Watu wamevunjiwa nyumba kwa "amri kutoka juu" licha ya kuwa na amri za mahakama kuzuia uvunjaji huu!
Nyerere alisema kwamba, mkiruhusu kuongozwa na dikteta, mtaumia. Na yeye hata hatawahurumia, kwa sababu mtakuwa mmejitakia hilo.
Alisema ukigusa moto,utaungua, hii ni kanuni ya asili, si kanuni ya Nyerere.
Alisemahivyo, video zipo Youtube. Search "Nyerere katiba1" "Nyerere katiba2" na "Nyerere katiba3".
Alikuwa anaongelea viongozi wa nchi kuongoza kwa kuvunja katiba, alilaani sana hili Salmin Amour alipoiingiza Zanzibar OIC.
Yale maneno yake yana umuhimu sana kwa kipindi hiki cha Magufuli. Kwa sababu tunaona ujinga ule ule wa nchi kuendeshwa kwa kauli za mtu badala ya sheria na katiba.
Kwa hiyo na mimi narudia mule mule.
Shurutisheni viongozi waongoze kwa sheria na katiba, si kwa ubabe wao binafsi.
Mkishindwa hili, mkishangilia viongozi wanaovunja katiba, mkiishi kama mashetani ni stahili yenu.
Kwa sababu mmeshindwa kusimamia haki zenu za msingi za kikatiba.
Mmeamua kugusa moto, mkiungua msilalamike.