Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Katika sakata la makinikia ndipo nilipooona sura halisi ya magufuli, pamoja na kujinasibu pia kuwa mpambabaji na rushwa, huku akiikubali rushwa waziwazi, kwa Maneno hata matendo yake, nilimtazama kule Arusha wakati wa kutunuku kamisheni kwa jeshi letu, jinsi alivyo kasirika pale wale madiwani wa rushwa waliposhindwa kujitokeza wote.

Magufuli ni mwongo Sana na ameshatengeneza mfumo wa kupika data ili tu kuudanganya uma, makinikia, mishahara, ya wafanyakazi, vyeti feki, umoja wa kitaifa na baraza la mawaziri.

Kwenye makinikia alidanganya kwa kutumia tume yake iliyotengeneza sample mpaka ikazidi asilimia 100 kwenye uchanganuzi;

Mwezi wa tano may mosi alisema ataongeza mshahara kwa watumishi na kupandisha madaraja kwa mujibu wa sheria za utumishi lakini hakufanya hivyo na amekuja baada ya miezi mitatu kukanusha kuwa hayuko tayari kupandisha mishahara yaani anavunja sheria peupe, kutokujali wafanyakazi wengine wanaeza kuona ni sawa tu ila litaaribu utendaji kazi katika taifa na morali ya utendaji kazi itaondoka hivyo kuongeza mdororo wa uchumi.


Katika suala la vyeti feki ni mojawapo ya sehemu ambayo kafeli kwa asilimia mia moja kwa sababu ya kuweka upendeleo (double standards) kuwafukuza wengine kazi pasipo kuangalia utendaji wao ulivyo mzuri na kubakisha wengine kwa kuwa tu ana uswahiba nao. Maneno yake kwenye mkutano wa ALAT ni uthibitisho.

Kufeli kutengeneza umoja wa kitaifa ili kuweka mkazo katika maendeleo, magufuli amekuwa so muongo tu bali mwiba kwa ustahimilivu na umoja wa kitaifa. Amekuwa akisema Maneno waziwazi yasistahili kusemwa na mtu aitwae raisi wa taifa. Kuonyesha chuki hadharani kwa wanaokosoa matendo na Maneno yake ambayo kiuhalisi yana shida na matokeo mabovu tangu kuingia kwake madarakani, mfano ni mfumuko wa bei za vyakula na bidhaa sukuri ni mfano halisi alipoingia madarakani sukari ilikuwa shs 1500-1600 lakini kwa kutaka sifa za kijinga kama ulivyo kawaida yake ya kupenda kusifiwa tu akasababisha sukari kupanda haya kukosekana sehemu nyingine na kuwa kitu cha anasa, sukari ikapanda mpaka. 2500-6000 sehemu zingine halafu anasema ameishusha bei ya sukari baada ya kuingia madarakani. UONGO MTUPU NA ULAGHAI.

MAUAJI ya watu, na kutekwa kwa wakosoaji wake na serikali yake. Kupotea kwa Ben Rabiu Sanaane huyu alikuwa anamkosoa wazi wazi kuuhusu elimu yake, aliyoipata kimagumashi magumashi, kwenye uzamivu wake.

Miili ya watu kuokotwa huku na huko mateso ya kimya kimya watu wanayo pewa na watu wanaosadikiwa kuwa ni polisi na kitengo cha usalama, kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa taiga letu.

Magufuli hajali zaidi ni Furaha yake kuona watu wanateseka katika mikono ya watu wake yeye ni aliowatuma.

Hivyo tutafika mahali watu watajimilikisha silaha kiuhalali theni tutakuwa tumefika pagumu,

Ni jukumu lako wewe na Mimi kumpongeza pale anapofanya vema na kumkosoa pale anapoenda Kombo, Kama mikopo ya FIBA kubwa tuliyopokea ya shs 500bilions tutalipa sisi kwa kodi zetu.

Yeye na watoto wake na wake zake atakuwa anakula pensheni kwa heshema.

Pia Magufuli haamini walinzi wa kitanzania amezungukwa na walinzi wa kuliangamiza taiga letu kutoka Rwanda kwa Paul kagame

Tanzania tuliokoe taifa letu kwa kusimama imara
 


Mleta maada naomba uhakika/ushahidi wa hilo, nijuzeni jamani maana roho imeniuma ghafra.
 
Uongo gani sasa, kwani sukari haikuwa 5,000/- alipoingia madarakani!?
 
Kuyasema hayo utaambiwa mchochezi,unatumwa na wazungu!!!

No wonder Kikwete hataki hata kujumuika nae,kkwenye bei ya sukari kuwa aliikuta shs 5000 ni unafiki mkubwa sana na matusi kwa mkwere!!

Huwa najiuliza tu mwandishi wa hotuba za raisi Ikulu ana kazi gani????

Kuna watu walianzisha kampeni ya Trump apimwe akili,hhuenda walikuwa wana maanisha TrumpRaper wetu!!!
 
Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni John Pombe Joseph Magufuli,na itakuwa hivyo mpaka 2025,jifunzeni kuelewa hilo na kupambana na hali zenu.Hizi nyingine humu JF ni porojo tu.Hii bidii yenu kwenye mitandao itumieni kujiongezea kipato.FULL STOP.
 
Uongo gani sasa, kwani sukari haikuwa 5,000/- alipoingia madarakani!?
Tunakuuliza na kumuuliza na yeye ilikuwa shingngapi? (kabla ya kujibu ukumbuke kuwa tulijuwa tunanunua kwa hela yetu na bei twaikumbuka)
 
Hiyo ya walinzi wake kutoka Rwanda imesemwa sana lakini serikali haijawahi kukanusha. Lakini kama ni kweli basi itakuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu wa ofisi ya Rais Na JWTZ na Taifa kwa ujumla. Hii ni kama uhaini!!! Haiwezekani!!!! Itabidi ichunguzwe kama itathibitika hatua kali zichukuliwe kwa aliyefanya maamuzi haya.
 
Sidhani Kama ni kweli kwa Rais wetu kulindwa na askari toka Rwanda, kwa hili serikali inatakiwa ilitolee ufafanuzi kwani suala limekuwa likizungumzwa Mara kwa Mara na kukaa kimya kwa serikali juu ya hili ni udhaifu mkubwa, kwanza ni sawasawa na kuliweka rehani taifa hili kama itathibitika ni kweli, msemaji wa serikali Dr. Abbas upo wapi juu ya hili, mbona mambo mengine unayafafanua kwa haraka Sana, kwa hili vipi?
 
[emoji125]
 
Mleta maada naomba uhakika/ushahidi wa hilo, nijuzeni jamani maana roho imeniuma ghafra.
Pita ikulu ya magogoni pale ukuta uloizunguruka ferry utawakuta askari wanaolinda ikulu yooote pembezoni mwa barabara jifanye unakwepa gari ili uwe karibu nao halafu wasalimie "habari zenu"wakiweza kujibu salama mi naleft JF....wale ni wanyarwanda pure...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…