Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hivi kama ni kweli kama wanavyodai CCM wenyewe kuwa kazi anayofanya Magufuli imerejesha imani ya Umma wa watanzania na hivyo kufanya wapinzani wakose hoja za kuwaambia wananchi, hebu CCM hao hao niwaulize maswali machache.

1.Ni kwa nini basi CCM hiyo hiyo ina hofu ya kupindukia hadi kufanya Rais Magufuli apige marufuku shughuli zozote za kisiasa zisifanywe na vyama vya siasa vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati chama chake cha CCM akikiruhusu kufanya shughuli zake za kisiasa bila kubughuziwa na Polisi?

2.Kama kweli Umma wa watanzania umerejesha imani kwa CCM kwa asilimia 100 kama ambavyo CCM wanavyotaka kutuaminisha, ni kwa nini basi CCM hiyo hiyo ina hofu kubwa kiasi ambacho haitaki kabisa Bunge lionyeshwe LIVE ili angalau tuwaone hao wabunge wa upinzani ambao CCM wanadai kuwa upinzani umeishiwa hoja?

3.Ni kwa nini yule mdada akiyekalia kigoda kule mjengoni Dom anaonyesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa CCM hadi kusababisha wabunge wa CCM wanawatukana waziwazi wabunge wa upinzani bila kuwachukulia hatua zozote wakati akiwabambikia makosa wabunge wa upinzani ili awatimue mjengoni ili atimize azma yake ya kulifanya Bunge hilo badala ya kutimiza wajibu wake Mkuu wa kuisamamia serikali, badala yake chombo hicho cha kuwakilisha wananchi kigeuke kuwa kama kikao cha NEC ya CCM kwa kuikingia kifua serikali?

4.Ni kwa nini teuzi zote za muhimu za utumishi wa Umma zimegeuka kuwa teuzi za kuwapa 'ulaji' makada wa CCM badala ya kuwa teuzi za kuangalia utendaji wa mtumishi mwenyewe bila kuangalia itikadi yake ya kisiasa kwa kuwa mtumishi wa Umma hapaswi kuonyesha mapenzi yake waziwazi kwa chama chake kwa kuwa utumishi wa Umma ni utumishi kwa watanzania wote na sio utumishi kwa chama chake cha CCM pekee?

Kwa mapungufu hayo ya serikali ya awamu ya 5 na utawala wa kibabe anaouendeleza Mkulu ambao unafanya hali ya uchumi kwa mwananchi kuzidi kuwa ngumu mitaani kunaendelea kufanya wananchi wengi waendelee kupoteza imani kwa serikali hii ya awamu ya 5 kutokana na serikali hiyo kuwafanya wananchi waishi kama mashetani........
 
UPINZANI UNAJIUA WENYEWE KWA KUOKOTEZA NA KULA MIZOGA!!

MAGUFULI ANA KAZI MOJA TU YA KUWALETEA MAENDELEO WATANZANIA KULINGANA NA ILANI YA CCM!
 
Upinzani ufe mara ngapi!???? Au umesahau uchaguzi uliopita mgombea wetu wa uraisi tulimuazima kutoka ccm na mgombea mwenza tulimuazima kutoka cuf, na msemaji wa chadema yetu akatoka nccr? Chezea gia za angani wewe!!!!!
 
Anajifurahisha tu huyo
 
Ajiandae kwa kipigo kitakatifu hapo 2020 maana watanzania tumesha amua kwa umoja wetu kuitupa ccm kwenye dust bin
 
Jamaa ndani ya ccm wanampka mafuta kwa mgongo wa chupa na mwisho wa siku ccm inamfia mikononi
 
Ni kweli kaka. Kama ilivyokuwa upuuzi kuamini kwamba UKAWA watashinda Uchaguzi wa Rais!!
Mimi nilikuwa ni mwana ccm lkn lazima tukubali kuwa kipigo walicho kitoa ukawa kwa ccm kimetuyumbisha sana na sasa ccm inayumba
 
Kwa chama cha upinzani kama chadema hata kwa fimbo siwezi kujiunga sembuse kuchukua nchi
 
UPINZANI UNAJIUA WENYEWE KWA KUOKOTEZA NA KULA MIZOGA!!

MAGUFULI ANA KAZI MOJA TU YA KUWALETEA MAENDELEO WATANZANIA KULINGANA NA ILANI YA CCM!
Kama ccm sasa inavyo okoteza na kupokea oil chafu na makapi
 
Upinzani ufe mara ngapi!???? Au umesahau uchaguzi uliopita mgombea wetu wa uraisi tulimuazima kutoka ccm na mgombea mwenza tulimuazima kutoka cuf, na msemaji wa chadema yetu akatoka nccr? Chezea gia za angani wewe!!!!!
Kama ccm ndiyo ishajifia kabisa ktk mikoa mbalimbali na sasa imebakia na miringoti tu
 
Ni kweli kaka. Kama ilivyokuwa upuuzi kuamini kwamba UKAWA watashinda Uchaguzi wa Rais!!
Una poit mzeya. Yani ni upuuzi kuamini et Ukwa wangeweza kuitoa CCM madarakani wakati tume ya UChaguz ni branch ya CCM. Jeshi la police ni vibaraka wa CCM. Katiba nayo mbovu. Yani upinzani wasipotaka Reform katika Tume ya uchaguz na katiba. Ikuru wataisikilizia kwa jiran.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…