Ukitaka kujua kuwa serikali imefilisika nenda halmashauri yoyote utajua kuwa tunaelekea kwenye kaburi, ofisi zimeishiwa pini, karatasi, Stepla, hakuna mafuta, magari yamekufa, miradi hakuna, pia wafanyabiashara wanalia bidhaa hazitembei purchasing power imepungua, ajira hakuna, serikali imepunguza wafanyakazi, makampuni nayo yameprun, zaman serikali ilikuwa inaajiri watu wengi sana na sekta muhimu kama udaktar lazima waajiriwe siku hizi MDs wapo home, serikali inatoa ajira ya watu 50 matangazo meeeengi utafikir imeajiri graduates wote, watumishi wanalia hakuna nyongeza wala marupurupu, mkuu anawivu kwa watu waliifanikiwa Mara bomoabomoa isiyo na kichwa wala miguu, fikiria hela ilivyo ngumu afu Nyumba yenu tegemewa inabomolewa, nimalize kwa kusema Benito Mussolini pia alisifiwa saana baadae waliokuwa wanamsifu ndio walimtwanga risasi ili apishe njia hata hapa tz wapo wanaomsifu jamaa lakini naamini wao ndiyo watakao kuwa na hasira kuliko hata wale tunaoona mwelekeo si mwema