Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kabla hujauliza yote hayo uliza kuhusu usalama na ubora wa hiyo miradi maana ule udsm tayari nyufa zishaanza kutokea!
 
When suffering knocks at your door and you say there is no seat for him, he tells you not to worry because he has brought his own stool
 
Huyo jamaa i nawezekana huwa anashauri wakandarasi wachanganye na hàmira //yeast kwenye sementi ukizindua Leo kesho unaflyover
 
Mkuu wewe ndio mkuu wetu ila kiukweli napata shida ninapo sikia miradi yamatirion na miradi ambayo duniani inafanyika kwa miaka na miaka sasa wewe unaimaliza kwa miaka kumi...
Ujenzi wa jiji la dodoma.
Ujenz wa dam kubwa afrika mashariki na kati nk...
Hivi kweli hii utaaliza for ten years only...
Nisaidie mkuu maana naona kama ndoto.
Utatekwaa
 
Katika nchi hii bado kero na changamoto muhimu zenye impact kubwa katika uchumi hazijafanyiwa kazi kwa kiwango chenye kutafsiri objective kuu ya serikali hii ya awamu ya tano. Sisemi kwamba serikali hii haijafanya mambo ya maana la hasha bali inasikitisha kuona kwamba serikali imeshindwa kuwa makini katika utekelezaji wa mikakati yake ya kuelekea Tanzania ya viwanda.

Naomba Leo hii niseme ukweli, niseme ukweli usio na chembe ya woga juu ya mtu yeyote bali ukweli ulio na lengo la kuniweka huru. " The truth will set me free "

UMEME WA UHAKIKA. Ninapoandika haya Mimi nipo gizani, si kwamba naishi nyumba isiyo na umeme hapana, nyumba ina umeme , unit za luku zimejaa but unfortunately nipo gizani ,, UMEME hamna! kwa nchi ambayo inaenda kujenga uchumi wa viwanda haya hayapaswi kutamalaki, inasikitisha kuona kwamba juhudi za kujenga nchi ya viwanda hazijaanza na uwepo wa umeme wa uhakika, viwanda gani bila umeme wa uhakika? uchumi gani wa kati pasipo umeme wa uhakika? . Serikali ya awamu ya tano imechukua hatua gani za kusisimua katika kutatua kero hii ya umeme ambayo bila kimung'unya maneno ndio kero iliyopaswa kuwa kipaumbele?

Nasema hivi kwa sababu ukiweka kwenye mizania utaona kwamba uwepo wa umeme wa uhakika ni faida kubwa sana kwa nchi kuliko kuwepo kwa treni za umeme, fly overs na Uwanja wa ndege wa Chato lakini je serikali hii imewekeza nguvu zaidi katika umeme? jibu ni hapana na linakuja swali jingine tatizo hasa si lipo wazi? kwamba Rais amekuwa akifanya maamuzi katika karibia kila matumizi ya pesa za umma, kwamba hii hela ifanye hiki na ile ifanyi kile jambo lililopelekea serikali yake kutoonesha dhamira ya dhati kufikia kile inachokihubiri (Tanzania ya Viwanda)

Lakini pia kuna suala la "MFUMO WA ELIMU" Miaka nenda miaka rudi nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na changamoto katika kuzalisha wasomi wenye fikra na uwezo wa kujiajiri. Ipo wazi duniani kote kwamba tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kujongea. katika muktadha huo huo nionyeshe juhudi za serikali katika kufanikisha kuondolewa kwa mfumo huu wa kuzalisha wasomi "feki" ambao hawana uwezo wa kufikiri nje ya box badala yake kuendelea kuwaza ajira za kuajiriwa.

Juhudi za serikali kutoa elimu bure na kuhakikisha upatikanaji wa madawati ni juhudi za kuungwa mkono lakini ni juhudi zenye impact ndogo sana katika kukabiliana na changamoto niliyoieleza. Serikali ilipaswa kuweka kipaumbele katika kubadili mfumo wa utoaji elimu nchini ili ikiwezekana idadi ya vijana wanaopata mafunzo ya ufundi kama uvuvi wa kitaalamu, ukulima, ufundi seremala, uashi , Uinjinia wa maana na si huu feki ambao Injinia wa electronics hawez tengeneza hata Earrphone , hawez hata kucopy tecnolojia yoyote , injinia wa Electricity hawez kutengeneza hata taa tu. Niwaulize watanzania wenzangu elimu hii inayozalisha wazungumzaji hodari badala ya watendaji hodari itaifikisha nchi hii katika ndoto ya kuwa ya Viwanda?

Lastly niwaulize wale ndugu zangu wanaotoka hadharani na kusema wanamuunga mkono Rais je wanafikiri sawa sawa kweli? haikatazwi kumuunga mkono Rais lakini si kwa upofu huu jamani,, imetokea hivi karibuni mbunge kaiingiza nchi kwenye ghrama ya kurudia uchaguzi katika jimbo lake gharama ambayo ni zaidi ya billion 5-10 , gharama ambayo ingetosha kujenga vyuo hadi vitano vya ufundi..

Inauma na inakera kuona katika karne hii bado watanzania tunaendeza vyama badala ya taifa , inashangaza kuona hadi wasomi kuamua kutumikia matumbo yao badala ya jamii ambayo inawategemea.
 
Ngoja tuwatume watumwa wetu masikini(Polisi) wanaotulinda waje wakuteke na kukuua kabisa maana hufai wewe.
 
Huu ndiyo mmoja wa uzi bora kwangu 2017
Kamanda...[HASHTAG]#Mpk[/HASHTAG] upoooo

Ova
 
ninacho jua mimi magufuli hana haraka yeye mmemuwekea miaka 10'ya utawala kikatiba lakini yeye anayo 20 . na ni rahisi tuu atamaliza 5 ya kwanza mtamchagua ya pili, hili halina shaka, mkimchagua kipindi cha pili, basi , wapinzani anaowakanyaga kichwani leo atawapa katiba mpya kwa mgongo wao, kwa hiyo katiba itabadilishwa , na hapo yeye ataanza vipindi vyake vya miaka mitano mitano kwa katiba mpya. kwa hiyo mtazamo wa miaka kumi wetu ni hasi, mtazamo chanya ni miaka 20 na he means it come what may, kama hutaki kuona vipindi hivi pamabana naye, i tell you the truth mungu wa tundu lissu hutakuwa naye
 
wakuu.
kwa kuanza kabisa mheshimiwa Raisi ukweli huu upokee na uufanyie kazi, hali ya maisha kipindi chako ni ngumu mno na mzunguko katika biashara umedorora , waaagize hata wasaidizi wako masokoni wakaulize hali ikoje halafu watakueleza na wasikufiche kitu.
ukweli ni kwamba hali ni mbaya jaribuni kurekebisha na kuna maeneo unafanya vizuri na kuna maeneo unafanya vibaya.
 
Mimi nilidhani ni kama utani hivi bungeni kufungiwa kua live, baadae hakuna kufanya mikutano nje ya eneo alilochaguliwa mtu, tukasikia wanahabari wanalalamika kunyimwa uhuru wa kuongea na kuandika, magazeti yakafungiwa na sasa hata watu kusema "vyuma vimekaza" hakuna, ukisikika unatiwa ndani.

Sasa tunaelekea wapi? tunataka tuishije?ni vipi hayo yote niliyoyataja hapo juu yanaweza kukwamisha maedeleo ya taifa? Bila kupeana changamoto za kimitizamo taifa litakwendaje mbele?

Wapinzani mmeshindwa namna ya kudhibiti haya pengine kwa sababu mnaogopa, mnaongelea kwenye mitandao ya kijamii tuu lakini physical implementations hazionekani why? Kwa aina ya utawala tulionao hivi sasa wala hata siwezi kubisha kua upinzani unaweza kufa, hii ni kwa sababu wapinzani nao bila ya hayo mambo niliyoyataja hapo juu uhao wao haupo tena na wao wamelikubali hilo.

Nina imani kukiwa na upinzani wenye sauti moja nchi nzima hakuna atakayewazuia kufanya mambo yaliyo ndani ya katiba.
 
wakuu.
kwa kuanza kabisa mheshimiwa Raisi ukweli huu upokee na uufanyie kazi, hali ya maisha kipindi chako ni ngumu mno na mzunguko katika biashara umedorora , waaagize hata wasaidizi wako masokoni wakaulize hali ikoje halafu watakueleza na wasikufiche kitu.
ukweli ni kwamba hali ni mbaya jaribuni kurekebisha na kuna maeneo unafanya vizuri na kuna maeneo unafanya vibaya.
Inawezekana kweli kuna maeneo anafanya vizuri na maeneo mengine anafanya vema ila driving force ya nchi ni uchumi kama kwenye uchumi anaboronga kama inavyooneka sasa basi kiujumla tunasema hafanyi vizuri kwenye uongozi wake.

Leo US anaheshimika kwasabbu ya uchumi imara na si vinginevyo. Uchumi imara ndiyo misingi ya vitu vyote. Ukiwa na uchumi mbaya lazima utakuwa na siasa mbaya na hata amani itapotea tu.

Cha msingi bwama mkubwa inabidi afanye jitihada za madhubuti za kuweza kuweka haya mambo sawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom