A.alleikhum mabibi na mabwana,nisiwachoshe sana na utangulizi,kama title inavyojieleza
Nimekua nikisikia kauli za kukombolewa/kutetewa/kusaidiwa kwa mwananchi mnyonge toka mwishoni mwa mwaka 2015,nguvu inayotumika kumuanisha mnyonge anayetetewa/kusaidiwa na utawala ni kubwa kuliko uhalisia,yani hata mnyonge hajui kama anatetewa/kupatiwa unafuu wa maisha,huyu Mnyonge ni yupi?
Naona gharama za maisha zinapaa,bidhaa muhimu zikipanda bei,vifaa vya ujenzi havishikiki,wakulima wanalia na pembejeo na masoko ya mazao yao,gharama za matibabu na upatikanaji wa dawa muhimu,watumishi wanyonge mfano walimu,askari na kada zingine maisha yao sio siri,wengi wanasema wanamkumbuka Mkwere...haya na mengine mengi yananifikirisha kutaka kumfahamu huyu mnyonge...
Au kama yumo humu JF ajitokeze tumjue..