Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hakuna Tume huru ya Uchaguzi Duniani labda iundwe na malaika period!
 
Bado sijaona chochote kilichofanyika awamu hii kumsaidia mtanzania wa hali ya chini badala yake msosi umetoka kwenye mara 3 kwa siku mpaka mara 1 kwa siku.
 

Sio Magufuli au serikali itakayo kuletea maendeleo, ni wewe ndio utakayeleta maendeleo. Magufuli anakufagilia njia, ana ondoa uwizi, ukandamizaji na usmbufu na amefungua milango kwa wawekezaji na hadi sasa kwa miezi minane kumesha kua na mikakati mikubwa kadhaa itakayo anzishwa.
Siko nchini kwa sasa lakini hivi karibuni nimeogea na jamaa zangu huko kila mmoja anakuambia sasa hivi kuna heshima kubwa huko maofisini na bado. Tukijali maslaha na tukaacha malumbano ya siasa tutakuja kupata maendeleo na hayo tunayaona wazi kabisa sasa.
. Tatizo la watanzania wanataka hayo maendeleo wayapate mara mmoja, wakilala usiku na kuamka asubuhi waone maendeleo lakini hawajiulizi wao walifanya juhudi gani ya kuleta maendeleo.
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo tu.
Anakotupeleka hata njiani hakuna pa kununua chakula, na kuchimba dawa ni porini!
Tuombe tusitobozee kismayu
 

Ndugu tatizo la baadhi ya watanzania hasa wanao shangilia siasa kama washabiki wa mpira ndio wasio ona hayo yote. Wao wanachotaka wapate maendeleo na waone kila kitu kine tekelezwa kwa siku mmoja. Na wengine ndio hao wanao omba serikali ishindwe ili wapate la kusema.
 
Kuishi kwingi ni kuona mengi.. sisemi kitu..!
 
Naomba tmakuful



Naomba makufuli arudishe utawala wa kijerumani ukiokota sanduku la pesa upeleke polic
 
Ukipenda kupigiwa makofi na kushangiliwa,ni lazima kwanza uahidi makubwa kama vile kujenga mwezini au chini ya habari,ujaribu kufanya mambo makubwa kama vile kuhamisha bahari, n.k.

Hata hivyo,ukwel ni kwamba,ahadi za aina hiyo ni ngumu kuzitekeleza na hata ukijaribu kuzitekeleza utaishi kujaribu tu na kuharibu na mwisho wa siku mikono hiyo hiyo iliyotumika kukupigia makofi, ndio hiyo hiyo itakayotumika kukuzaba makofi kwa kushindwa kutimiza ahadi zako.

Hili ndio somo letu la leo na mwalimu wako Salary.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…