Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwa mzungusha mikono kama wewe huwezi jua muelekeo wa nchi...subiri 2020 uwazungushie tena mikono
Ndiyo maana akauliza wewe usiye mzungusha mikono na unayeelewa vision ya nchi yetu kwa sasa msaidie/mueleze naye aelewe.mbona vijana wa ccm mnakuwa wajinga kiasi hiki?
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo.
Hiyo nia nzuri unaipimaje? Kitu gani kafanya mpaka umuone anania nzuri? Kuongea tu? Ni kiingozi gani wa Tanzania umewahi kuongea mabaya dhidi ya Tz? Tunapokosea wadanganyika ni pale tunapoamini kuwa watu wale wale,wa chama kile kile,Sera zile zile na mfumo ile ule wa utawala kwamba unaweza kufanya kitu cha tofauti ati maji na,MTU,kabila na dini yake imebadirika.I can assure you.mtasubiri sana
 
Yeyote anayemponda jpm ameguswa kimaslahi kwa namna moja au nyingine,hawa ndo wale serikali walikuwa wanaiendesha kweny ndege leo u.s.a kesho u.k. so mimi sishangai
 
Yeyote anayemponda jpm ameguswa kimaslahi kwa namna moja au nyingine,hawa ndo wale serikali walikuwa wanaiendesha kweny ndege leo u.s.a kesho u.k. so mimi sishangai
Tatizo wanawatuma vilaza kuja kuchokoza mada ...mwisho wa siku tunawakong'oli kwa hoja na kashfa juu....!
 
NITARUDI BAADAE NADHANI UMESHAPATA UELEKEO SASA
 
I like ccm.Yaani Tanzania kama naona Vision lather inaendeshwa kwa ahadi? I like it?
Hatujui kwamba ataanza kuboresha kwanza umeme ndo afwate viwanda..

Au aanze viwanda kwanza ndo afwate umeme...
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] hii ndo Bongoland
 
Pamoja na mipasho na taarabu kama kawaida yenu Lumumba umejitahidi. Nina maswali kadhaa.
1. Unaweza kuacha uarifu uendelee kwa vile hujaajiri polisi wa kutosha?

2. Kwa sheria na mahakama zilizopo hatuwezi kuwajibisha wezi wa Escrow?

3. Una uhakika gani kwamba mkimaliza kujenga mhakama hamtatwambia sasa tunaenda kutunga sheria ya mafidadi? mkimaliza mtatwambia mnaandaa wataalam wa mashitaka!

4. Hivi mahakama ni majengo?

5. NSSF lengo lao namba moja ni nini? Wataliacha waende kuanzisha viwanda vya juice au bia?

5. Kodi inakusanywa kama tunavyoambiwa, mbona ambulance zimekosa mafuta na ofisi hazina hata karatasi? Halimashauri zimetumia mapato ya ndani hadi wamekopa posho za madiwani na sasa ni miezi mitatu madiwani hawajalipwa posho kwa miezi mitatu nchi nzima!
 
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....

HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!

Ukiangalia hapa jukwaani wewe ni mmoja wa waanzisha post nyingi ikiwemo na kuchangia post. Ila kwa sehemu kubwa ya michango yako unachangia kipuuzi, kishabiki na kejeli. Sioni shida kwani ndio demokrasia, tatizo langu ni kwamba wewe umewekwa na chama chako kukitetea hapa mitandaoni. Nilitaraji kwenye sehemu kama hizi ndio ungekuwa unamwaga nondo na kutolea ufafanuzi mambo mengi ikiwemo na upotoshaji wowote. Unaposhauri watu wakasome ilani na ahadi kuna tofauti gani na kile unachoponda kila mara kwamba EL aliwaambia wananchi wakasome ilani ya ukawa kwenye mitandao!!?

Ni kwanini unakimbilia kwenye kejeli na upuuzi, kirahisi ni kwamba mengi ya hayo yaliyoahidiwa yameahidiwa tu kwa mazoea kwani huwezi kuingia kwenye kampeni bila ahadi wala ilani. Nchi hii haijawahi kuwa na tatizo kwenye upande wa maandishi wala mipango, ila tatizo la nchi liko kwenye utekelezaji, hivyo hapa ndio ulipaswa kuchanganua kwamba tunafikaje huko kwani katika budget inayoendelea kusomwa haiakisi hilo. Sasa watu wanataka ufafanuzi isije ikawa ni kauli mbiu kama nyingine zilizowahi kutolewa na mpaka leo hata wale waliozitoa wanashangaa watu wameendeleaje kuwa wavumilivu kwa kile kilichotokea.
 
Nchi haina vision,kila MTU wanafanya yake.wakati wenzetu walioendelea wakifikiria 5o to 100 years to come,sisi tunafikiria Leo,Rais wanafikiria miaka kumi ya utawala wake.Asante sana ccm nchi inaongozwa kwa ahadi? Badala ya mgombea kuna na mkakati on how atafanya kutufikisha kwenye ndoto yetu kama taifa? A nakuja na ahadi na mwisho wa siku tunabaki pale pale du.inauma sana
 
Mmmmm!!! Hapa bendera fuata upepo,tunapeperushwa tu tutakapongongeshwa ndo tutafia hukohuko
 
Inaelekea mleta uzi alikwishapotea kitambo. Hajui mbele wala nyuma;kushoto wala kulia, mwelekeo sahihi ni upi. Sasa amesikia sauti ya JPM inamuelekeza amfuate. Kwa kuwa alikwishapotea haamini iwapo huko anakoelekezwa aelekee ni dira sahihi. Ninamshauri amfuate JPM. Kwa kuwa awali alipotea peke yake, sasa akipotea atakuwa na company ya JPM. Ondoa na shaka.
 
Hivi ni sehemu gani, jf, au mitandao mingine naweza pata hoja na mada zinazojibiwa Wa hoja. Maana inaonekana kama huwa kuna watu wanatumwa kujaribu kila mjadala sijuini kwa faida ya nani.

Nitarudi bdae
 
Msgufuli bado anafanya mambo km bado yupo kwenye kampeni!
 
Kiuchumi ni viwanda kuelekea uchumi wa kati
kijamii ni elimu bure hadi kidato cha nne
kisiasa kuna kukamilisha kiporo cha katiba mpya
...................................................
tafsiri ya yote tuanaanza kuangalia bajeti na hotuba za mawaziri bungeni. sema mh! uamue usilala kabisa maana TBC hiyooo usiku wa manane!
 

Tafsiri ya hiyo ndugu Tindo ni moja tu, mada hii imewaudhi wana CCM kwa kuhoji utendaji na uelekeo wa serikali hii ya CCM!!

Afadhali hata Jakaya Kikwete alipoingia mwanzoni mwa utawala wake, ingalau alikuwa na utaratibu wa kuwa anazungumza na taifa kila mwisho wa mwezi kuelezea uelekeo wa sera zake za kiuchumi pamoja na kutoa ufafanuzi wa some burning issues za wakati husika. Kwa mfano ikitokea watu watu wanajiuliza swali km hili la mleta mada kwamba hivi tunaelekea wapi, alijitokeza na kutoa msimamo na kuwaweka watu ktk mstari hata kama ni kwa kuzuga tu!!

However, utamaduni huu nao ulijifia automatic, kwani pamoja na hayo ukosoaji kwa kila alichokuja nacho ulimfuata nyuma yake!

Huyu yeye hata hayuko huko bali ni purely anaenda enda tu, yupo yupo tu kwa ku create matukio yatakayompa publicity. Ukiona kakaa kimya kwa muda flani watu wanaanza kutojua uwepo wake, basi ujue atatafutiwa tukio na mahali ambapo ataibukia huku akiwa ameambatana na camera za TV ili watu waseme,
".....lol....aisee lima - Magufuli bwana, leo kidogo awatumbue ........".

Yes, hivi ndivyo tunavyopelekwa na tunavyokwenda kama taifa

Mimi na wengine nadhani tunatarajia Rais pamoja na kurejesha nidhamu ktk utumishi wa umma, kusimamia makusanyo ya kodi nk tulitarajia sasa aje na mikakati mahususi ya kuijengea misingi imara kwa kuhakikisha kunakuwa na sheria madhubuti zitakazosimamia na kuyaimarisha haya anayoyaanzisha.

Lakini binafsi sioni chochote kwani anapita mule mule walikopita watangulizi wake, na maana yake iliyo dhahiri ni moja tu, ni kuwa hata yeye atachoka na atashindwa tu na atatahamaki 2020 imebisha hodi mlangoni kwake!!

Well and good. Tunaambiwa kuna ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 - 2020 na kwa hiyo tuisome hiyo na ndiyo uelekeo wa Magufuli. Swali kwa hawa wanaosema haya.

Kwani kuna awamu CCM haijawahi kuwa na ilani? Zilileta tofauti gani eti? Mbona ndizo hizo hizo ilani tofauti tofauti za CCM zimekuwa msingi wa malalamiko na majipu haya haya yanayotumbuliwa leo?....This is purely confusion!!
 
Umenivunja mbavu! ungemaliza kwa kutushauri mi na mwenzangu kwamba kupotea njia ndo kujua njia.
 
Kwa mzungusha mikono kama wewe huwezi jua muelekeo wa nchi...subiri 2020 uwazungushie tena mikono
Safiiii jibu lako zuri 2020 tunazungusha mikono Zaid kudaaadeki hakuna tunapoelekea tunazidi kutaabika
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…