jeshi kubwa la vijana wanaotoka mashuleni kuingia soko la ajira (ambalo halipo) Mfano; pesa ile angejenga mifumo ya umwagiliaji.
Angalia pesa ya bombardier zote hizo zingejenga mtandao wa umwagiliaji ekari ngapi ? Kwa miaka mitano mtandao huo wa umwagiliaji ungeajili watu wangapi? Nchi ingekusanya kodi kiasi gani. Tungepunguza vibaka wangapi ? Hilo ndilo jukumu la serikali. Ni ujinga kuamini mhitimu atarudi kijijini kushika jembe LA mkono.
Wenzetu Singapore, Malaysia. Korea Kusini, serikali waliweka Mazingira mazuri ya fursa, waliwawezesha wananchi. Isitoshe watu wawe huru katika nchi yao, pasiwe na udikteta, mtu mmoja asiwe ndiyo sheria. Samahani nikutoe kidogo.
Uliona kilichotokea Tanga siku za nyuma kidogo. Mama aliyeingia na bango akitaka Rais amwone ili kudai mirathi yake. Siku ya sheria nadhani. Rais alitoa agizo kwa Jaji Kiongozi hadharani, eti Jaji chukua simu ya mama huyo shughulikia shida yake. Ooh my God. Rais anamwamulisha Jaji Kiongozi !!!!? Rais anaingilia Mahakama !!
Acha ile mpya ya awali; Mahakama wamalize kesi haraka na kuwafunga mafisadi ili awape pesa wanayodai !!!? OK katika hali kama hii, Kiongozi Dragoon utapata nchi na wananchi wenye maisha bora. Kwa kusema hayo siwatetei wala rushwa, wakwepa kodi, wala wapiga dili maofisini.
Hao wapo na wataendelea kuwepo maana hata Marekani, Japan bado wapo. Tujitajidi walau tuwe kama Kenya.
Sent using
Jamii Forums mobile app