Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Uongo gani sasa, kwani sukari haikuwa 5,000/- alipoingia madarakani!?
Yeye ndiye alisababisha ipande baada ya kawazuia kina bharesa kuagiza mbona wote tulikuwepo unafikiri ni zamani sana hadi tumesahau.
 
Kumbee? Duu tumekwisha
 
Ni urais UPI wenye tija kwa tafa lolote duniani,(a)urais kama taasisi iliyo active (b)urais kama taasisi isiyo active?
 
hapo umenena kaka
wanafikiri propaganda hizi humu JF zitazaa matunda mapema . nooo!!!!
it works of course but it will take ages before it bears fruit.
 
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutafakati pia kupanga kesho zetu. Ila kuna kundi moja linashangaza sana! Wao wana slogan inasema hivi:

“Life goes on...” yaani “Maisha Yanaendelea..” mathalani mambo yote yanayo wazunguka yanaenda mlama!

Uchumi udolole, demokrasia ibanwe hata mauaji yatokee wao wanaona sawa tu! Eti “..MAISHA YANAENDELEA”
 
Mkuu kwani hatma si hupangwa na Mungu,tutaishi halafu tutakufa ndiyo hatma yetu.
 
Kila mmoja ana mustakabali wake. Usikubali kuamini kuwa maisha tunayopitia ndio yanaamua mwisho wako.
 
Hatima yetu ni kuupa likizo ubongo na tusijuwe cha kufanya hadi remote control itakapoongoza.
 
kwamba uongozi wa nchi umekushinda? Kwanini kupambana na ufisadi kuwaathiri Watanzania walio wengi ambao si mafisadi?

Kama ufisadi mbona nawe unaufanya!? Hujasema lolote kuhusu rushwa ya milioni 10 kwa kila mbunge wa MACCM iliyotolewa October 25, 2016 pale lumumba?

Mbona unaendeleza ubadhirifu kwa kuchota trillions kutoka hazina bila idhini ya Bunge?

Kujenga chato Airport ni ubadhirifu mwingine unaofanya. Hivyo achana na uongo wako sema kweli tu uongozi wako wa nchi umeshindwa na utaendelea kushindwa kutokana na sera MUFILISI, kukurupuka na kuendesha nchi kama vile una hati miliki.

"Licha ya ukweli kutokana na hatua tunazozichukua za kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma, wapo wananchi wa kawaida ambao si wezi wala mafisadi wanaoathirika, hili ninalifahamu, lakini kama kweli tunataka kupambana na wizi na ubadhirifu pamoja na kuleta maendeleo kwa nchi yetu, athari hizi hatuwezi kuzikwepa, mabadiliko ya aina yoyote ile lazima yana athari kama hizi, lakini jambo la kututia moyo ni kwamba athari hizi mara nyingi ni za kipinzdi kifupi", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba..."Mabadiliko ni magumu mwanzoni, yatakuwa machungu yanapofikia katikati, lakini mwishoni matokeo yake ni mazuri au ni matamu, hivyo nawaomba wananchi na watanzania tuvumile katika kipindi hichi cha mpito, baada ya muda mfupi mambo yatakuwa mazuri, lakini hata kama hayatakuwa mazuri hivi karibuni, watoto na wajukuu zetu watanufaika, na huo ndio uzalendo".
 
Atasemaje ukweli wakati anaingia madarakani sukari ilikuwa Tsh 5,000/=
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…