Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tulikwenda porini pamoja, tulikwenda shinyanga pamoja, tukaenda bagamoyo pamoja lakini tulienda mpaka Tanga pamoja leo hii Jiwe umenitenda.

Unamaanisha nini mkuu na hii route.......?

Maana ni vigumu kutenganisha hiyo miji na ushirikina......!
 
tuunge pia wizi wa 1.5 Trillion. Tumuunge mwizi wa aina yake???
 
Mbona haya makonda hayaongei kwenye hotuba yake leo au serikali hii ajira imezipiga kapuni. Hata jk angetaka kununua ndege angeweza au kujenga stiglers angeweza ila alikuwa na huruma ya watu wapate maisha bora. Na maisha bora ni ajira inaongera consumption rate. Sasa hivi ajjira zoto ni za uongo na za majukwaani. Huyuhuyu makonda alitangaza ajira za kuhesabu magari watu wakapeleka aplications kibao pale tanroads lakini mpaka leo mwaka sasa hamna kinachoendelea. Ajira zilitangazwa za bomba la mafuta kutoka uganda mpaka tanga mwaka saaa hamna kinachoendelea nahisi hata aplication wameshachoma. Kila kitu ni uongo tu mwanzo mwisho na kufanya kazi kwa kujionesha kwenye vyombo vya habari. Mbona jk amefanya mengi hatukuona kila siku kelele kwenye maredio na akijisifu amejenga daraja la kigamboni, anaajiri kila mwaka na mengine mengi. Kweli huu utawala ni wa kishamba
 


Sawa, hongera sana kwa kutambua mchango mkubwa wa CCM, usijali JK atahusika kwenye kuchagua mrithi wa Raisi Magufuli ambaye pia atakuwa CCM hivyo huenda ukampata JK mwingine na hali kurudia kama ilivyokuwa hapo awali kama ulivyoieleza chini ya CCM ya JK mambo yalikuwa bora kabisa kwa mujibu wa maneno yako, hivyo CCM itaendelea kwa maana inatoa viongozi bora kama JK!
 
Jamani asilimia kubwa ya watanzania tunaishi hapahapa kwa baba Jesca hali ya kiuchumi,,kisiasa kijamii tunaiona ilivyo... Kinachonishangazaa na kuniacha mdomo wazi Ni ,,,baadhii wanaona mambo yapo 100% sawaaa kabisa ( we are on the right track) na wengine wanaona tunapotea tuendako siko( Mimi Ni mmoja wao)... .Ni kweli hatuwezi kuwaza kwa namna moja lakini kwa asilimia kubwa matatizo yetu na changamoto zinazotukabili zinafanana!.... Hakuna maji safi 50+ ya Uhuru ,,Elimu bado duni, ,, mfumuko wa bei kila uchwao,, siasa chafuu,,, nyinyi mnaosema we are on the right truck mpo nchii hii kweli?../.
 
na wengine wanaona tunapotea tuendako siko( Mimi Ni mmoja wao)...
Ukiona dereva kakosea njia na abiria wako safi tu huenda wewe ndio umekosea badala ya la Turiani umekwea la Mwanza shuka next stop.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…