Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Alipoingia tu madarakani alisema atahakikisha watanzania mnaishi kama mashetani, kwahiyo mkuu vumilieni maumivu hadi atakapoondoka zake
 
Kila unachojaribu kufanya, kikitaka kuleta mafanikio kidogo SERIKALI inakupiga "MTAMA"


Si kweli, umefanya nini serikali imekukataza? Kama ulikuwa umezoea kuuza unga na kuzurura mjii lazima utaona maisha magumu kwako. Ni shida yako, mbona wengine tunaishi kwa raha?
 
Kwan safari imeisha au unataka ushukie njiani tusubiri tuendelee na safari maana cc n abiria tu
 
Nyerere aliwahi kusema tunamwapisha Rais ili ailinde Katiba na kuitetea kufa au kupona pale anapoona inachezewa
Lakini hivi sasa tuna Rais mvunja Katiba live bila chenga huku Bunge likimuona yuko sawa kisa ni mwana ccm mwenzao

Hivi sasa tuna Katiba haiko juu tena bali Rais ndio yuko juu ya kila kitu

Neno Katiba ndio muongozo Mkuu halipo tena hivi sasa
Bali tuna Rais ambaye ndiye Katiba yenyewe

Ningependa magufuli aiheshimu Katiba na sio kuwa juu ya katiba

Mambo mazuri mengi anayofanya yanaminywa na ukiukwaji wake wa Katiba
Nimkumbushe tu walikwepo wababe wa sheria za kichwani lakini leo hawapo na mwisho wao uliishia pabaya
 
Ungetaja vipengele vya katiba ambavyo vimevunjwa na Mh. Rais basi mada yako hii ingeonekana ya maana na yenye maslahi kwa taifa.
 
Hata hayo yanayoonekana mazuri nayo yanatia shaka maana baadhi yanafanyika huku kukiwa na tuhuma kuwa yanafanywa bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma na bila kupata kibali cha Bunge.
 
Nyerere aliwahi kusema tunamwapisha Rais ili ailinde Katiba na kuitetea kufa au kupona pale anapoona inachezewa
Lakini hivi sasa tuna Rais mvunja Katiba live bila chenga huku Bunge likimuona yuko sawa kisa ni mwana ccm mwenzao

Hivi sasa tuna Katiba haiko juu tena bali Rais ndio yuko juu ya kila kitu

Neno Katiba ndio muongozo Mkuu halipo tena hivi sasa
Bali tuna Rais ambaye ndiye Katiba yenyewe

Ningependa magufuli aiheshimu Katiba na sio kuwa juu ya katiba

Mambo mazuri mengi anayofanya yanaminywa na ukiukwaji wake wa Katiba
Nimkumbushe tu walikwepo wababe wa sheria za kichwani lakini leo hawapo na mwisho wao uliishia pabaya
Nanukuu...Mambo mazuri mengi anayofanya...bhasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Kama haya ni ya kweli ambayo wanafanyiwa kabila hili basi nchi yetu tayari imegeuka. Ingawa tunaweza kusema ni ya kweli au siyo ya kweli, vipo vihashiria vinavyosema ni ya kweli.

Wapo watu fulani wakubwa tu wenye makampuni yao ambao walikuwa wamekaa kama kamati fulani kujadili namna ya kukabiliana na kile walichokiita changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara. Watu hawa ni wa kabila moja maarufu sana Tanzania linalotoka kanda ya kaskazini. Kiukweli ni maneno ambayo nimeyasikia wakiyaongea tena wanayapa mkazo kwelikweli na mbinu ili kujikwamua.

Jamaa mmoja akasema yeye ni mtu anayeomba tenda mbalimbali za kusambaza vifaa kwenye taasisi za serikali ila amekuwa akipata changamoto ya kunyimwa tenda lakini akakiri wazi kuwa kabla ya utawala wa awamu ya tano mambo hayakuwa hivi! Huyo akadiriki kusema kuwa aliamua kuanza mchakato wa kubadili jina lake la ukoo kwenye documents anazoombea tenda ili tu asikatwe kwa kigezo hicho. Anakiri wazi kuwa walau hilo limeanza kumpa uhai. Naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyosema "Siwezi kutumia tena jina la TARIMO kwenye kuomba zabuni. Limekuwa likiwa kikwazo kwangu! Hata wanangu wote nimewaambia wabadili jina lao la ukoo kwenye mambo yao ya shule! Wasitumie kabisaa jina hilo" Mzee huyo kweli akawa anasisitiza hivyo.

Katika maongezi yao kumbe kuna mama mmoja mfanya biashara ambaye alishauriwa asiweke jina lake la asili kwenye makabrasha yake ya kuomba tenda ya mabilioni ya fedha kwenye moja ya mashirika ya serikali. Nadhani aliyemshauri ni mmoja kati ya wazee waliokuwa wakijadiliana katika mjadala huu. Mara lile jina lake likaanza kujadiliwa. Nadhani hili jina linaweza kuwa linatokea Maeneo ya Wilaya ya Moshi. Lakini katika mjadala wao wakagundua kuwa jina hili halifahamiki sana kama jina la kikabila. Mara nikaona mzee mmoja akinyanyua simu na kumpigia yule mama na katika maongezi yake akamuambia "Kwenye documents usiweke jina la ukoo la mume wako! Hilo linajulikana, tumia jina la upande wa baba yako ambalo linaonekana siyo maarufu kulitambua" Kwakweli nimeacha mjadala ukiwa hot sana na inaonekana hili kabila limeanza kukutana na adha kubwakubwa za hapa na pale katika miangaiko yao ya kutafuta riziki.

Pamoja na hayo nalisifu kwa kung'amua hilo na kuanza kutafuta mbinu za kukabiliana na hili jambo.

Hayo ndiyo niliyokutana nayo kijiweni moja ya maficho maalum ya wazee maalum ambapo nilibahatika kuingia hapo baada ya kuwa nimempeleka boss fulani kumkutanisha na mtu ila huu mjadala umechukua muda mrefu nawanajadili kwa umakini na wanaweka uthibitisho! Wengine wanasema kuwa wanapigiwa simu kutoka huko juu na watu wanaowapenda na wamekuwa wakiwapa huo ushauri wa kuondoa kabisa majina ya koo zao au kuyaandika kwa herufi moja tu pale wanapotaka kuomba zabuni mbalimbali.

Hapa ni kazi kwa kazi.Tafuta mbinu ya kupata kazi!
 
Hayo ni cha mtoto. Zile asilimia 10% za halmashauri kwa kina mama na vijana huku kwetu, imebidi watendaji wa kata waitwe na wajieleze baada ya kubainika kuwa walionufaika na hela hiyo ni pamoja na wanachama wa upinzani. Hivyo ndivyo vi-wonder
 
Unafiki mtupu, siku ya kufa kwako utabaki mdomo wazi, huko hatujafika hata kidogo na hatutafika, tender hutangzwa na hutolewa kwa yule aliekidhi vigezo na si vinginevyo.

Kama huko nyuma taratibu zilikiukwa na upendeleo ulitawala kwa wasio na vigezo kupewa tender, zama hizo zimepita, hanyimwi mtu tender kwa kabila lake, acha kupanda chuki, hailisaidii taifa, sanasana ni kuliangamiza
 
MTOA POST UNAMAANISHA KUWA TENDA WANAPEWA WATU WA KANDA YA ZIWA HASA WASUKUMA???!!!KAMA NI KWELI HII HALI SIO YA KUFUMBIA MACHO
Mkuu huu mjadala nimekutana nao na wanatoa shuhuda mbalimbali. Yupo mmoja amesema kuwa aliomba mkopo ila alitakiwa kuthibitishwa na hazina ili benki imkopeshe. Jamaa kasema alinyimwa mkopo kutokana tu na kabila lake. Hii ni baada ya msajili wa hazina kumkataa. Tena ni huyu msajili wa sasa.Alipopeleleza akaambiwa kuwa kabila lake limemponza. Wanajiapiza kwa majina yao ya asili wanayaacha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom