Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa Rais,

Pole kwa Majukumu!.....natumai ujumbe wangu huu utakufikia hapo "Jumba Jeupe" japo unaweza kuonekana ni ujumbe usio na maana na wa hovyo but kikubwa ufike sehemu husika.

Mh. RAIS, Nimejaribu kutafakari mambo mengi yahusuyo hatma ya taifa letu tangu ulipoingia madarakani, naona umeshapoteza dira na lengo lako uliloingia nalo madarakani.....

Mh. Rais, bila kupepesa macho wala mikono nathubutu kusema ya kwamba wewe ndiye Rais unayeweka historia ya "Rais kimeo kuwahi kutokea tangu tupate Uhuru" huna dira, huna lengo thabiti, huna maono, huna Utu, nakiri kuwa cheo cha urais kimepata m'bakaji (Nisamehe kwa lugha yangu kali).

Mh. Rais, wewe ndiye Kiongozi pekee uliyeleta balaa, malalamiko, shida, manyanyaso na mgawanyiko mkubwa katika taifa (umekuwa adui mkubwa wa demokrasia na mshikamano kitaifa, umekuwa Nepotist na selfish wa kiwango cha hali ya juu, Ukanda, Ukabila na hata Uchama! Inasikitisha!

Mh. Rais, tangu uingie madarakani, ajira hamna (vijana waliomaliza vyuo kuanzia ulipoingia madarakani yaani 2015+ wanakula msoto mtaani).....Hali ngumu ya maisha, nani aliyesalimika katika hili? Wewe ndiye rais pekee ambaye chini ya uongozi wake, upinzani unaonekana ni uadui, manyanyaso ya polisi na vyombo vya usalama kwa raia hakika umeweka pamba masikioni!!

Mh. Rais, huu ni mwaka wa tatu tangu uingie madarakani (soon utaingia wa nne), ila najua unajidanganya kwa kujivuni Elimu Bure (ilhali hakuna implementation na strong strategies), lakini pia utajivunia MaBombardier, SRG, Stiglers Gorge na Uwanja wa ndege wa Chato!...ila nakuhakikishia utaondoka madarakani ukiwa na deni kubwa kutoka kwenye mioyo ya Watanzania wengi walioteseka na uongozi wako dharimu.

Nani anayetaka Stiglers Gorge na Mandege wakati hapewi nafasi yake kikatiba kama mwananchi mwenye imani, itikadi, na maono huru? Hakika mtu uyo hayupo, na kama yupo hawezi kuwa si punguani wa akili!!

Mh. Rais, nikukumbushe tu ya kwamba hao wakuhadaao kwa kisingizio cha kukuunga mkono, ndio haohao watakao pelekea anguko lako....

Nimalizie kwa kukupa ujumbe huu "THE NUMBER OF FOLLOWERS YOU HAVE, DOES NOT MAKE YOU A BETTER PERSON THAN ANYONE ELSE,..REMEMBER, ADOLF HITLER HAD MILLIONS, JESUS HAD ONLY TWELVE".......


__nakungoja mlangoni____
Hata waliokupa likes hawajitambui. Nonsense!
 
Rushwa zimekata, Wauza unga mmetiwa kapuni, siasa za majitaka na uongo majukwaan zimekoma, semina na warsha feki holaaaa, wazee wa 10% kibano, waliokuwa na pesa chafu sasa kama mashetani, bandarin mizigo ya bure piniiii, kodi haikwepeki ni mwendo wa UHALISI TUUU mnaobishana na zamma hizi lazima mpate taaaaabu sana.
Tin number zinapatikana haraka, kibali cha ujenzi kinatolewa kila wiki,viongozi wamekuwa karibu na wananchi kutatua kero zao e.g Mawaziri, umeme umesambazwa vijiji vingi, wakulima tumeruhusiwa kuuza mazao nje, n.k
 
kuongoza watu wasiojua wanataka nini ni kazi kubwa.Anayetaka demokrasia na uhuru aende china ambako hadi askofu wa kanisa anateuliwa na serikali.No democracy but there is development.JPM PIGA KAZI SHETANI NA WENZAKE WANAPATA TABU SANA,GOD IS WITH YOU FOREVER.
Itakua yupo na mungu Sio MUNGU. Mungu si dictotor wala halishi CHATU binadamu.
 
Kuna demu mkaaaaali.... anapita karibu yangu.... ngoja nimalize kumuangalia kwanza
 
Zero brain at his best...Mwache JPM apige kazi kama vipi hama nchi
Mkuu hayo Ni mawazo ya KICHWA chako tu . Ahame kwa amri yako?, ungekuwa na uwezo kiwango hicho ungesha hamisha NJAA iliyowajaa wana lumumba VICHWANI.
 
Zero brain at his best...Mwache JPM apige kazi kama vipi hama nchi
Kama umesoma vizuri bandiko la huyu GT automatically Kuna kifungu kinasema kuwa watu kama ninyi ni mapunguani. Hakika ume-qualify upunguani wa kiwango cha juu kabisa
 
maendeleo yapi unayo ongelea ya vitu ama watu.

yaani utoe mifano ambayo haiendani bado nikubali (huko lumumba ndo mmefunzwa ivo) huku nje tumefunzwa kuhoji.

hakuna maendeleo yoyote (ya watu) yaliyo onekama ila kwa maendeleo ya vitu visivyo na msada anajitahidi
hama nchi katafute maendeleo ya watu,hakuna nchi iliyoanza kujengwa kwa raha,lazima wakati wa kupanda mkulima apate shida ila wakati wa kuvuna atafurahi.tatizo hamjui mnataka nini
 
Itakua yupo na mungu Sio MUNGU. Mungu si dictotor wala halishi CHATU binadamu.
unamjua king David,unamjua Yoshua?kasome uone mambo waliyofanya halafu ujiulize walikuwa na Mungu au hamna.Inaonekana humjui Mungu vizuri
 
Na
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Na hawajui ni lini watumishi Wa umma wataongezewa mshahara na nyongeza ya kila mwaka kuwa regular.
 
Naomba mnieleze hivi yale makinikia yako wapi,je acacia bado wanasafirisha dhahabu au hawasafirishi je ile tume ya maprofesa wa madini mliyotumia gharama nyingi kuwagharamia tena kwa pesa za walala hoi km nyie CCM mnaifikiriaje,hlf mtuambie milion 50 za kila kijiji zitatoka lini,khs ile ndege mbovu iliyoko Mwanza tatizo nn sbb kama ilikuwa mpya imekuwaje iwe mbovu ghafla,mtuambie ununuzi wa madiwani na wabunge umetolewa uthibitisho na akina nassari mbn mmekaa kimya hamuoni mnazidi kumkufuru Mungu mnaposema eti nyie ni wasema kweli na ni wapenzi wa Mungu na huu unafiki utawafanya kila msemacho au mtendacho kisionekane,pia mnijbu hivi ni kwa nn serikali yenu imejiingiza ktk kila biashara hadi inafikia hatua makampuni binafsi yanapunguza watu ina maana nyie waliompa kura ni wafanyakazi wa serikali tu huu ubaguzi mnaufikiriaje,hivi mnatambua kuwa walipa kodi wazuri ni wale mnaowafanyia figisu figisu na msiowajali na hawa ni private sectors,Mniambie pia hivi ni kwa nn mnaonyesha chuki ,ubavu na uonevu kwa vyama pinzani inafikia hatua wanakuwa kama wageni au wakimbizi ktk nchi yao,hili nyie mnalionaje hivi hamuoni kuwa mnaowanea wana ndugu na jamaa zao na pia nyie mna ndugu zenu mtaani hivi wakiamua kulipiza visasi nyie mtapona maana mnalindwa vipi hao ndugu zenu na watoto wenu wanaosoma na watoto wa hao mnaowaonea?kwa nn mnawatumia polisi kuhujumu uchaguzi ni kwa nn msiwe huru tu ili muonee ni kwa jinsi gani wananchi wanawakubali,hizi teuzi za wanachama wa upinzani mnapowanunua na kuwapa vyeo inamaanisha nini,je huko upinzani kuna vichwa sana kuliko ndani ya CCM kama ndivyo kwa nn msiache hivi vyama vikue na viwatengenezee cream nzuri ila nyie mnaviua na mwisho naomba kujibiwa maisha bora yamekuwa kwa wana ccm tena waliojingiza ktk siasa na wanaokesha wanasifia mkuu na chama je hamuoni kuwa mnahatirisha umoja na kwa nini inafikia hatua chaguzi za maaskari polisi na magereza zinaingizwa ktk siasa hii ina maana askari wetu wote ni CCM,NISAIDIENI TU NIELEWE MIMI NA WANANCHI WENGINE WANOHITAJI KUJUA
 
Tulieni mfue viatu vya wanene hapo ufipa ili mikono yenu ya kinafiki iende kinywani.

Mambo ya kuhangaikia rasilimali za nchi hii yanahitaji uelewa mkubwa mno ambao Tanapa nzima hamna mwenye huo uelewa.
 
Tulieni mfue viatu vya wanene hapo ufipa ili mikono yenu ya kinafiki iende kinywani.

Mambo ya kuhangaikia rasilimali za nchi hii yanahitaji uelewa mkubwa mno ambao Tanapa nzima hamna mwenye huo uelewa.
Kama nchi nzima hakuna mwenye uelewa tunastahili kuitwa shithole country
 
Pole pole yupo busy na kuchota pesa za walala hoi

Na kuwenda kununu vichwa vilivyo zalishwa na chadema ili akavitumie katika chama lao

Maana katika chama lao hakuna watu wa maana ndio maana wanao hamia huko wanapewa nyadhifa mbali mbali
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom